Amani, Utulivu CCM, Vurugu, Machafuko, Chadema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amani, Utulivu CCM, Vurugu, Machafuko, Chadema?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Oct 18, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Huu ni mjadala mwingine katika jamii, unaotawaliwa na hoja nyepesi nyepesi; Vinginevyo kilicho kizito ni kwamba kama mtu ni muumini wa nadharia za machafuko (theories of conflicts and violence), basi Tanzania ilitakiwa iwe katika machafuko kwa muda mrefu sasa; Kinyume na hayo, Tanzania bado inaendelea kuwa nchi ya Amani na Utulivu on a ‘MACRO SCALE', ukiachilia Mbali Matukio Ya Vurugu YA Hapa na Pale on a ‘MICRO SCALE'; Pamoja na haya yote, Kuna Kila Dalili Kwamba Hatupo Mbali Kupoteza Sifa Hii kama Taifa;

  Kabla ya kunyosheana vidole na kulaumiana kwa hoja nyepesi nyepesi, nadhani ni muhimu tumrejee kidogo Mwalimu Nyerere; Kuna mambo mawili makubwa ambayo sidhani kama ni ya mjadala; Kwanza, ni Ukweli kwamba Mwalimu Nyerere Kuwa ndiye Mjenzi Mkuu wa Taifa la Amani na Utulivu ambalo sote bila ya kujali itikadi za vyama, tunajivunia; Pili, ni ukweli kwamba msingi wa Ujenzi wa Taifa hilo, ilikuwa ni Azimio la Arusha;

  Ebu tutazame Mwalimu ana maoni gani juu ya suala hili lililopo mbele yetu (Shivji, 2000):

  ["It is not that peace has come by itself. The source of peace in Tanzania is not that the Arusha Declaration has done away with poverty even a little bit. Isn't there this poverty we are still living with? This poverty is right here with us. It is not the same economy we are grappling with? The fact is not that the Arusha Declaration has banished poverty even by an iota – nor did it promise to do so. The Arusha Declaration offered hope. A promise of Justice, hopes to the many, indeed the majority of Tanzanians continue to live this hope. So long as there is this hope, you will continue to have peace. Here in Tanzania we have poverty but no ‘social cancer'. It is possible it has just begun. But otherwise we don't have a social cancer. There isn't a Volcano in the making, that one day it is bound to erupt. We have not yet reached that stage because the people still have hopes based on the stand taken by the Arusha Declaration. It did not do away with poverty but it has given you all in this hall, capitalists and socialists alike, an opportunity to build a country which holds out a future of hopes to the many.

  To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, when there is no hope? When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I'd be surprised if these Tanzania refuse to rebel, why?

  When the majority don't have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools. Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools. So Tanzanians would be fools, ****** (imbecile, morons, retarded/majuha), if they continued to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?

  Therefore we cannot say that we have now reached a stage when we can forget the Arusha Declaration. Don't fool yourselves. This would be like that fool who uses a ladder to climb and when he is up there kicks it away. Alright, you are up there, you have kicked away the ladder, right, so stay there because we will cut the branch. You are up there, we are down here and you have kicked away the ladder. This branch is high up, we will cut it. Your fall will be no ordinary fall either.

  Let me say no more. It is sufficient to say we should accept our principles, we should continue with our principles of building peace and peace itself. Tanzanians should continue to have faith in the party, in the government and in you in positions. Tanzanians should see you as part of them not their enemies. They should trust the party, the government and you who have opportunities for there is no country where everyone is equal. These fingers of mine are not equal, and in that sense there is no such equality anywhere."]

  Mwalimu Anatufunda Nini?

  Kwanza:
  Hali aliyoinzungumzia Nyerere Miaka 25 iliyopita, inazidi kujitokeza leo Tanzania;
  Pili: Mwalimu alizungumza maneno haya Wakati wa Mfumo wa Chama Kimoja Cha Siasa (CCM), na ilikuwa ni MIAKA NANE (1987) Kabla ya Kuzaliwa kwa CHADEMA (1995), Hivyo SIO SAHIHI Kuelekeza Lawama Hizi Moja Kwa Moja Kwa Chadema;
  Tatu: Mwalimu alikuwa anatuonya Kwamba, Kitendo Cha Kuachana na Azimio La Arusha Bila Kwanza Ya Kuangalia Yepi Bado Yanatufaa, Kitapelekea Mmomonyoko wa Amani na Utulivu Tanzania;

  Nia yangu sio kujenga hoja kwamba nani anahusika na hali ya sasa ya kutoweka kwa amani, na badala yake, kujenga mazingira ya mjadala huo kwa faida yetu sote; Nitafanya hivyo kwa kujadili nadharia za machafuko (theories of conflict and violence) katika mataifa, ili baadae tuje kuzijadili kwa mazingira ya Tanzania. Zipo nadharia kadhaa zinazoelezea vyanzo vya machafuko ndani ya taifa, na kama nilivyojadili hapo awali, kwa muumini wa nadharia hizi, Tanzania ilitakiwa iwe katika machafuko makubwa muda mrefu uliopita;

  Nadharia hizi Zinaelezea Virutubisho Vikuu Vya Machafuko Katika Taifa Kama ifuatavyo:


