Amcharanga mapanga mkewe kisa kutokuzaa

Amcharanga mapanga mkewe kisa kutokuzaa

......huyo mwanaume ni zaidi ya shetani,miaka 18 ni binti mdogo alitakiwa awe high school. Inasikitisha kwa kweli!
 
Hawa watu sijui wakoje, huu ukatili hadi lini ???? kila siku wanawake kadhaa wamefanyiwa ukatili, ebu kuweni na huruma ninyi wanaume, kama unavyoweza kumuonea huruma dada yako uliyezaliwa nae vivo hivo muonee huruma mkeo. sijui tuwalilie na machozi ya aina gani ili muache kututendea ukatili.
 
maskini mwweee....ndoa yenyewe mwezi huu inafikisha mwaka mmoja loooh.....kazi ipo kweli....hapo ukute mwanaume hata hajui kama yy huenda ndio chanzo cha mkewe kutopata mimba
 
Hawa jamaa ni wajinga tatizo wana miguvu hawana cha kufanyia
kanda ya ziwa hakuna wanaume kuna cannibals
 
Hawa watu sijui wakoje, huu ukatili hadi lini ???? kila siku wanawake kadhaa wamefanyiwa ukatili, ebu kuweni na huruma ninyi wanaume, kama unavyoweza kumuonea huruma dada yako uliyezaliwa nae vivo hivo muonee huruma mkeo. sijui tuwalilie na machozi ya aina gani ili muache kututendea ukatili.

Ndugu hao hata si watu ni wanyama, watu hatuko na roho za aina wengi wao hata ukiangalia sura zao utaona zinafanana na kina nani zaidi
 
Hawa jamaa ni wajinga tatizo wana miguvu hawana cha kufanyia
kanda ya ziwa hakuna wanaume kuna cannibals

Mkuu umezingatia nini kusema kanda ya ziwa hakuna wanaume? Unafahamu kama kanda ya ziwa ni zaidi ya Tarime na mkoa wa Mara? Watendee haki wanaume wanaoishi mikoa hiyo nadhani umewakosea sana. Dar INA machangudoa wengi lakini hatusemi dar hakuna wanawake, kumbuka huwezi kubeba dhambi ya mwenzio imeandikwa na nadhani ni sahihi kila mtu atabeba mzigo wake.
 
mikoa yote ya kanda ya ziwa wengi ndio zao mkuu hutaki unaacha
 
mikoa yote ya kanda ya ziwa wengi ndio zao mkuu hutaki unaacha

Unaposema ni wote unakosea saana mkuu, tatizo ni huo mkoa huo, mmoja. Ni watu wa kughecha ndivyo walivyo, wao wanaona eti ujasiri uliochanganyika na upendo.
We unaona cha ajabu hata wake zao wala hawawezi kaondoka!! Anaweza kukatwa viungo karibu vyote lkn haondoki ng'o.
 
Mkuu inakuwa vipi unatutuhumu vijana wa kanda ya Ziwa kwa makosa ya mtu mmoja?

Hizi tabia ni hulka za mtu mmoja mmoja na sio kundi la watu.

Siungi hoja suala la kumsurubu mkewe kisa kutokuzaa,huu ni ukatili mkubwa sana ambao baadhi ya ndugu zetu wakurya wanaufanya kuumiza wanawake.Hatua stahiki inabidi zichukuliwe huyu firauni apambane na mkono wa sheria.

chachu ombara;
Kama kweli weye umetokea kule kwetu, sidhani ka unamaanisha maneno yako. Mila zetu haziruhusu hayo maneno yako. Hivi huyu mwanamke akimfunga mumewe, mahari nnani atayarudisha?? Ni weye chachu ombara au nnani??
Kikurya tunasema; Anaharibu mahari yake mwenyewe. Hivi nikuulize, mtu akila bazoka yake alio nunua dukani utamwuliza?? Mwanamke wa Kikurya hapo anaraha moyoni kuwa kweli mume wake huyu anampenda sana. Anataka ampe mtoto ili azidi kumpenda.
Ushauri wangu kwa huyu mwanaume ni kuwa miaka 18 bado saana tu. Amtunze vizuri huyu mke na atamzalia Mamura wengi tu. Asiogope, muda bado upo. Warudiane na wasidi kupendana. Tunasema; Ndakughecha harafu, tuhanjanee.
Sasa atampenda kweli kweli muke wake huyo. Sirikari isiingirie hata maisha yetu na muke niriye ripa mahare. Ntakutuna kituri mbane.
 
nilipo soma tuu ujumbe juu yan title fikra zangu moja kwa moja zilinipeleka Tarime
 
naona wakuria tunatukanwa sana humu ndani naomba heshima iwepo Tafadhali kosa la mtu moja moja si la watu wote tafadharini sana tusidhalilishane
 
nadhani umefika wakati wa kuwapa adhabu kali hawa jamaa. wamejaa kiburi na wanajisifia kwa ukatili na unyama huu wakidhani ndio maisha.
 
Hii mijitu inashindwa kabisa kuelewa kuwa hata wanaume wanaweza kuwa ndio chanzo cha kutozaa,wapo na ni wengi sana,sio wanawake tu ambao ni wagumba hata wanaume pia.
 
Back
Top Bottom