Amebakwa msaada wa kisheria jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amebakwa msaada wa kisheria jamani

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by commited, May 20, 2012.

 1. commited

  commited JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  habarini za asubuhi ndugu zangu, bila shaka kwa uwezo wake maulana wote hatujambo.
  Ni mejitokeza hapa kupata ushauri ili nami nikautoe sehemu ili kuhakikisah haki inapatikana,

  kuna mdogo (binti miaka 20) wa jamaa yangu amebakwa hapo maeneo ya arusha majuzi alhamisi usiku (17/05 2012) mida ya sa mbili usiku, alitumwa sehemu akachukue maziwa, kwa bahati mbaya wakati anapita sehemu ambayo kiasi kuna giza, akatokea mtu (kijana wa kume) akamziba mdomo na akamtolea kisu kisha akambaka. Sasa kwa bahati mbaya huyu binti ambaye ni mdogo wa jamaa yangu anasema huyo kijana aliyemfanyia huo ukatili hamjui jina ila kwa sura anamtambua kuwa wanaishi naye hapo mtaani, ni mara kadhaa huyo mbakaji amewahi kumtongoza huyo binti lakini huyo binti (aliyebakwa) amekuwa akimkataa.

  Ugumu wa hii ishu unakujaje, huyu binti baada ya kubakwa tangu hiyo alhamisi usiku alivyobakwa hakusema, zaidi ya kushinda ndani na huku akilia, mpaka jana jumamosi asubuhi wazazi walipomuhisi anatatizo, kumuhoji ndio akaeleza hayo niliyoeleza
  maswali,
  1. Wazazi hawana uwezo wa kiuchumi, sasa wanaanza kuhofia kuwa wakienda polisi then mahakamani, inaweza kuwa gharimu pesa nyingi ambazo wao hawana
  2. Wanahisi hawatakuwa na nguvu ya kisheria kwa kuwa ule ushahidi halisi wa labda majimaji ya mbegu za kiume hayapo tena kwa sababu huyo mbakwaji tayari ameshaoga
  3. Na kwa mujibu wa maelezo yaliyopo inahisiwa huyu binti ameingiliwa siku mbaya ambazo inawezekana atakuwa anaujauzito

  sasa ndugu zangu naomba tusaidianae mawazo kwa sababu naamini humu kila mtu anamazo tofauti, lengo ni kusaidia kama huyu binti anaweza bado kwenda mbele ya vyombo vya sheria, na je kama bahati mbaya akapimwa akautwa tayari ana mimba au virusi vya ukimwi ni nini cha kufanya..
  Karibuni kwa ushauri na maoni, tukio limetokea alhamisi usiku.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Mahakama za Tanzania hakuna haki kama huna pesa, mshauri mbakwaji aende kwa mganga akalipize.
   
 3. commited

  commited JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bujibuji asante mkuu, lakini unadhani ni hilo tu analoweza kufanya? Tuwe serious kidogo mkuu fikiria angekuwa mwanao, au ndugu yako ungefanyaje mkuu.. Karibu
   
 4. commited

  commited JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  wakuu karibuni kwa michango yenu muhimu, bujibuji unaweza kurudi tena kusema chochote?
   
 5. Bigjahman

  Bigjahman JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Dih:A S embarassed:
   
 6. commited

  commited JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu bigjahman.. Karibu japo useme chochote mkuu, tunakzi kubwa sana kuwalinda watoto wetu wa kike kwa ujumla, karibu mkuu
   
 7. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Aisee hili ni tukio serious......maaadam mbakaji anajulikana hebu nenda kituo cha msaada wa kisheria ama TAWLA chama cha wanasheria wanawake watampa msaada wa kisheria bila tatizo...tena kama ishu kama hii wako fasta sana

  Sijui kwa Arusha wako mitaa ipi ila jaribu ku-google utafute adress zao na au uwapigie............Fanya hivyo mkuu na mwenyezi Mungu atakuzidishia....leo kwa mdogo wa rafiki yako kesho kwako.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Hakika ndicho ambacho ningefanya, mahakamani na kwenye vyombo vya sheria haki hamna, kimbilio hamna, dawa ni moja tu street justice
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Ukienda huko utaambiwa umesha haribu ushahidi na uthibitisho
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,847
  Trophy Points: 280
  Dah! mimi nampa pole sana huyo binti nafikir hakuna jinsi hapo manake akienda polis kna mambo ambayo hayatakuwa na msaada hasa wa kiupelelezi. cha msingi kabisa binti akapimme maambukizi the soonest kisha baada ya miez 3 apime tena. pia apime na mimba kama anayo sisemi vibaya ila ni bora akaitoa manake kuwa na mtt ambaye hutakuwa na raha naye kwangu mimi ni msalaba manake kila siku utakuwa unamkosa mungu so ni bora ukaitoa ili uwe na dhambi ambayo utatubu na itaishi. kuhusu huyo kijana aachane naye manake atakujazia gharama ambazo zitakugharimu. ingekuwa hakunaga rushwa basi ningemshauri aende polis kijana atiwe ndani lakin hapo utaona akienda leo kesho katoka sasa hadi inaudhi.
   