  1. Ukosefu mkubwa wa ajira katika taifa;
  2. Idadi kubwa ya Vijana ndani ya taifa;
  3. Idadi kubwa ya Makabila na mgawanyiko mkubwa wa imani za Kidini;
  4. Machafuko ya Kisiasa Kwenye Nchi Zinazopakana na Taifa husika;
  5. Hali Duni (Kimapato) kwa wananchi walio wengi;
  6. Utegemezi (usiokwisha/chronic) wa Misaada kutoka mataifa ya nje, hasa katika kuendesha bajeti ya nchi;

  Swali linalofuata ni, Je, Virutubisho Hivi Vipo Tanzania? Ufuato ni Mtazamo wangu juu ya hili:

  1. Ukosefu mkubwa wa ajira katika taifa
  Hiki ni kirutubisho cha kwanza cha machafuko ndani ya nchi; Mamilioni ya watanzania wanakabiliwa na tatizo la ajira, wengi wao ikiwa ni vijana walio kati ya umri wa miaka 15 na 25; Kwa mujibu wa Benki ya Dunia (2010), jumla ya watanzania 850,000 huingia katika soko la ajira kila mwaka, huku wachache wakifanikiwa kupata ajira rasmi na za kudumu; Benki ya Dunia inakadiria kwamba - ifikapo mwaka 2015, jeshi hili litaongezeka by an extra 1.3 Million; Swali linalofuatia ni je:


  • Jeshi Hili Linaingia Kwenye Soko la Ajira na Ubora wa Namna Gani?

  ELIMU YA MSINGI
  Tukianza na vijana wanaomaliza elimu ya msingi, jumla ya wanafunzi katika mfumo wetu wa shule za msingi inakaribia MILIONI TISA; Katika hawa, inaelezwa kwamba ni 80% ndio huwa wanafanikiwa kumaliza elimu ya msingi, [sawa na karibia watoto MILIONI SABA NA LAKI MBILI], huku 20% ya wanafunzi waliobakia wakishindwa kumaliza elimu yao ya darasa la saba kwa sababu mbalimbali – [sawa na karibia watoto MILIONI MOJA NA LAKI NANE];

  Kwa maana hii kila baada ya miaka michache, watoto zaidi ya Milioni Moja Wenye Umri wa Kuwa Shule, huishia mitaani wakiwa na umri chini ya miaka 15;

  MUHIMU
  Kati ya wanafunzi tuliobaini wanamaliza elimu ya msingi (watoto milioni saba na laki mbili), ni 20% tu ndio hufanikiwa kuendelea na elimu ya sekondari (milioni moja la laki nne), na watoto waliobakia (takribani milioni tano na laki saba), hujumuika na wale wenzao ambao hawakuweza kufika darasa la saba, hivyo kufanya Jumla ya watoto wanaoishia mitaani bila ya elimu zaidi ya darasa la Saba, katika interval ya miaka michache, kuwa takribani MILIONI SABA NA NUSU;

  Hili ni sehemu ya kundi katika jamii ambalo Mwalimu Nyerere anawazungumzia kwani wanaishi katika mazingira yaliyokosa kila aina ya haki (Social injustice, Economic injustice&Political injustice); Kundi hili kwa kiasi kikubwa sana limeshakata tamaa na Utawala Wa CCM; Tukumbuke pia kwamba kabla ya kufariki dunia, Nyerere aliwahi sema maneno haya (1995):

  "Watanzania wanataka Mabadiliko, na Wasipoyapata CCM, watayatafuta kupitia Chama Kingine"

  Sasa, kwa bahati mbaya au nzuri, kutegemea Mtu Yupo Upande Upi wa Hoja, Chadema kinaendelea kuwa Chama Mbadala alichozungumzia Mwalimu, na isitoshe, wakati wa uhai wake, Mwalimu alitaja Chadema kwa jina - kwamba kina kila dalili ya kuja kuwa na mafanikio siku za usoni;

  ELIMU YA SEKONDARI
  Mbali ya tatizo lililopo kwenye elimu ya msingi, kwa mujibu wa Benki ya Dunia (2010), katika kipindi cha mwaka 2000 – 2010, jumla ya wanafunzi milioni moja la laki tatu walimaliza elimu yao ya Sekondari; Kati ya hawa:


  • Waliopasi kwa Division One ilikuwa ni 3% (wanafunzi takribani 39,000)
  • Division Two, 5% (takribani wanafunzi 65,000)
  • Division Three, 15% (takribani wanafunzi 195,000)
  • Division Four, 50% (takribani wanafunzi 650,000)
  • Division Zero, 26% (takribani wanafunzi 338,000)

  Kwa maana hii, iwapo tunachukulia kwamba wanafunzi waliopata madaraja ya Kwanza hadi Tatu ndio uendelea na elimu ya juu, basi ina maana kwamba kati ya wanafuzi milioni moja na laki tatu waliomaliza elimu zao za sekondari katika kipindi hicho (2000 – 2010), waliofanikiwa kuendelea na elimu ya juu ni 25% tu [sawa na wanafunzi 325,000 kati ya jumla ya wanafunzi 1,300,000]; Hivyo, katika kipindi hiki, wanafunzi wa sekondari walioishia mitaani ni karibia 975,000; Hata kwa wale wanaofanikiwa kuendelea na elimu ya juu, bado suala la ajira huko mbeleni sio la uhakika;

