Amboni Tanga: Askari Polisi, JWTZ wapambana na majambazi wenye silaha nzito za moto

Mpuuzi Yeriko Nyerere bado anaendelea kumwaga mropaganda zake za kipuuzi

Hii kitu ameleta Yeriko ndio yenyewe. kila siku tumekuwa tukipiga kelele jeshi la polisi kutumika na ccm kuleta propaganda na kuacha weledi wa kazi yao. Leo hii unatarajia watu wawaamini tena na kuwapa ushirikiano kwa jambo kama hili.Siku zote wamekuwa wakiwahusisha wapinzani na ugaidi wa kutungwa kwa kushirikiana na viongozi wachovu wa ccm leo hii ama kuna ugaidi kweli ama uongo kama kawaida yenu nani atawaamini? Kwa hapa tulipofikia jeshi la polisi litegemee ushirikiano toka kwa chama cha ccm kwani limeacha kazi yake ya kulinda raia wa nchi hii bali kulinda maslahi ya ccm. Hili litakuwa fundisho na wangalau litalifanya jeshi la polisi kutekeleza wajibu wake na sio kusubiri amri toka chama cha mapinduzi jinsi ya kutekeleza wajibu.
 
Ccm wanatengeneza movie ili baadae wawahusishe UKAWA, tumia akili yako ya kawaida gaidi hawezi kwenda kuonesha magaidi wenzie walipo hata kwa kurogwa labda awe kibaka, toeni upuuzi wenu hapa(ccm siyo mleta mada)

Mkuu haya mambo tusiyahusishe kwanza na siasa maana nchi haipo salama kwa sasa kuna maadui wa nje na ndani.
 
Nimeskitika sana kusikia msemaji mkuu wa Chadema na Ukawa mtandaoni kutetea ugaidi uliopo Amboni. Anadai eti Police wanashambulia wenyewe. Ajue kuwa hadi sasa kupitia ITV, Askari wanne hadi sasa wamejeruhiwa na kuna askari zaidi ya 200 eneo la tukio.

Nashauri Jeshi la Police limkamate Yericko Nyerere kwa mahojiano zaidi kwa udanganyifu wake kwa umma na udanganyifu wa kutumia mtandao.

Yericko badilika si kila jambo unatanguliza siasa, siku moja yatakuja kukutokea puani.
 
Kina Mwigulu na team yao ya CCM wameshatuaminisha ktk utapeli wao.
Kumbuka kanisani Olasiti bomu lilipuka lkn hakuna aliyekamatwa zaidi ya muendesha bodaboda, mkutano wa CDM uwanjani soweto Arusha bomu lililipuka likauwa na kujeruhi watu hakuna aliyekamatwa wala vyombo vya usalama havijui, Zanzibar mapadri wamepigwa risasi wameuwawa vyombo vya usalama havijui ni nani wanaofanya haya yote.
Wakaja wakasema Lwakatare ni Gaidi na huyu mtu anaitwa Mwigulu alisema ana ushahidi duniani na mbiguni lkn kumbe ni utapeli.

Leo hii utakuja kuniaminishaje kwamba eti vyombo vya usalama vimegundua kuna magaidi hapo Tanga wenye silaha nzito kiasi kwamba polisi wamewashindwa.
Waligunduaje hawa wanausalama wetu?
Otherwise hao magaidi kama watakuwa wametumwa na CUF, CDM au NCCR nitaamini.
 
Hayo ni matokeo ya kuingiza dini kwenye siasa, mala tutawapa mahakama ya kadhi.mala Rwakatare ni gaidi watu wakidai haki zao huko zanzibar, wanaitwa magaidi, sasa hapa ndipo tuyaona hasa nani ni gaidi, siasa za ccm ndio zimetufikisha hapa.

Mwongine huyu, shame on you.
 
1. Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,

Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,

Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2
2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,

Kila mara niwe kwako nikiburudika,

Nakupenda sana hata nikakusitiri,

Nitalalamika kukuacha Tanzania.

