Mtende
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 6,385
- 7,295
napenda kuwatia moyo wale ambao walijiandikisha lakini hawajaona majina yao katika vituo vya kupigia kura,tafadhali hakikisha unafika ofisi ya kijiji au ofisi ya kata yako kuna madaftari ya kudumu ya wapiga kura ambayo husambazwa katika kila kijiji na kata kwa ajili ya watu kuhakikisha majina yao pale yanapokuwa yamekosekana katika list,hivyo hadi sasa nimepata taarifa kuwa hayo madaftari ya kudumu yameshasambazwa hivyo pls nendeni mkahakikishe kwani pengine ni makosa ya kimaandishi tu yametokea ndio maana hujaona jina lako,usikubali kupoteza haki yako kwa ajili hujaona jina lako,ni hayo tu.