Amenikimbia kisa nakoroma nikilala

Sikununu

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2015
Posts
341
Reaction score
101
Dah! Inaniuzunisha ila ndio hivo amenikimbia na kuniacha solemba huyu mpenzi wangu kisa tu nakoroma sana.Ilikuwa kama utani mara nyingi ananiambia we sikununu unakoroma sana kama chura mda mwingine mpaka ananiamsha nikiwa usingizini nakoroma kwa raha zangu

Kusema na ukweli nilikuwa na mpango nae huyu binti baada ya kukwaruzana na kuachana na mzazi mwenzangu ambaye tumezaa hila sina mapenzi naye baada ya kunibambikia mimba hivi hivi nikiwa naona mchana kweupe ndipo binti huyu kigori aliponikubali bila hata kutumia nguvu tuishi pamoja.

Nawaomba sana wanawake msitufanyie hivi sisi tunaokoroma jamani.
 

Mh angekuwa mwanamke anakoroma ingekuwaje . Et unakoroma kwa raha zako hahaaaa . Wewe usiku haujishughulishi uko bze unakoroma umesikia mwanamke amewaacha wazaz wake akakufata wewe ili aje akoromewe . Alafu unasema mwanamke amekubambikizia mimba . Sasa unaishi na mwanamke badala ujitume umpe mimba ww unalala tu unakoroma unategemea nini? Pole sana
 
Fanya mazoezi upunguzeni uzito na kukoroma kutapungua,hilo Tumbo mkuu😆
 

Kama unakoroma uwe unalala na nguruwe uache kumdstb mwenzio. hujui km usingizi unahitaji utulivu na ukimya?
 
Uwege unalala na helmet.
 
Hahahahahaha...dogo umenichekesha kinyama!...ati unakoroma kama nini ....??...kwa raha zako mwenyewe!
 
Sasa mtu unakoroma kama punda,utaacha kukimbiwa!
 
Kukoroma usingizini ni disturbance kwa kweli, unastahili kukimbiwa
 
Itakuwa kuna zaidi ya kukoroma. Alipokukubalia alikuwa anatafuta hifadhi ya muda tu.
 
Mtu akiwa anakoroma silali nae karibu, usingizi unapaa kbs
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…