Rejea siku za mwisho. Maneno ya Mungu yako wazi kabisa: Watakuja mashahidi wa uongo, wengine mpaka watasema wao ndio Yesu, watu wenye kujipenda wenyewe, watu watapenda sana fedha..., wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana (Kama baadhi humu jf), wasiotii wazazi wao, wasiowapenda wakwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu, wenye mfano wa utauwa lakini wakikana nguvu zake. Ni budi kwa kila mmoja kuzipima nguvu zinazojitokeza nyakati hizi. Iwe ni katika ukristo au katika uislam. Mashetani na mapepo yanazidisha kasi ya kupingana na Mungu huku wakijitahidi kuonyesha kuwa wana uwezo ule ule alio nao Mungu. Nyakati hizi wamezuka wahubiri wa aina mbalimbali waliojipachika uaskofu, unabii, mitume, watu wenye upako nakadhalika. Ni vizuri kuzipima nguvu hizi kabla ya kuzishabikia kwa sababu zina vielelezo vyote vya dalili za kuwadia kwa siku za mwisho. Jambo la mtu kufa na kukufuliwa kwa njia yeyote lisingekuwa jambo la minong'ono bali lingekuwa ni jambo la mastaajabu na muujiza ambao ungepelekea watu kumininika kama walivyomiminika kwa babu wa loliondo ingawa kwa babu nako kuna maswali mengi ya kujiuliza yanayokosa majibu bado.