Ameanza Mbwana Samatta, bado wengine wanasubiri pongezi za serikali

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Ilikuwa ni jambo la kuwatia moyo wanamichezo, wakati Mbwana Samatta alipokuwa ndio habari ya wiki nzima, baada ya kupata tuzo ya mchezaji bora wa ndani wa bara la Afrika. Kuanzia Mwenyekiti wa CCM Taifa mpaka mashabiki wa soka wanaotoa mawazo yao pembeni ya mafundi viatu wa mijini, hakuna aliyeacha kumsifia Samatta na Mafanikio yake.

Lakini mwanamichezo anayefanikiwa huwa na hadithi ndefu nyuma ya mafanikio yake. Namuona Mbwana Samatta kama mwanamichezo aliyeibuka kibahati bahati na kwa sababu Baba yake ni mtu mwenye nidhamu na mtazamo wa mafanikio, akapata bahati ya kusimamiwa vizuri tangu akiwa nyumbani Mbagala. Wapo vijana wengi ambao hawawezi kuwa na bahati kama ya Samatta, ya kulelewa kwa nidhamu ya hali ya juu kama mwanamichezo. Hawa wanahitaji kufikiwa na serikali. Maana yangu wizara ya michezo ijipange kwelikweli ili kila taasisi inayoshughulika na michezo iweze kuzalisha kina Samatta wengi kadri iwezekanavyo. Hapo ndipo penye changamoto, kuna mahitaji ya walimu wengi wa michezo, kuna mahitaji ya ujengaji upya wa nidhamu ya uongozi katika ngazi mbalimbali za taasisi za michezo.

Yapo mengi ya kufanywa na wizara ya michezo. Didier Drogba ameajiri watu wengi wa Ivory Coast kupitia miradi yake. Nwankwo Kanu kaajiri wanigeria wengi sana kupitia miradi yake. Kwanini Samatta na wanamichezo wengi watakaofanikiwa kimataifa wasje kuchangia ukuaji wa uchumi kwa kuongeza ajira mbalimbali?. Natumani Waziri Nape Nnauye ameshafahamu ukubwa na ugumu wa kazi inayoikabili wizara yake. Samatta ametoa ajira kwa kampuni zilizojenga nyumba zake, bado hajaanzisha miradi mbalimbali itakayogusa kwa ukaribu kabisa maisha ya wakazi wa Mbagala. Bado hajajenga mahospitali na shule za kukuza vipaji vya soka, ambazo zitaajiri watu wengi sana. Na mafanikio ya kiuchumi ya Mbwana Samatta yatakuwa ndio kichocheo kwa vijana wengi kufikiria ni jinsi gani wanavyotakiwa kutoka jasho na kujituma ili waweze kufika mbali.

Serikali ya awamu ya tano isiishie tu katika kuyapongeza mafanikio ya Mbwana Samatta, ijipange katika kuhakikisha kina Samatta wengi zaidi wanajengewa mazingira sahihi ya kufika mbali. Natumaini wataalam wanaofanya kazi chini ya uongozi wa waziri Nape Nnauye watayasoma mawazo yangu.
 
Nafikiri na yule Mtanzania anayecheza basket ball USA naye amefanya vitu vyake kuwainua watanzania!
 
Back
Top Bottom