  MUHIMU
  Ni dhahiri kwamba wengi ya watoto (vijana) hawa ambao hawaendelei na elimu za juu, wanaingia kwenye soko la ajira wakiwa hawana ujuzi wa kutosha kuweza kumudu ushindani katika soko; Lakini hili lisingekuwa tatizo sana iwapo wangekuwa wanavutiwa na ajira kwenye sekta ya KILIMO; lakini kwa bahati mbaya, ni idadi ndogo sana ya vijana hawa wanavutiwa na ajira katika Sekta ya Kilimo; Hili ni tatizo, hasa ikizingatiwa kwamba bado KILIMO kinatambulika rasmi kama sekta kuu ya ajira, na pia Uti wa Mgongo wa Taifa ‘Kiuchumi';

  2. Idadi kubwa ya Vijana Ndani Ya Taifa
  Hiki ni kirutubisho cha pili cha machafuko ndani ya nchi; Suala hili linaenda sambamba na lile la awali – yani tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana; Lakini kwa kuongezea tu, kwa mujibu wa African Economic Outlook (2010), zaidi ya 60% ya watanzania hawajavuka umri wa miaka 25, na inakisiwa kwamba ifikapo mwaka 2015, idadi hii itaongezeka na kufikia 75% ya jumla ya idadi ya watanzania; Kwa maana hii, ifikapo mwaka 2015, watanzania zaidi ya milioni 33 watakuwa chini ya umri wa miaka 25; Hili ndio "TIMING BOMB" ambalo wanasiasa mbalimbali wamekuwa wanajaribu kulijadili kisiasa;

  3. Idadi kubwa ya Makabila na mgawanyiko mkubwa wa imani za kidini
  Kirutubisho hiki kipo bayana: Inasemekana Tanzania ina makabila zaidi ya mia moja na ishirini, na pia Taifa limegawanyika karibia nusu kwa nusu kati ya Waumini wa Kislam na Waumini Wa Kikristo;

  4. Machafuko ya Kisiasa Kwenye Nchi Zinazopakana na Taifa husika
  Hiki ni kirutubisho cha nne; Tanzania imezungukwa na nchi ambazo - karibia zote zimepitia machafuko ya aina mbalimbali, huku nyingine zikiendelea kuwa katika hali ya machafuko; Kutokana na machafuko haya, Tanzania ilishawahi kupokea jumla ya wakimbizi karibia milioni moja kutoka nchi za maziwa makuu zilizokuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe; Kuna wakati Tanzania ilikuwa ni moja ya mataifa yenye idadi kubwa ya wakimbizi duniani;

  5. Hali duni za vipato vya wananchi walio wengi
  Hiki ni kirutubisho cha tano; Kwa mujibu wa takwimu za IMF, Pato la Taifa Tanzania ni takribani Dola Bilioni 23 kwa mwaka; Vile vile, kwa miaka kumi na mbili mfululizo (2000 – 2012), uchumi wa nchi unakuwa kwa wastani wa karibia 7% kwa mwaka; Huko nyuma, Benki ya Dunia iliwahi kutamka kwamba - nchi ikiwa na kasi ya namna hii kwa miaka zaidi ya kumi mfululizo, inakuwa katika nafasi nzuri ya kufikia malengo yote ya MILLENIA, hasa kupunguza umaskini kwa 50%;

  Lakini Je, Umaskini Tanzania Umepungua Kwa Kiasa Gani?
  Pato la taifa la Dollar Bilioni 23 kwa mwaka, linaiweka Tanzania katika nafasi ya kumi na nne kwa ukubwa kiuchumi barani Afrika (kati ya mataifa 53), na nafasi ya ‘98' duniani kati ya jumla ya mataifa 185 yaliyomo kwenye orodha ya Benki ya Dunia (2011); Kasi yetu ya kukua kwa uchumi (takribani 7% kwa mwaka), inaiweka Tanzania kuwa nchi ya 12 Afrika na ya 43 duniani;

  Hizi discrepancies hapa ni tosha kuleta mashaka kuhusu thamani ya uchumi wetu ni kwa faida ya nani; Vinginevyo, kilicho dhahiri ni kwamba - Tanzania ina rasilimali nyingi zinazovutia mitaji mingi kutoka sehemu mbalimbali za duniani (kwani uchumi wetu unaendeshwa na mitaji ya nje kwa karibia 75%), lakini mitaji hiyo haiji kwa ajili ya watanzania walio wengi, wala kwa manufaa ya watanzania walio wengi, bali inakuja kutokana na rasilimali nyingi zilizopo Tanzania na kwa manufaa ya wachache;

  Swali linalofuatia ni JE:


  • Who Gets the Largest Share and Who Benefits the Most?

  Bila shaka jibu ni kwamba – sio watanzania walio wengi, hasa wakulima vijijini; Zipo tafiti zinaonyesha kwamba asilimia ya waanchi wanaofaidika na uchumi wa leo Tanzania, haizidi 10% ya watanzania wote, licha ya nchi kujaliwa kila aina ya rasilimali; Kwa maana nyingine, kukua kwa pato la taifa na uchumi hakupelekei Maisha Bora kwa watanzania walio wengi;

  Ifuatayo ni sehemu ndogo ya ushahidi juu ya hili:

  Pamoja na Tanzania kuwa ni nchi ya '98' kwa ukubwa wa uchumi duniani, na nchi ya '43' kwa kasi ya kukua kwa uchumi duniani, katika suala la GDP Per Capita, Tanzania ni nchi ya sita kutoka mwisho Duniani; Tanzania ni bora kwa nchi zisizozidi tano ambazo ni: Malawi, Madagascar, Burundi, Liberia na DRC; Kwa maana nyingine rahisi, kwenye suala la vipato kwa wananchi, Tanzania ni nchi ya sita kutoka mwisho duniani, hivyo kufanya watanzania kuwa miongoni mwa watu maskini kuliko wote duniani, huku nchi yao ikiwa ni moja ya nchi tajiri kupindukia duniani;

