Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Thabit Madai

Member
Oct 8, 2024
52
138
IMG-20241008-WA0046.jpg

Na THABIT HAMIDU, ZANZIBAR

Bahati Issa Suleiman 51, Mkaazi wa Kikungwi Mkoa wa Kusini Unguja alikuwa mgombea wa nafasi ya Udiwani wadi ya Bungi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Bahati ambae pia ni mwanaharakati wa kupinga vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na watoto simulizi yake ya pekee inaeleza changamoto alizopitia katika harakati za kuwania nafasi ya uongozi na kubainisha sababu zilizomkwamisha kutimiza ndoto zake.

Bahati alianza harakati za kisiasa mwaka 2015 mara baada ya kupatiwa mafunzo na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tamwa -Zanzibar ambapo aligombea nafasi mbaalimbali ndani ya chama cha Mapiduzi CCM.

"Sikuweza kukata tamaa hata kidogo licha ya kuwa kila nafasi ambayo nilikuwa nikigombea naikosa, maneno ya kukatishwa tamaa na mitazamo potofu katika jamii inayonizunguka ni changamoto ambazo nilikuwa nakabiliana nazo takribani kila siku katika harakati zangu za kuwania nafasi za uongozi,"Anasema Bahati.

Anaendelea kusimulia kuwa, moja ya sababu iliyomkwamisha kushika nafasi ya uongozi na kuwa kuwamisha wanawake wengi ni pamoja kutokujiamini kwa wanawake.

"Sisi Wanawake ni wengi katika mchakato mzima wa uchaguzi lakini tunashindwa kujiamini kugombea, kuwaunga mkono wale wanawake ambao wamejitokeza kugombea na hii inatokana na kuwa sisi wenyewe hatujiamini na hatuamini kama mwanamke anaweza kuwa kiongozi mzuri katika jamii," Bahati anaeleza.

"Wakati nagombea sikuweza kupata uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa na wanawake wenzangu na hapa nilibaini kuwa mitazamo yao ni potofu juu ya mwanamke kuwa kiongozi lakini sikuwez kukata tamaa hata kidogo na bado nina ndoto ya kuendelea kugombea hadi pale ntakapo kuwa kiongozi,"Amemaliza Bahati.

Wakati Zanzibar inaendelea kusukuma kwa kasi agenda ya Dunia ya 50 kwa 50 kati ya Wanaume na wanawake katika uongozi, nchi kama Rwanda tayari imepiga hatua na kufikia 60 kwa 50, Huku 60 wakiwa wanawake na 50 wanaume na ile hoja kwamba Wanawake hawawezi kuongoza ni dhahiri kuwa si sahihi.

12.jpg
Jumla ya wapiga kura milioni 29.1 wa Tanzania kati yao Zanzibar ni 566,352 waliwachagua viongozi waliogombea urais, uwakilishi, ubunge na udiwani kwa vyama mbalimbali vya siasa vilivyogombea uchaguzi.

Kwa mwaka 2020 wa uchaguzi mkuu mchakato wa kuwania nafasi za uongozi majimboni kwa wanawake ulihamasika mno kiasi kwamba wanawake wapatao 300 walijitokeza kwenye vyama mbalimbali vya siasa hasa vyenye ushindani mkubwa hapa Zanzibar.

Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa Visiwani Zanzibar Almas Mohammed anaeleza vikwazo vinavyowakabili wanawake kwenye uongozi ikiwemo, Mitazamo hasi,Majukumu ya nyumbani, ubaguzi wa kijinsia, Kukithiri kwa mfumo dume katika siasa na hata Serikali na hata kukosekana kwa uungwaji mkono ndani ya vyama na katika jamii.

"Hizi ni baadhi tuu ya changamoto ambazo zinawakabilia wanawake kushika nafasi za uongozi ambapo jamii inapaswa kuondokana na mitazamo potofu ya kuwa Mwanamke hawezi kuongoza kwani dunia ya sasa tunashuhudia viongozi Wanawake na wanafanya mambo makubwa kuliko Wanaume," Amehatimisha Almas.

Kwa mujibu wa ripoti ya Maalumu ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 iliyotolewa na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar – TAMWA –Z inaeleza kuwa,kupitia nafasi ya uwakilishi kwenye majimbo 50 ya Zanzibar wanawake ni nane tu, pia wabunge wanaowakilisha Zanzibar wanawake ni wanne tu,Mawaziri wakiwa ni sita sawa na asilimia 33 na Makatibu wakuu ni saba sawa na asilimia 39.

Kwa upande wa Wakuu wa Mikoa mwanamke ni mmoja tu sawa na asilimia 20, Wakuu wa Wilaya ni wanne sawa na asilimia 36 na Masheha wanawake ni 68 sawa na asilimia 17 kwa masheha wote ambao ni 389.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-Z) ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali ambayo imejikita kuwatetea Wanawake na Watoto, jukumu lao kubwa kuhakikisha Tanzania bara na Visiwani kuna usawa wa kijinsia, Dkt Mzuri Issa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa Zanzibar amesema moja ya changamoto ambayo inawakwamisha Wanawake wengi kushika nafasi ya uongozi na kufikia 50 kwa 50 Zanzibar ni kukosa rasilimali fedha.

“Rasilimali fedha huwafanya Wanawake wengi na hata vijana kushindwa kufikia malengo yao ya kuwa viongozi wa kisiasa, tuna wajibu wa kupigania kuwainua Wanawake kiuchumi ili waweze kufikia melengo yao ya kuwa viongozi na kufikia agenda 50/50” Amemaliza Dkt Mzuri.

Tunu Juma Kondo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT) amesema changamoto za wanawake wenyewe kutokufahamu kuwa wanahaki ya kugombea nafasi ya uongozi

"Watu wetu kwa muda mrefu walikuwa wanadhani kuwa nafasi za uongozi ni nafasi za watu maalum hivyo muamko ulikuwa mdogo wa wao kujitokeza kugombea na kuwa changomoto ambayo inarudisha idadi ya Wanawake kushika nafasi za uongozi," Amesema.

Sheria ya vyama vya siasa nchini namba No.5 ya mwaka 1992, sura ya 258 inaweka sharti kwa vyama vya siasa nchini kuhakikisha usawa wa kijinsia katika kuandaa na kutekeleza sera zake.

Utafiti uliofanyika mwaka 2013 uliofanyika na wadau kutoka vyama 16 vya siasa nchini Tanzania pamoja na wanasheria umebaini kuwa bado kuna changamoto ya utekelezaji wa sheria hiyo kutokana na baadhi ya vyama vya siasa kutoweka mazingira wezeshi wagombea wanawake.

Thabit Idarous Faina ni Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar - ZEC amekiri kuwepo kwa changamoto zinazowakabili wanawake kufikia nafasi ya uongozi huku akieleza kuwa Tume ina sera jumuishi ya jinsia ambayo inalenga kuhamasisha jinsia zote kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
 
Kuna baadhi ya jamii zinaamini kwamba mwanamke ni kama chombo cha starehe kwa mwanaume , kuzaa watoto na kuwalea tu ! Hata kwenda dukani , sokoni ni kosa ! Kuna baadhi ya nchi zilizo chini ya Islamic sharia, mwanamke haruhusiwi hata kuendesha gari, kuwania uongozi, kucheza mpira, au hata kufanya shughuli za kijamii kama uzalishaji n.k ! Dah !







Huu ni upuuzi uliotukuka
 
Back
Top Bottom