Amazing true coincidences.

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,235
2,000
Unaweza kuongeza uliyokutana nayo au ya kwako.

"Zangu source hazijulikani"

Mfalme wa Italia wa 18, Umberto alikwenda mgahawani huko Monza na Mkuu wa majeshi Emilio Ponzia Vaglia. Mmiliki wa mgahawa alichukua oda ya Mfalme Umberto. Baada ya muda kidogo Mfalme aligundua kwamba yeye na mmiliki wa mgahawa wanafanana kwa kila kitu na walionekana karibu sawa. Wanaweza kuwa ndugu.

Walipokuwa wakizungumzia jinsi walivyofanana, waligundua kuwa:-
---- wote wawili walizaliwa tarehe 14 Machi 1844.
----Wote wawili wamezaliwa katika mji huo huo.
----Wote wawili walioa na wamefunga ndoa na wanawake wanaoitwa Margherita.
----Mmiliki wa mgahawa alifungua mgahawa wake siku hiyo hiyo Umberto alipokuwa Mfalme.

Cha kushangaza Miaka michache baadaye, mwaka wa 1900 Mfalme Umberto aliambiwa kuwa mmiliki wa mgahawa alifariki. Mfalme Umberto alisema kwa watu wake wa karibu jinsi alivyokuwa amesikitishwa saana na kusikia habari hii ya mtu aliyefanana naye kufariki. Baadae mfalme alipigwa risasi mara nne na kufariki dunia na muuaji inasemekana aliitwa Gaetano Bresci. Mfalme Umberto alizikwa Pantheon.
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,235
2,000
Wengi mtakuwa mnamsoma au kumskia mwanamama Mwandishi wa vitabu kama "The perennial bachelor" na "All kneeling" Anne Parrish.

Alikuwa na mumewe kwenye likizo huko Paris mwaka wa 1920. Walikuwa maktaba wakiangalia na kusoma vitabu, Anne akachukua kitabu alichokuwa anakipenda zamani kiitwacho "Jack Frost and others stories."

Anne alimwambia mumewe kwamba alikuwa anakisoma na alipewa nakala ya kitabu hicho alipokuwa mtoto na wazazi wake.Mume wa Anne alichukua kitabu na kukifungua. Katikati alikutana na kikaratasi kilichokuwa na usajili ulioandikwa kwa mkono tena kwa mwandiko wa mkewe "Anne Parrish, 209 N Weber Street, Colorado Springs".

Uandishi huo uliandikwa kwa mkono wa Anne. Ilikuwa ni kitabu cha Anne alichokuwa anakisoma enzi zile.
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,235
2,000
Hii ndiyo kali yao nimeitoa "readers digest"


Wakati mwingine mapacha wana hadithi za kushangaza ila hawa ni kali yao. Wavulana wadogo walijitenga baada kuchukuliwa na wazazi wengine. Wazazi wapya wa wavulana hawajawahi kufahamiana na hawajawahi kukutana. Ila kila mmoja aliambiwa alikuwa na ndugu.

Miaka arobaini baadaye mmoja, James aliamua kufuatilia ndugu yake ajue alipo. Baada ya kumtafuta muda mrefu, akamkuta ndugu yake, na alikutana na haya:-

--- pacha mwenzie naye aliitwa James! Ingawa hawajawahi kukutana.
--- wote wawili walikwenda kusoma "law enforcement"
---Wote wawili walikuwa na ujuzi bora ufundi seremala na kuchora.
---Wote wawili walioa wanawake walioitwa Linda.
---Wote wawili walikuwa na watoto, mmoja alitwa James Allan wa mwingine aliitwa James Alan.

---Baadae kila mmoja alitengana na mkewe na kuoa tena wanawake walioitwa Betty!

--pia wote wawili walimiliki mbwa na kila mmoja alimpa jina la Toy!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom