Amboni Tanga: Askari Polisi, JWTZ wapambana na majambazi wenye silaha nzito za moto

Nawashauri tuombe sana kwa amani ya taifa hili.Haijalishi hii ni sinema au kweli ni magaidi. Hizi clip ukiziangalia hazitoi picha nzuri kwa taifa.

Huwezi jua vijana wa ngapi wamekuwa influenced already.

Askari wanapopoteza maisha kweli bado tunasema ni sinema hii?

Yamkini humu tuna magaidi wanaotaka tuamini kwamba mambo yako shwari.

Boko Haram walianza hivi hivi.Tusipochukua hatua sasa ns kuunga mkono operation hii tutazama wote.

Usilolijua ni kama usiku wa giza!
 
Kweli wewe ni mfu, Namkumbuka jaji kwenye zile kesi za kulazimishia ugaidi wakati hata ingredients za the so called Ugaidi hazikuwepo, jaji akasema DPP wacha ujinga wa kutamani ugaidi, tunaombea kitu ambacho itakuwa vigumu kukabiliana nacho in future,

Btw, kwa hiyo wewe unasapoti Tanzania kuna ugaidi? Ninachokiona ni kuwa tunaomba balaa kwa sababu za kisiasa ambayo itatu-cost more that what you will yield. UGAIDI SIYO KARATA YA KUTUMIA KWA YEYOTE AWAE, look at our neighbour, angalia nchi kubwa na zenye intelligence si ile ya kova kwenye maandamano but still these boys are abled to penetrate.

For your information, magaidi are well trained soldiers and they are smart that you think.

Tanzania hatujawahi kupambana na ugaidi,kwa hiyo hata kiuwezo hatujui tupo vizuri kiasi gani. Waulize wanaijeria, people tend to think that are not militarily good, but ukweli ni kuwa hawa magaidi wapo vizuri kizana na kimkakati, yani its well panned and organised. Waulize Wakenya-West gate mall.

Acheni upuuzi wa kueneza fikra za kigaidi kwa malengo ya kisiasa, itatugharimu hata kama malengo yenu yatafanikiwa.
tatizo kubwa haliko katika ukweli wa ulichokiongea, bali liko katika kutokujua kile unachokiongelea.
labda nikukumbushe tu kuwa hakuna kikundi cha kigaidi kilichoanza harakati zake na watu 100. kinakuwa ni kikundi cha watu wachache wenye malengo madogo huku kikiendelea ku recruit wengine na malengo yao yakizidi kukua.
1. alshabaab walianza wachache kabisa huku malengo yao yakiwa ni utekaji wa meli katika pwani ya somalia, matokeo yake kikundi kikakua na kuitawala somalia nzima na kutishia kuisambaratisha kenya.. hilo hamlioni
2.boko haram kilianza kama kikundi cha kidini kinachohubiri imani kali za kiislamu na kupinga elimu ya kimagharibi. leo hii jeshi la NIGERIA(moja kati ya majeshi bora kabisa africa) limetangaza kushindwa kukabiliana na boko haram. Cameroon na Chad nazo ziko chini ya mashambulizi ya boko haram.
ungekuwa unatumia kichwa chako kufikiria na ungekuwa namapenzi mema kwa nchi yako NADHANI UNGEKUWA UMEKWISHAONA dalili za ugaidi ndani ya nchi yetu kupitia UAMSHO ya zanzibar.
kwani mpaka sasa ni vingozi wangapi wa dini waliokwisha uwawa??
kwani mpaka hivi sasa ni viongozi wangapi wa dini waliomwagiwa tindikali ??
kwani mpaka sasa ni nyumba ngapi za ibada zilizokwisha chomwa???
kwani mpaka sasa ni watalii wangapi wamekwishamwagiwa tindikali??
kwa akili zenu ndoooooogo mnadhani haya ni matukio madogo na yasiyohitaji attention.
poleni na ninawakumbusha tena, UGAIDI HUANZA NA WATU WACHACHE WAKIWA NA MALENGO MADOGO. NA WINGI WAO HUONGEZEKA HUKU MALENGO YAO YAKIHAMA TOKA MADOGO NA KUWA MAKUBWA ZAIDI NA ZAIDI.
ninasikitika sana kuona hata katika matukio yanayohatarisha usalama wetu sote nyie mnaleta bangi zenu za bavicha. ila siwashangai kwani kila kitu kinachohitaji kulitetea taifa, nyie mnakuwa kinyume. nakumbuka mgogoro na RWANDA jinsi mlivyokuwa upande wa rwanda na kagame.
KAZI YA MBWA NI KUBWEKA
NA SISI TUNAWAACHA MBWA WAFANYE KAZI YAO
 