  Wapo wanaoweza kujenga hoja kwamba GDP Per Capita sio kielelezo kizuri, hivyo tujaribu kuangalia vielelezo vingine juu ya umaskini wetu watanzania: Idadi ya Watanzania wenye $1.25 (karibia 2,000/=) au chini ya hizi mifukoni mwao kila siku ni karibia 70% (karibia watanzania milioni 30); Na Watanzania wenye $2 (takribani 3,000/=) mifukoni mwao kila siku, ni karibia 90% (sawa na watanzania takribani milioni 36);

  Je: Shillingi elfu mbili au elfu tatu kwa siku
  inatosha kwa matumizi ya aina gani kwa mtanzania wa leo kwa mahitaji kama vile nauli, chakula cha familia, mahitaji ya watoto shule n.k? Ni dhahiri haitoshi, na kwa maana hii, zaidi ya watanzania milioni 30 wanaishi maisha ya kuunga unga, na yasio na matumaini kama alivyojadili Nyerere awali;

  6. Utegemezi wa misaada usiokwisha kutoka nje, kuendesha bajeti ya nchi

  Hiki ni kichecho cha mwisho cha machafuko, kukijadili; Tunafahamu kwamba Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa kutegemea misaada kutoka nje kuendesha bajeti ya nchi; Kwa miaka zaidi ya 30 sasa, Tanzania imekuwa katika kumi bora ya orodha hii kidunia; Inakadiriwa kwamba, tangia uhuru, zaidi ya dollar za Kimarekani Bilioni KUMI zimeingia Tanzania kwa njia hii; Swali la kujiuliza ni je:


  • Mabilioni haya ya dollar, yamefanya kitu gani cha maana kwa watanzania walio wengi (hasa vijijini)?

  Swali hili ni muhimu, hasa ikizingatiwa kwamba, wananchi walio wengi hawaelewi kwamba Fedha hizi kuitwa misaada haina maana kwamba zinakuja bure, kwani ni mikopo yenye masharti na riba nafuu ambayo hulipwa na fedha za walipa kodi – wakulima, wafanyakazi, mama ntilie, machinga, n.k;

  Madhara Ya Kutegemea Sana Misaada:

  Yapo mengi, lakini kwa madhumuni ya mjadala huu, kwanza, Utegemezi Huu ambao sasa umekuwa ni wa Kudumu, umeua dhana ya "KUJITEGEMEA" katika nchi yetu, na badala yake, tunajulikana kama moja ya mataifa matajiri duniani ambao ni "OMBA OMBA";

  Pili, kutegemea sana misaada kuna athiri BALANCE OF PAYMENTS ya nchi yetu: Maana rahisi ya kuelewa dhana ya Balance of Payments: BOP ni tofauti iliyopo baina ya MALIPO TUNAYOFANYA nje ya nchi (outflows) kama vile madeni, manunuzi ya bidhaa muhimu kwa maendeleo ya uchumi kama vile mashine, vipuri, magari ya serikali, n.k, na MALIPO TUNAYOPATA kutoka nje ya nchi (inflows), kama vile mapato yanayotokana na kuuza mazao yetu nje, madini yetu n.k;
  Lakini kwa vile kwa miaka mingi tumekosa uwezo wa kuzalisha bidhaa muhimu kupitia viwanda vyetu na badala yake tunaagiza hata vitu virahisi kutengeneza nchini, na kwa kuwa kwa miaka mingi tumekuwa hatutumii vizuri mikopo kutoka nje kwa kuwekeza kwenye sekta ambazo zitatusaidia tujitegemee kama taifa, OUTFLOWS (malipo ya mikopo, manunuzi ya capital goods n.k) zinakuwa ni kubwa kuliko INFLOWS (mapato yetu kutoka kwenye biashara ya kimataifa n.k), na kupelekea Balance of Payments Deficits;

  Na Kutokana na Deficit hii kuendelea kuwa mzigo – kutokana na kukopa zaidi na zaidi bila ya kujitengenezea mazingira ya kujitegemea na pia kulipa madeni yaliyopo kwa uhakika; na pia kutokana na suala ufisadi kuzidi kushika kasi, nchi nyingi wahisani zimeanza kulegeza kamba, na hatuna uhakika iwapo wahisani wataendelea kutusaidia katika bajeti zetu kwa kwa viwango vinavyohitajika; Na iwapo misaada katika bajeti itapungua, huku taifa likiwa halijajitengenezea mazingira ya kujitegemea, hii itapelekea kupungua kwa kwa huduma za kijamii kutoka serikali ya CCM, jambo ambalo linaweza kuchochoea hali ya machafuko nchini;

  HITIMISHO
  Tumeona kwamba virutubisho vyote sita vya machafuko katika Taifa, vipo Tanzania; Lakini pamoja na hayo, kwa kiasi kikubwa, Tanzania bado inaendelea kuwa nchi ya Amani na Utulivu, licha ya uwepo wa Volcano anayoizungumzia Mwalimu Nyerere. Maswali ya Kujadili:


