Ameniblock na kuninunia

humility21

JF-Expert Member
Jan 8, 2021
448
620
Wakuu, naomba mnipe tafsiri juu ya jambo hili.

Kuna demu nilikuwa namtokea tokea bahati nzuri kiasi tukawa tunaenda vizuri ktk mawasiliano yetu ingawa kuna kipindi cha hapa mwisho mwisho mawasiliano baina yetu yalipungua sana huyu demu akawa hapokei simu zangu wala kujibu sms zangu lakini mimi sikujali, nikawa naendelea tu kumtumia sms kumsalimia na kumpigia simu hata kama haonyeshi ushirikiano.

Sasa kama wiki 2 zilizopita nilimtumia tu sms moja yenye ujumbe wa tofauti sio ujumbe wa kimapenzi bali ni ujumbe wakuelimisha ambao unamfaa kila mtu kuhusu maisha, baada ya hiyo sms demu akablock namba yangu kwa kuhisi ule ujumbe ulikuwa umemlenga yeye na ni kama nilikuwa nimemkashifu, baada ya hapo nikatumia namba yangu nyingine kumwambia kitendo alichofanya cha yeye kuniblock sio kizuri, vile vile nikamueleza ile sms nilikua nimeituma kwa marafiki zangu wote na sio yeye peke yake, na nikweli niliituma kwa kila rafiki yangu, kwasababu alikuwa ameshaniblock nikaamua kumwambia namtakia kila la heri kwenye maisha yake na yeye akanijibu sawa.

Baada ya wiki moja tangu mimi na yeye mawasiliano yetu yaishe, nilikutana na huyu demu mahali fulani mjini katika pilika pilika zangu za kila siku, baada ya kukutana mikajaribu kumsalimia kumjulia tu ili kumjulia hali ila nikaona mwenzangu ameninunia na pia kunikaushia ingawa wakati tunaachana nilimwambia mimi sina kinyongo na yeye hata kama ameniblock na tunaachana. Sasa zimefika wiki 2 nikiangalia whatsapp naona bado huyu demu bado ameniblock.

Naomba mnisaidie wadau kutafsiri ni kwanini huyu demu ameninunia licha ya mimi kumfafanulia kuhusu maana ya ile sms niliyokuwa nimemtumia na bahati nzuri sms yenyewe haikuwa ya matusi na pia bado nilimwambia mimi sina kinyongo na yeye licha ya yeye kuniblock na mawasiliano yetu kuisha, yaani nikimwonyesha kwamba mimi nina moyo safi tu.

Naomba tafsiri wakuu kwasabu gani huyu demu alininunia nilipokutana nae. Je, sababu inaweza kuwa labda kwakua labda nilimuambia namtakia kila la heri kwenye maisha yake, yaani hakutakuwa na mawasiliano zaidi?
 
Pengine huna pesa

Pengine bado hujitambui

Pengine bado hujakua

Anakudharau

Hakutaki

Wewe ni king'ang'anizi

Hitimisho: Huna sifa anazozitaka na ni wazi kuwa hakutaki. Endelea na maisha yako. Kwani kukublock wewe inakupunguzia nini? Usilazimishe mapenzi hasa mahali ambapo ni wazi hupendwi wala kuthaminiwa.
 
Huna pesa

Hujitambui

Bado hujakua

Anakudharau

Hakutaki

Wewe ni king'ang'anizi

Hitimisho: Huna sifa anazozitaka na ni wazi kuwa hakutaki. Endelea na maisha yako. Kwani kukublock wewe inakupunguzia nini? Usilazimishe mapenzi hasa mahali ambapo ni wazi hupendwi wala kuthaminiwa.
Umegusa maeneo yote muhimu
sitegemei kama kuna ushauri mwingine zaidi ya huu
Labda tu kwa kupigilia msumari

Usijiulize kwanini huyo dada kawa hivo bali jiulize kwanini umekubali kuwa kwenye kundi la wanaume/wavulana maboya.
 
Huna pesa

Hujitambui

Bado hujakua

Anakudharau

Hakutaki

Wewe ni king'ang'anizi

Hitimisho: Huna sifa anazozitaka na ni wazi kuwa hakutaki. Endelea na maisha yako. Kwani kukublock wewe inakupunguzia nini? Usilazimishe mapenzi hasa mahali ambapo ni wazi hupendwi wala kuthaminiwa.
Sijamaansha Mimi ni king'ang'anizi, nimeomba tu tafsiri ya kitendo cha yeye kuninunia
 
Unawataka wanawake mabinti yaaan wanaojiita pisi kali, ??

Hawa wananjaaa, hawana Kazi, wamemaliza chuo, labda bado ni wana chuo, labda anakazi ila pesa haijawah mtosha mtu, labda tu kana maisha ya mbwbwe




Get the money

Get the Power

Get the Women .
 
Back
Top Bottom