Nawashauri tuombe sana kwa amani ya taifa hili.Haijalishi hii ni sinema au kweli ni magaidi. Hizi clip ukiziangalia hazitoi picha nzuri kwa taifa.

Huwezi jua vijana wa ngapi wamekuwa influenced already.

Askari wanapopoteza maisha kweli bado tunasema ni sinema hii?

Yamkini humu tuna magaidi wanaotaka tuamini kwamba mambo yako shwari.

Boko Haram walianza hivi hivi.Tusipochukua hatua sasa ns kuunga mkono operation hii tutazama wote.

Usilolijua ni kama usiku wa giza!
NDUGU YANGU..
kuna kila sababu ya hili taifa kurudi katika mfumo wa chama kimoja. ama sheria za uanzishaji wa vyama na jinsi vinavyofanya kazi iangaliwe upya na kurekebishwa.jambo la hatari linalotishia usalama wa taifa kwa kiwango hichi halafu watu wanaleta siasa za kitoto kiasi hiki!!!! kuna video zinasambaa WATSUP mbona hawaziongelei.
hii inasikitisha na kwa kweli hili taifa lina misukule wengi kuliko wanadamu timamu. kila kitu kinatafsiriwa kisiasa na mwishowe hata mambo sensitive yanaonekana ya kipuuzi. kuna kila sababu ya kupambana na hawa mamluki maana mimi naamini '' HAWA WAPOTOSHAJI WALIO MIONGONI MWETU NI HATARI ZAIDI KULIKO MAGAIDI WENYEWE'
 
Huyu atakuwa Abdullah bin Kaisi, JWTZ mnyofoeni koromeo gaidi mkubwa huyo..!
Wanatafuta umaarufu kwa mgongo wa dini eti jihad1 wameishiwa kabisa hakuna atayewanuga mkono hawatamaliza hata wiki watasahaulika kabisa wanadhani TZ inaweza kuwa kama kenya na nigeria wameula wa chuya hawana mashiko kabisa wanachokitaka hakieleweki shwain wakubwa.
 
wanatangaza jihadi wamevaa yeboyebo,alafu wanaishi kwenye mashimo,hawa ni wehu tu hawa...
 
Jamani mmesahau Osama alikuwa anaishi mapango ya Torabora. ...amboni is a very strategic area kwa hawa watu.

Unaweza k uelewa kwanini Askari Jeshi wameshindwa kukamata hata mmoja!
 
Sio Salehe Otango ni Osale Otango tokea Kenya aliyewatesa wakoloni mno. Just for record.
P1010807.JPG
Mkuu umenikumbusha katika Historia eneo hili ndipo walipokuwa wakikaa na kuishi hao akina Osale Otango
P1010805.JPG
Na hapo juu kidogo ndio kuna njia waliyokuwa wakipitia kwenda na kurudi Mombasa lakini kwa sasa tunaambiwa imejifunga na ni hatari