  1. Nini ni Chanzo Kikuu cha Mmomonyoko wa Amani na Utulivu Nchini Tanzania?
  2. Je, Ni Chadema? Kwa Hoja Zipi?
  3. Je, Ni Kweli Kwamba Mjenzi wa Taifa La Amani Na Utulivu Ni ‘Mwalimu Nyerere' Kupitia Azimio La Arusha?
  4. Kama Jibu Kwa Swali la Tatu ni NDIO, Kwa Vile Nyerere Hatunaye Tena na Azimio La Arusha Hatunalo Tena, JE, nini imebakia kuwa nguzo kuu ya Kulinda Amani na Utulivu Katika Nchi Yetu?
  5. Je, Ni CCM? Kwa Hoja Zipi?
  6. Kama Jibu Kwa Swali la Tatu ni HAPANA, Bila ya Kujali Itikadi Zetu Za Vyama, Nini Ni Mbadala Rasmi Wa Azimio La Arusha Ambao Unaeleweka na Unaokubaliwa na Walio Wengi Kwamba Una Manufaa Kwa Taifa, na Mbadala ambao CCM na Chadema Wote Wapo Tayari Kuufanyia Kazi, CCM ikiwa Chama Tawala au Chama Kikuu Cha Upinzani au Chadema ikiwa Chama Tawala au Chama Kikuu Cha Upinzani?
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Makala makini. Taifa lisilo na maono huangamia. hii ni divine principle. Dira yetu ni nini?
   
 3. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ndugu Mchambuzi, Watanzania tu wavivu wa kusoma. Unapoweka makala ndefu kama hii usitegemee mchango wa kutosha.
   
 4. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Zimamoto, lakini siangalii sana quantity ya wachangiaji bali quality ya wachangiaji; Natambua wapo wachache ambao huwa tunakuwa na mijadala mizuri na mirefu iliyojaa migongano ya mawazo katika masuala kama haya, kama vile kina nguruvi3, kobello, jokakuu, Jasusi, Mkandara, EMT, Jingafalsafa, Mimibaba, kimbunga, jmushi1, bongolander na wengine wengi tu ambao siwezi kuwakumbuka kwa haraka haraka;

  Ni matumaini yangu tutakuwa na mjadala mzuri, hasa ikizingatiwa kwamba huko tuelekeako (2015), watanzania wengi wamekubali kwamba tunahitaji mabadiliko, lakini wapo wengi zaidi ambao licha ya hayo, bado suala la CCM, Chadema, Amani na Utulivu, Machafuko, Vurugu, linaendelea kuwachanganya, na hivyo kuwa katika nafasi ya kuchagua chama cha siasa mwaka 2015,tofauti na dhamira zao moyoni;

  Je wewe una mtazamo gani juu ya hili?
   
 5. G.T.L

  G.T.L JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Heshima kwako MKUU...Nimekuelewa.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hakuna hoja dhaifu unazoainisha hapa zenye uzito zaidi ya hoja ya poor leadership ninayoiona mimi ndiyo iliyotufikisha watanzania hapa tulipo. Stronger leader anaweza kuona mbali na kuzuia yasitokee. Weak leader kwake bora liende, na kila mwenye jukumu ni wajibu wake, hana ile kitu followup, mbaya zaidi mwenye kuboronga ajipime mwenyewe na aamue kujiondoa, maana yake kuwaonea haya au kuwaogopa kuwawajibisha wateule wake?. Hii ndiyo hoja ya haya yanayoendelea hapa nchini. Hakuna sababu ya list kubwa kwani huko ni matawi tu, kwani kama ni tatizo la ajira na wingi wa vijana ni la muda mrefu si Tanzania tu, ila ulimwengu wa tatu na wa kati wakati nchi nyingi hutakuta tunayohangaika nayo.

  Matatizo ya uchumi duniani nchi zilizoendelea wanajuta kuzaliwa, makampuni mengi yamebaki majengo nyumba za mapopo, shoppinga malls zimebaki tupu na baadhi kugeuza vyuo vyuo na vituo vya afya, biashara na uzalishaji umedumaa tofauti na Tanzania ambako huwezi kuona mahame kama hayo katika nchi tajiri. Huko hawafanyi hayo pamoja na kwamba hali ya huko imepelekea watu makazi yao (nyumba) kukumbwa na foreclosure kwa sababu ya kukosa ajira, na wengi kuishia kuwa homeless, hilo lingekuwa bongo nini kingetokea? Kwa sababu ya strong leadership wanajua one day hopefully can be better kutokana na mipango madhutubi inayofanya na strong leadership waliyonayo.

  Ikishafikia watu kukata tamaa katika poor leadership haya ndiyo matokeo yake. Sawa na timu kuwa na wachezaji wazuri lakini unashangaa kwa nini inaboronga, kuna kitu ambacho wachezeaji hawaridhiki kama ilivyotokea Yanga karibuni, walipomfukuza Kocha mambo yamebadilika.

  Tuwe wa kweli poor leadership ndiyo iliyotufikisha hapa, hata nchi nyingi zilizoendelea hazikufikia mafanikio tokana na kiongozi wa kitaifa kuishi zaidi nje ya nchi yake, bali kushiriki kikamilifu mambo ya kila siku nchini mwake na kuwa karibu na wananchi huku akifuatilia kwa makini utendaji wa wateule wake kuhakikisha uwajibikaji wa kila mmoja.

  Hata Sultani, mfalme au malkia pamoja na enzi zao walizo nazo si kwa kiwango cha JK kuhamishia Ikulu kuwa ndani ya ndege ya rais na kwenye mahotel ya kitalii duniani. Gharama hizo anazotumia ipo siku zitaainishwa tutabaki midomo wazi kwani makubwa yangefanyika.

