Amcharanga mapanga mkewe kisa kutokuzaa

Amcharanga mapanga mkewe kisa kutokuzaa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,163
Reaction score
11,230
attachment.php

MTU mmoja mwanamume, aliyetajwa kwa jina la John Weghai amemjeruhi vibaya mke wake, Anastazia John (18) kwa kumkatakata na mapanga kwa kile kinachodaiwa kuchelewa kwake kupata ujauzito, katika maisha ya wawili hao waliyoanza Februari mwaka jana.

Mwanamke, Anastazia John (18) anayedaiwa kucharangwa mapanga na mume wake, John Weghai.

Tukio hilo la kinyama lilitokea katika Kijiji cha Mariba, Kata ya Mriba, wilayani Tarime mkoani Mara na majeruhi huyo amelazwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji ambapo ameshonwa nyuzi 67.

Akizungumzia tukio hilo, msichana huyo alisema kuwa mumewe amekuwa akimpa matatizo mengi katika ndoa yake kiasi cha kumkosesha amani kwa kumpiga mara kwa mara akimtuhumu kuchelewa kupata ujauzito.

"Kwa kweli nimekuwa nikipata mateso makubwa tangu niishi na mwanaume huyu, nimekuwa nikipigwa mara kwa mara sababu nachelewa kupata mimba na yeye anataka mtoto.

"Naviomba vyombo vinavyotetea na kusaidia matatizo ya ukatili kama haya viweze kusaidia watu wanaofanyiwa maana yanaondoa utu wa mtu na kumfanya kuishi kinyonge,"alisema Anastazia.

Alisema siku hiyo alipata majeraha makubwa katika began a titi lake la kushoto, kitu kinachompatia maumivu makubwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Valeria Msoka, alisema wamesikitishwa na tukio hilo, akisema ni ukatili uliopitiliza lakini wataendelea na jitihada za kupambana na matukio ya namna hiyo katika jamii.

Alisema muda mfupi tu umepita tokea warejee kutoka wilayani Tarime wakiwa na ugeni mkubwa wa kimataifa kupambana na masuala ya ukatili na kutoa ujumbe kwa wananchi juu ya athari zake lakini kuna watu hawajabadilika.

"Tulitoa maoni kwenye Katiba mpya inayopendekezwa na tunashukuru yamepita juu ya kuangaliwa upya kwa sheria ya wanaofanya makosa ya ukatili kwenye jamii huenda ikaja kuwa suluhisho juu ya matukio haya,"alisema Msoka.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Kanda maalum ya kipolisi Tarime/Rorya limesema mtuhumiwa bado hajakamatwa na jitihada za kina zinaendelea kufanywa ili kuhakikisha anakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kaimu Kamanda wa Tarime/Rorya, Sweetbet Njwewike alisema katika tukio hilo lililotokea Januari 22 mwaka huu lilichelewa kutolewa taarifa jambo ambalo limechelewesha kupatikana kwa mtuhumiwa.

Tukio hilo limetokea siku chache tu tokea mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Graca Machel kuwepo wilayani Tarime, akihamasisha kampeni ya kuepuka ukatili kwa watoto na akina mama.

Chanzo: GPL
 
Attachments

  • JF Mapanga.png
    JF Mapanga.png
    110 KB · Views: 7,759
Huu ndio ujasiri wanaojivunia vijana wa kanda ya ziwa.......ujasili ambao unamuongezea matatizo na mabalaa badala ya neema....ujasiri ambao utamfanya aishi maisha ya digi digi maisha yake yote....ujasiri ambao ambao matumizi yake mpaka ndege wanamcheka....
 
Mkuu inakuwa vipi unatutuhumu vijana wa kanda ya Ziwa kwa makosa ya mtu mmoja?

Hizi tabia ni hulka za mtu mmoja mmoja na sio kundi la watu.

Siungi hoja suala la kumsurubu mkewe kisa kutokuzaa,huu ni ukatili mkubwa sana ambao baadhi ya ndugu zetu wakurya wanaufanya kuumiza wanawake.Hatua stahiki inabidi zichukuliwe huyu firauni apambane na mkono wa sheria.
 
Takwimu zinaonyesha kuwa katika kila vijana kumi wa kanda ya ziwa sita kati yao wana ugonjwa wa akili na watatu kati yao ni wendawazimu na mmoja tu ndiye mzima..unaweza ukaona ni jinsi gani kucheleweshwa kwa kujengwa kwa hospitali ya vichaa kanda ya ziwa kunavyoleta madhara kwa jamii ya kanda ya ziwa hasa wanawake maana ndio wahanga wakuu wa vitendo vya kijasiri vinavyofanywa na hao wagonjwa wa akili wa huko....
 
Si kwamba nawatuhumu bali ndio hali halisi ya vijana wa huko ambao kila kukicha wapo hapa wanajisifia ujasiri ambao unawaangamiza wanawake wa huko...baaada ya kuonyesha huo ujasiri kwenye mambo ya msingi kama kilimo ili muondokane na umasikini kama sio ufukara..........
 
Hatakama nchiyetu hatuna ukabila ila hawajamaa wa tarime no,sioi wala sitapenda mwanangu aolewe mwana kakushinda yanini mangum? muache tafuta yule uonaye hana tofauti kupiga yanini
 
Takwimu zinaonyesha kuwa katika kila vijana kumi wa kanda ya ziwa sita kati yao wana ugonjwa wa akili na watatu kati yao ni wendawazimu na mmoja tu ndiye mzima..unaweza ukaona ni jinsi gani kucheleweshwa kwa kujengwa kwa hospitali ya vichaa kanda ya ziwa kunavyoleta madhara kwa jamii ya kanda ya ziwa hasa wanawake maana ndio wahanga wakuu wa vitendo vya kijasiri vinavyofanywa na hao wagonjwa wa akili wa huko....

Ni bange mkuu, wanavuta sana mpaka wanakuwa wendawazimu.
 
Ndio sababu kuna watu wanadai sisi waafrika bado tupo kwenye evolution process!.

Lakini pia kuna majuha ambao wana upofu si tu wa macho bali hata wa akili.

Tukio kama hili likitokea huko Ulaya na Marekani wanaanza kutoa maoni kama vile hilo tukio haliwezi kutokea kwingine duniani.

The human condition is the same all over.
 
hivi kwn Tarime kuna mzizi gn usiong'oleka too much kila cku wao tu.
 
Makabila mengine ni laana kabisa, yaani huko tarime kila kukicha huyu kaua mke yule kaua mtoto yule kaua ng'ombe wa mwenzake yaani ni sarakasi mtindo mmoja, au huenda hawa sio watz ni watu wa sudani kusini, maana hawatabiriki, pole majeruhi.
 
Back
Top Bottom