P1010753.JPG
Na hapa ndio sehemu ya kuingia yenye muonekano wa Ramani ya Africa na picha ya Simba
 
mkuuu sielewi ni kigenzo gani ulichotumia kuwaita hao VICHAA, labda unawaona hawana nguvu,lakini bado umeonyesha hofu kuu,nikukumbushe tu,somalia ,syria, Jamhuri ya Afrika ya kati kote machafuko yalianza na chochoko za watu wachache na hatimaye kufikia hapo walipo leo,Sielewi kwanini hilijambo linachukuliwa kirahisi hivi wakati tukijua kabisa usalama wa majiran i zetu uko mashakani..Kenya,DRC,Uganda nako si salama sana, nani anajua hao vijana uliowaita wahuni ni Watanzania? NI MUHIMU SERIKALI IKACHUKUA HATUA MADHUBUTI NA SIO KUTOA TAMKO LA KIHUNI KAMA HILO LA CHAGONJA
Bwana Mpululu hawa vijana nimewaita vichaa kwani naziona akili zao sio sawa,wao wanafikiria kwa kufanya qutotations za kitabu kitakatifu(quraan)wanaamini kweli kuna kijana wa kitanzania mzalendo anaweza kuhamasika na huo upuuzi wao wa utopia kufanya ugaidi na kuungana nao ktk kuutimiza utopia walionao vichwani mwao ili kufanya machafuko nchini mwetu,nimewaita vichaa kwani wameshindwa kujua wapi pa kwenda kupigana na kuichagua nchi yetu.Tena zaidi niliwaita wao ni wahuni kwa sababu walifikiria kwa hizo quotations zilizokuwa zikitumiwa na OBL walidhani itakuwa ndio easy weapon kuwahamasisha wabongo kujiunga na uhuni na uhalifu wao dhidi ya taifa letu imara(sijui statements alizotoa yule police sifikiri ka zimetuonyesha sisi ni imara).Statement aliyotoa askari Chhagonja zinautata mwingi ndani yake na sijui ni kwa nini alishindwa kuwaita wale vijana magaidi na badala yake kuwaita ni majambazi,mimi nimebahatika kuiona ile vedio yao ya kwanza wakijisifu jinsi wakivyofanya yale mashambulizi dhidi ya askari wetu na jinsi walivyofanikiwa kuwapora silaha,nilishindwa kuelewa kuwa itakuaje vihuni kama vile vikatufanyia kitendo ka kile na vikaachwa mpaka kufikia kujigamba katika mitandao na mpaka kufikia kujigamba na pamoja kutumia lugha ya intimidation dhidi ya serikali yenye uimara wa usalama ka Tz.Hivyo viji nchi vyote ulivyovitaja ni bado vichanga sana ktk masuala ya security ya nchi ka jinsi tulivyo sisi,sisi tuliachiwa blue print ya usalama na marehemu mwenyewe hayati Kambarage pale nchini kuna system iliyojengwa na mwenyewe master ya hali ya juu sana,kumbuka watanzania sio wajinga kiasi hicho ,mpaka wafikie kujiunga pamoja na walemavu wa akili ka wale vijana.Mr Murage Msherwampamba.
 
Kufuatia operesheni ya Februari 14 iliyoendeshwa na Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la wananchi kukabiliana na uhalifu katika mapango ya Amboni, Tanga, kama kawaida na kitu cha kutarajiwa vyombo vingi vya habari vimepuliza kwa kishindo vuvuzela/tarumbeta la kuhusisha operesheni hiyo na magaidi, wakidokeza kuhusu kundi la Al-shabab.

Tunasema ni jambo la kusikitisha sana kwamba yanapotokea matendo ya uhalifu kama haya kwa haraka vyombo vya habari huyadandia na kuhitimisha kwamba ni Al-shabab au magaidi kwa makusudi hata kabla ya kukamilika uchunguzi ili kuulenga Uislamu na Waislamu.

Tunaweka wazi kwamba operesheni hii imedhihirisha zaidi kimbelembele endelevu cha baadhi ya vyombo vya habari namna vinavyochachamaa kubeba ajenda ya propaganda ya uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Katika operesheni hii licha ya Jeshi la Polisi kukanusha kupitia Kamishna Paul Chagonja, kwamba waliokabiliana nao ni wahalifu na sio magaidi, na msimamo huo huo kusisitizwa tena na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Said Magalula, bado vyombo mbali mbali vya habari vilionekana kulazimisha kwa nguvu kubwa na kuimba wimbo wa magaidi na Al-Shabab.