  Kiongozi legelege na dhaifu ndio matokea tunayoshuhudia sasa na bado makubwa yaja.
   
 7. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Candid Scope,

  Asante kwa mchango wako; Nakubaliana na wewe kwamba udhaifu wa uongozi umechangia sana kutufikisha hapa kama taifa; Lakini kwa mtazamo wako, udhaifu huo katika uongozi ulianza lini? Na ni katika maeneo gani? Na je, ni lini watanzania walio wengi walianza kukata tamaa na hali zao za maisha? Na je ni kutokana na sababu zozote nje ya uongozi dhaifu? Na nini ni mtazamo wako kwa maswali matano niliyouliza mwisho wa bandiko langu namba moja?
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160


  Tanzania kabla ya awamu hii ya Kikwete ni tofauti sana na awamu zilizotangulia pamoja na kasoro kadhaa ambazo zilijitokeza. Rais amekuwa mtu wa kuzungumzia udini bila kufafanua maana yake na yaliyojilia baadhi ya dini kuwa na vurugu zisizo muhimu na kuwa mwanzo wa uvunjaji wa sheria na amani nchini, Kikwete hajaonekana kukemea bali inapotokea na kuongea kwa upole usioonyesha mtu mwenye mamlaka ya kukemea kinachoendelea.

  Mfano mmoja na Mauaji ya Mwangozi, katika hotuba ya Kikwete Mwisho wa mwezi aligusia jambo hilo, na akazungumza kwa upole mno kwamba
  jamani naomba tuwatumie vizuri polisi na tuwaelewe vizuri. Hii inajenga picha gani kwa yaliyotukia? Dhahiri kuonyesha ulegelege na udhaifu badala ya uwajibikaji uliotazamiwa na wananchi.

  Mwinyi alionekana kuwa legelege kidogo, lakini alikuwa makini na kufanya jitihata za kuhakikisha cabinet yake inawajibika kwa pamoja ndiyo yaliyotokea akina Mzee wa Kiraracha kuwajibishwa kwenye baraza la Mawaziri bila shinikizo la bunge hali kadhalika waziri wa Fedha wakati huko Kighoma Malima. Leo hii katika historia ya nchi hii bunge limekuwa na kazi ya kuishinikiza serkali kuwawajibisha watendaji wa ovyo ovyo serikalini na raisi alipotia pamba masikioni bunge limewajibika kutishia kura ya kutokuwa na imani ndipo kwa woga amechukua hatua.

  Mkapa amekuwa kidogo strong katika kujenga uchumi wa nchi ingawa amekuwa mwepesi katika kuliza maliza taifa na hazina za wafanyakazi kama uuzwaji wa mashirika ya umma ambao umemwacha katika shutuma nzito hali kadhalika kuamua viongozi wenye nafasi kugawana fixed asserts za serikali kama nyumba wa watumishi wa umma, nk.

  Lakini kipindi cha Kikwete pamoja na kwamba nimeshuhudia pia awamu ya kwanza ya Nyerere sijapata kuona kiongozi dhaifu na mpenda matanuzi binafsi kama Kikwete bila kujali gharama anazotumia kwamba zinaigharimu nchi. Mzunguko wake kwenye global hii kukopa pesa naone huruma kiongozi atakayefuata kupata mzigo mzito wa madeni, maana Mkapa alijitahidi sana kupunguza deni la Taifa kwa juhudi zote na alifanikiwa.

  Misukosuko ya kidini ilianza siku nyingi lakini vingozi walikuwa makini kuepusha shari kabla mambo hayafikia mahali pa baya. Nakumbuka wakati Augustin Mrema alipokuwa naibu waziri mkuu, choko choko hizi zilijitokea, aliitisha kikao cha viongozi wawakilishi wa dini za kiislamu na wakristo, mimi nikiwa bado kijana mbichi sana ningali katika uwanja wa Habari, niliwakilisha Publication mojawapo pale Diamond Jubilee. Nilichoshuhudia ni Mrema kujitahidi kupatanisha na kuwaweka sawa wale walioleta choko choko. Wazungumzaji wakuu kidini waliku yule Muft mwenye busara wa zamani Hemed bin Hemed, upande wa RC Pengo akiwa askofu msaidizi wa DSM alimwakilisha Mwadhama Rugambwa. Hayo yalisaidia kutuliza mambo yaliyokuwa yanataka kufumuka. Kama siku hizi wangefanya hivyo huenda akina ponda wasingefikia hapa kwa vile sasa hivi waliona hakuna anayeweza kuwafanya kitu sababu ya udhaifu wa serikali.

  Kikwete kwa vyo vyote hawezi kukwepa kitanzi hiki, ni dhaifu na yanayojilia ni matunda ya ulegelege na udhaifu wake katika kuongoza nchi.
   
 9. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Candid Scope,

  Naelewa hoja zako kimsingi, lakini bado swali langu ni je: Nini kilimfanya Mwalimu Kuzungumza maneno yale kama nilivyoyaweka kwenye bandiko langu namba moja? Mwalimu anazumgumzia hatari ya kutoweka amani na utulivu kwa vigezo alivyotoa, na hii ilikuwa ni miaka kumi na nane kabla awamu ya nne haijaingia madarakani. Umejadili kwamba awamu ya pili na ya tatu, uongozi wa nchi ulikuwa makini zaidi katika kulinda amani na utulivu, na ukatoa mfano wa jitihada za Mrema na viongozi wa dini; Je, unadhani Tiba dhidi ya machafuko, ya dini kwa mfano ilipatikana katika awamu zilizopita au kilichopatikana ilikuwa ni dawa za kupunguza tu maumivu?