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2
3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,

Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,

Ninakuthamini hadharani na moyoni,

Unilinde name nikulinde hata kufa.

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2
 
Umeshuhudia ama umesimuliwa?? Lete ushahidi hapa

Kwa hiyo wewe unataka kushudia au acha kusambaza ujinga Kwa watu kama hunacha kusema kaa kimya. Usilete siasa na mambo ya kiusalama. Au unahusika nini ndio unataka kupotosha ukweli wa jambo?
 
Mafunzo ya majeshi yetu huko makambini yamejikita zaidi kwenye kuwasurubu raia na sio kuhakikisha usalama wa raia......sasa hivi imefikia hatua mpaka raia akisikia askari kauwawa tunashangilia.....askari wetu tunawakumbuka kwa mabaya kuliko mazuri....hili tukio linatakiwa livifumbue macho vyombo vya usalama......wasidhani kuwa kila mambo ni siasa......waamke kutoka usingizini na waianze kazi iliyowapeleka depo........TAIFA KWANZA...........
 
Mbona vinatumwa vikaragosi tu kwa mgongo "tetesi" "taarifa kutoka Tanga" "dondoo kutoka Tanga"!!??

Jeshi la polisi halina msemaji!? JW hawana msemaji!!?? Au ndio BADO MNAPIMA UPEPO KUONA KAMA TUTAKUBALIANA NA HIZI LONGOLONGO!!?? SHAME ON YOU!!
 
Nimeskitika sana kusikia msemaji mkuu wa Chadema na Ukawa mtandaoni kutetea ugaidi uliopo Amboni. Anadai eti Police wanashambulia wenyewe. Ajue kuwa hadi sasa kupitia ITV, Askari wanne hadi sasa wamejeruhiwa na kuna askari zaidi ya 200 eneo la tukio.

Nashauri Jeshi la Police limkamate Yericko Nyerere kwa mahojiano zaidi kwa udanganyifu wake kwa umma na udanganyifu wa kutumia mtandao.

Yericko badilika si kila jambo unatanguliza siasa, siku moja yatakuja kukutokea puani.

Mimi msemaji wa Chadema na Ukawa?? Hebu soma kwakutulia kile nilichoandika mkuu, punguza mihemko.
 
Nimeskitika sana kusikia msemaji mkuu wa Chadema na Ukawa mtandaoni kutetea ugaidi uliopo Amboni. Anadai eti Police wanashambulia wenyewe. Ajue kuwa hadi sasa kupitia ITV, Askari wanne hadi sasa wamejeruhiwa na kuna askari zaidi ya 200 eneo la tukio.

Nashauri Jeshi la Police limkamate Yericko Nyerere kwa mahojiano zaidi kwa udanganyifu wake kwa umma na udanganyifu wa kutumia mtandao.

Yericko badilika si kila jambo unatanguliza siasa, siku moja yatakuja kukutokea puani.

Tatizo hili walilipandikiza polisi wenyewe kutumika na ccm kupandikiza ugaidi usiopo nchini, leo limetokea la kutokea mnamlaumu Yeriko? Ni hivi kama kweli tunachukia jeshi la polisi kutoa matamko ya uwongo tena dhidi ya upinzani ni wakata sasa kulitaka jeshi hilo lifanye kazi kwa weledi na sio kusikiliza na kutekeleza matakwa ya chama kimoja ili kibakie madarakani. Na jeshi la polisi lisipoangalia na kujitenga na ccm iko siku kutatokea tatizo na wananchi au wapinzani kwa kuona wananyanyaswa na polisi wakaamua kuwasaidia maadui toka nje. Ama hujawi kuona washabiki wa simba kuishangilia timu ya nje inapocheza na yanga na kinyume chake? Sasa ni wakati muafaka wa jeshi la polisi kukaa mbali na vyama vya siasa na kutekeleza wajibu wake bila upendeleo.
 
Back
Top Bottom