Aidha, ilidhihirika baadhi ya vyombo kuhusisha operesheni hiyo na matukio ya uvamizi wa vituo vidogo vya polisi vya Mngeta, Kilombero, Morogoro na cha Bukombe, Mkoa wa Pwani. Matukio ambayo hata jeshi la Polisi halijawahi kamwe kuyahusisha na masuala ya ugaidi.

Tunauliza jee ikiwa jeshi la Polisi linaweka msimamo kwamba sio ugaidi. Kwa nini tena baadhi ya vyombo vishikilie na kulazimisha msimamo huo ikiwa havikubeba ajenda ya siri?

Lazima tuweke bayana kwamba vyombo hivyo vinabeba bango hilo la propaganda ili kuwatosa zaidi Waislamu licha ya madhara na misiba mikubwa inayotusibu kwa kaulimbiu ya uwongo ya ‘ugaidi'.

Tunapenda kukumbusha kwamba tangu Marekani ilipoilazimisha dunia hususan nchi changa zikiwemo nchi zetu za Afika Mashariki kupambana na Waislamu na Uislamu kwa ujanja wa tamko la ugaidi (vita dhidi ya Uislamu).

Waislamu dunia kote ikiwemo katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki tunaishi kwa khofu, wasiwasi mkubwa na tumekuwa wahanga wa mauwaji, ,mateso na propaganda chafu.

Leo hata vile vyombo vya habari duni amma kwa kuburuzwa, kuajiriwa au kujipendekeza kwa madola makubwa hususan Marekani vinafuata sera ya kiuadui dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kudandia na kulipinda kila tukio ili kuutosa Uislamu na Waislamu. Vyombo hivyo vikijisahau kwamba Waislamu ni miongoni mwa wateja wake wakubwa.

Aidha, tunakumbusha kwamba tabia hii ya baadhi ya vyombo vya habari kupayukapayuka kwa uadui dhidi ya Waislamu na Uislamu ni jambo la hatari ambalo huvuruga mahusiano mema baina ya watu, sio tu Tanzania bali dunia nzima.

Kwa kumalizia, ni wakati wa kutanabahi kwa baadhi ya vyombo vya habari, wanasisa na watendaji wao zikiwemo taasisi za ujasusi, ulinzi na usalama kwamba licha ya kubebeshwa na Marekani ajenda ya uadui na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Bado dola hiyo inazieka nchi zetu hizi, viongozi na watendaji wake kuwa ni watu wa daraja duni hata kuliko watumwa na wanazitazama nchi zetu, viongozi na raia wake kwa jicho la dharau isiyo na mfano.

Hali hiyo hudhihirika katika miamala ya kila siku baina ya maafisa wa madola hayo makubwa hususan Marekani wanapokuwa na maafisa wa nchi zetu.

Basi hili ni funzo la kutosha kwa nchi changa kama yetu kuacha uadui na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Uadui ambao kiudhati ni ajenda tu ya kubebeshwa na wengine.
 
katika hotuba yake ya mwishoni mwa mwezi wa february Rais Kikwete hakumtaja mwanajeshi aliyeripotiwa kupoteza maisha huko katika mapango ya Amboni Tanga.. Lakini amewataja askari saba wa jeshi la polisi waliouwa mbali na tukio la Amboni Maswali ni haya je (a) Kasahau kumtaja ..? Ukizingatia yeye ni Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote (b) au Hakukua na tukio la wanajeshi kuhusishwa..? (c) au hakukua na maafa...? Vyombo vya habari vilizuiwa kwenye tukio, hivi haya mambo yamekaaje..? je ni nini kilichoko nyuma ya pazia..?
 
Back
Top Bottom