  Kwa mtazamo wangu, tatizo lililopo sasa linatokana na nchi kukosa dira na mwelekeo ambao unakubalika na watanzania wote, dira ambayo ina inspire, inajenga matumaini, inajenga uzalendo, dira inayozingatia umuhimu wa equal treatment & equal opportunity kwa watanzania wote katika social, political and economic spheres, bila ya kujali dini, au ukabila n.k; Ukosefu wa Dira ya namna hiyo kitaifa imezaa "Ombwe", ambalo sasa limeanza kujazwa na Ethnicism, Racism, Religiousism, Chauvism n.k;

  Kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu, ombwe hili halijaanzia awamu ya nne, badala yake, kinachotokea ni kwamba chini ya awamu ya nne, ombwe hili limezidi kuwa kubwa, ingawa sio awamu ya nne iliyojenga mazingira ya ujio wa ombwe hilo; Awamu zilizopita hazikuja na tiba kamili au chanjo dhidi ya tatizo lililopo, badala yake, dawa ya kupunguza maumivu, na ugonjwa huo umeshika kasi tena awamu ya nne;
   
 10. T

  TMwamafupa Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na bandiko la 9 kuhusu kutufanyia kazi tatizo la kimsingi la tija ndogo katika uzalishaji mali kukidhi mahitaji ya kiuchumi ya nchi.Utawala wa Mwalimu uliweka Azimio la Arusha kama hatua ya awali kukidhi mahitaji ya kiuchumi na kijamii.Hali hii ilisaidia kuwapa matumaini Wananchi juu ya Uongozi wao kuwa unajishughulisha kuwajengea hali nzuri ya maisha yao.Ilikuwa ni bahati mbaya sana hali ya uzalishaji mali kupitia mashirika ya umma ulianza kuzorota baada ya vita ya Kagera mwanzoni mwa mwaka 1980.

  Baada ya hali hiyo kujitokeza,utawala wa Mzee Alli Hassan Mwinyi ukaingia na siasa ya ulebarali kwa ajili ya kurekebisha uchumi ambao ulikuwa umedumaa.Marekebisho yalienda sambamba na kulegeza masharti ya umiliki wa fedha za kigeni na uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje.Hali hiyo ilishuhudia uingizaji wa bidhaa kutoka nje na kupunguza hali ya ukosefu wa bidhaa kwenye soko la ndani.

  Bahati mbaya sera hiyo haikwenda sambamba na uboreshaji wa uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za ndani na matokeo yake ilichangia kujitokeza kwa nakisi kubwa ya urari wa biashara ya nje.Hali hii ikasababisha kushuka kwa thamani ya sarafu ya ndani na kusababisha mfumuko wa bei.Uzalishai viwandani na masahambani ukashuka na kusababisha upunguzaji wa wafanyakazi na ukosefu wa ajira kwenye miaka ya 90 hadi 2000.

  Ulipoingia utawala wa Rais Mkapa kulikuwa na ubinafsishaji wa mashirika ya umma na kufungulia milango kwa uchimbaji madini ya dhahabu.Hali hii ilienda samamba na makusanyo ya kodi ya serikali kuongezeka na kuongeza uwezo wa serikali kutoa huduma za kijamii.Bahati mbaya utawala huo ukaasisi uporaji mali wa kimfumo na kushamiri kwa rushwa nchini na ukandamizaji wa demokrasia.Kipindi hiki dalili zozote za ghasia zilikuwa zikizimwa kwa nguvu kubwa za kidola(Mwembechai 1996 na Kisiasa pemba 2001.

  Kuingia kwa utawala wa Rais Kikwete kulikuja pamoja na uvumilivu wa kisiasa na kidini,hali iliyowapa mwanya wa uhuru mkubwa wa kutoa maoni.Hali hii haikudumu sana baada ya kugundulika skandali ya benki kuu ambayo ilisababisha kupungua kwa imani ya Wananchi kwa Serikali.Mbaya zaidi majina ya wahusika wakubwa kutajwa hadharani na bila ya kuchukuliwa hatua.Hapa ndo tunashuhudia ghasia za kisiasa na kidini kwa sababu wananchi wamekosa imani kwa uongozi wa kisiasa.
   
 11. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Tmwamafupa,

  Asante sana kwa somo lako zuri; Kwa mtazamo wa hoja yako, ni dhahiri kwamba utawala wa TANU/CCM ndiye mjenzi wa amani na utulivu, lakini utawala huo huo umeshindwa kusimamia mabadiliko ambayo wananchi wengi waliyategemea baada ya uhuru kupitia TANU na baadae CCM; Ni kutokana na wananchi kuanza kukata tamaa ya uongozi wa CCM, joto la Volcano analozungumzia Mwalimu Nyerere ndio linazidi kupanda; Vinginevyo nimegundua kwamba haukutaja Chama chochote zaidi ya CCM ingawa indirectly kupitia viongozi wake wakuu, na pengine hii ni ishara kwamba tatizo sio chama bali viongozi? Pia hakuna sehemu umejadili chama cha upinzani, zaidi kutaja CUF indirectly kupitia mauaji ya mwembechai, na pengine hii ni ishara kwamba vyama vya upinzani ni victims tu wa hamasa ya umma uliokata tamaa?