 11. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo huli kwa sababu vyakula vingi na TBS wanachakachua............
  Huoi kwa sababu kuna wanawake waongo
  commited nenda tu ...........usikate tamaa...ushahidi hautegemei jambo moja tu............lakini pia at least mbakaji ajue kwamba watu hawataki mchezo...la sivyo atarudia tena
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi navyo juu mtu akibakwa mnaweza mkamjua mbakaji, hata ziwe zimepita siku kama hajaguswa na mwanaume mwingine...Navyo elewa mimi baada ya ku sex, sperm zitakuwa zimeisha ingia kwenye uterus (they’re fast swimmers) and washing the vagina won’t help...Poleni sana nendeni police mkafungue file ili mka mchukue kwa uchungzi wa kumpima mtamshika tu hana ujanja.
   
 13. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Dah! kweli huu ni ukatili wa hali ya juu. hivi hawa wanume ni bangi au kitu gani mpaka kutishana kwa visu sababu ya ngono ambayo wataiita mapenzi, tena bila kupendwa.
  Kwanza nataka nikilaani kwa laana zote za rohoni na mwilini kitendo hiki, na hasa huyo aliyekitenda, alaaniwe pia.
  Pili, nashauri kwanza huyo dogo apelekwe hospitali, ili akapate japo uchunguzi. kweli kunaweza kuwa na gharama, lakini naamini hospitali nako kuna watu siyo wanyama, so wanaweza kuwa resonable na wakamsaidia, ilimradi tu ajieleze vizuri. (Mfano mi nishawahi kusaidiwa hapo kcmc, nilikuwa na mdogo wangu - RIP - alikatwa mguu kwasababu ya kansa ya mifupa, so wakati nahangaika kumtafutia mguu wa bandia, nikakuta iko ghali sana, basi nikajieleza vizuri tu kwa dr hapo, alinisaidia sana maana alinipinguzia zaidi ya laki 6, by then 2007. Bahati mbaya dogo alifariki muda kidogo baadaye)
  Tatu mkuu, dogo akapate ushauri nasaha, maana atakuwa ameathirika sana kisaikolojia. kuna washauri wengi tu ambao wanaweza kumsaidia bila fedha. mfano kanisani au msikitini kwake, kwenye vituo vya jamii vya ushauri (social, and community councelors) ambavyo vipo idara za ustawi wa jamii wilaya au mkoa, hata hospitalini kwenye vitengo vya ushauri nasaha.
  mwisho kaka, akatafute haki yake mahakamani. Mungu ndiye mgawa haki, lakini hawezi kuingilia kati bila yeye kwanza kufanya juhudi za mwanzo. aende poilisi, kisha mahakamani, na hapo ndipo Mungu atampigania. mimi ni mkristo, so kwa imani yangu naamini Mungu huvumilia makos na dhambi nyingi, lakini si hii ya uzinzi, uasherati (sodoma na gomora ziliangamizwa baada ya watu wake kutaka kuwabaka malaika; gharika la nuhu ilikuja baada watu wake kukithiri kwa matendo kama hayo, ni mifano tu) kwahiyo awe na uhakika kuwa Mungu atampigania, atamfanyia mlango wa kuotkea.
  aende kwa wanasheria, au vyama vya misaada ya kisheria, kama wameweza kujitolea kumtetea Lulu, je, si zaidi sana kwa huyu ndugu?!
  nawasilisha mkuu, na poleni sana tena
   
 14. commited

  commited JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Platozoom, na wakuu wote hapo juu pamoja na bujibuji nashukuru sana kwa michango yenu.. Lakini kwa kweli hali inasikitisha sana, sasa kama vyombo kama polisi ndio tulitegemea viwe kimbilio la wanyonge.. La ndio hivyo tena kama huna kitu... Imenitach sana wakuu kwasababu haya matatizo yapo sana na yanachangia wimbi la watoto wa mitaani, na watu kuambukizana ukimwi... Nashukuru wakuu mungu awabariki sana
   
 15. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hao wazazi'wanahisi' vitu vingi sana. Kwa nini wasifike kwanza mahakamani kupata uhakika wa kiwango cha pesa kinacho hitahitajika? Sina uhakuka ila nadhani haiwezi kuchukua ressource nyingi kufungua mashtaka. Bila kujua wanahitaji ngapi hawawezi kujipanga, hawawezi hata kupata msaada toka kwa jamii (in case they decide to ask for financial help)
  Kuhusu suala la ushahidi, wakumbuke kua ushahidi wa ubakaji unapatikana kwa namna nyingi, sio kwa kuwepo kwa zile mbegu tu. Ningewashahuri wafike kituo cha polisi haraka iwezekanavyo. Baada ya kituo cha polisi wafike pia hospital ambapo atapewa post exposure profylactic treatment ya kuziwia ukimwi na pills za kuziwia mimba.
   
 16. commited

  commited JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mkuu bhikola, nakushukuru sana ubarikikiwe ubarikiwe sana, in asikitisha naona dunia imnakwenda mwisho, kwa stahili hii tutaambukizana ukimwi na kuzidisha umaskini, tena kwa bahati mbaya ni mwanafunzi huyo binti.. asanteni sana mkuu, ngoja ni wagoogle TAWLA KUJUA HAPO ARUSHA WAKO WAPI NIMWELEKEZE JAMAA KESHO J3 WAENDE, FAMILIA YAKE NAYO IMECHANGANYIKIWA, NA HUYO BINTI YUPO KWENYE WAKATI MGUMU ANAOGOPA HATA KUTOKA NJE, ASANTENI SANA WANDUGU
   
 17. commited

  commited JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  RoussianRoultte asante sana ndugu, nimefarijika kwa comment yako, ngoja niwashee nao hizi comment zawadau wote tuone cha kufanya, nakushukuru sana ndugu, hapa ndipo jamii yetu ilipo fika .. ni pagumu sana
   
Loading...