  Tunachojifunza kutoka kwenye hoja yako ni mambo matatu makubwa:

  Kwanza, machafuko yanayonyemelea nchi yetu yanatokana na wananchi wengi kuwa na KIU ya Demokrasia inayozaa Equal Opportunity & Equal Treatment for all - bila ya kujali tofauti za kidini, kabila n.k;

  Pili, wananchi wana KIU ya kupata haki zao za kikatiba– Social, Economic and Political justice, na ni kutokana na ukosefu wa haki hizi, wananchi ndio wameanza kuamka na kuchukua hatua, lakini kwa kuanzia, kwa kutumia vyama vya siasa nje ya CCM ambavyo wanahisi vina uwezo wa kutimiza matarajio na ndoto zao; KIU hii ya wananchi kwa vile ni ya muda mrefu na imeota mizizi mirefu katika sehemu na kada mbalimbali za jamii, taratibu ‘expression of discontent' inaanza kujitokeza kupitia mlango wa UDINI, kwani ni dhahiri kuna hoja ya msingi hapa kwamba waumini wa dini moja hawakupata fursa sawa ikifananishwa na dini nyingine; Na tusipokuwa waangalifu, kwa vile pia yapo makabila mengi ambayo yanaendelea kuamini kwamba hayakupata fursa sawa kama makabila mengine, tunaweza kuhamia katika machafuko ya kikabila;

  Na somo la tatu hapa ni kwamba – Chadema haihusiki moja kwa moja na vurugu hizi, na kama ni kuhusika, basi ni kupitia kauli ya Mwalimu Nyerere (1995), niliyoiweka kwenye bandiko langu namba moja kwamba:

  "Watanzania wanataka Mabadiliko, na Wasipoyapata CCM, watayatafuta kupitia Chama Kingine"
   
 12. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Idadi kubwa ya Vijana Ndani Ya Taifa
  Hiki ni kirutubisho cha pili cha machafuko ndani ya nchi; Suala hili linaenda sambamba na lile la awali – yani tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana; Lakini kwa kuongezea tu, kwa mujibu wa African Economic Outlook (2010), zaidi ya 60% ya watanzania hawajavuka umri wa miaka 25, na inakisiwa kwamba ifikapo mwaka 2015, idadi hii itaongezeka na kufikia 75% ya jumla ya idadi ya watanzania; Kwa maana hii, ifikapo mwaka 2015, watanzania zaidi ya milioni 33 watakuwa chini ya umri wa miaka 25; Hili ndio “TIMING BOMB” ambalo wanasiasa mbalimbali wamekuwa wanajaribu kulijadili kisiasa;  Ndugu Mchambuzi
  Nimefurahishwa sana na ujenzi wa hoja zako. Kwa ujumla hoja yako ni imara na madhubuti. Nami nitachangia kwa ufupi sana maeneo mawili yanayohusu ajira kwa vijana na vipato vya watanzania. Tunaweza kuonekana kuwa tu wakorofi au tuko katika mstari wa kupinga lakini ukweli utabaki kuwa ukweli tu na ni lazima vijana wawe makini katika kupokea ujumbe mbalimbali wa kisiasa hasa kwenye zama hizi ambapo hali ya maisha inazidi kuwa mbaya. ni sahihi kuwa wote tunaamka asubuhi kuelekea kazini na tunarudi majumbani tukiwa hatuna makovu. ni sahihi kabisa. Lakini je tumewahi kujiuliza hali hiyo imeliwezeshaje taifa letu kuondokana na umaskini.

  Mfano rahisi tu unapozungumza vijana na ajira ungetarajia Wizara ya Kazi na Ajira ndiyo ingekuwa Wizara ya Vijana lakini ukiwapeleka Wizara ya Utamaduni na Michezo matarajio yako ni nini? Hivi tuna fikra angalifu kweli? Hebu tazama katika kila kikao cha Bunge kuanzia 2008 kumekuwa na wazo la kuanzisha Benki ya Vijana. Iko wapi. nani anasimamia hili na kwanini hawajibishwi hadi sasa kwa kushindwa hata kuandaa muswaada wa kuanzishwa kwa benki hiyo. Hivi kuna Sera ya kweli ya maendeleo ya Vijana? Angalia vijana wanavyotangatanga kutafuta mikopo ya elimu ya juu, angalia idadi yao inavyozidi kuongezeka mitaani wengi wakiwa wachuuzi.Yuko wapi mpanga mipango yao ili nguvu hiyo ya vijana iweze kutumika ipasavyo.

  Kuhusu hali ya vipato vya watanzania hili linatia uchungu mkubwa kwa kuwa bajeti zetu kila mwaka zimelenga katika kutatua matatizo ya viongozi badala ya kukwamua matatizo ya wananchi. Hakuna siri asilimia 90 ya kazi za Serikali ni kuangalia Waziri au Mkuu wa Mkoa au Katibu Mkuu hana nini. Bajeti au fedha za Serikali zipo kwa ajili ya kununua Fenicha, Magari ya kifahari, kujenga mabanda ya kuku kwenye nyumba za Serikali, kununua mafuta ya kukimbiza watoto wa wakubwa shuleni na wake zao sokoni. Hali hii imefanya watumishi wengi kukata tamaa na baadhi yao kujiingiza kwenye hujuma. Kwenye hali kama hii Ndugu Mchambuzi unatarajia nini? Ni wazi kuwa kutatokea mifarakano ya jamii kwa kisingizio cha dini, ukabila na siasa. Wenye kudhibiti mali watatumia kila namna ya nguvu ama kuua au kuzusha mambo yasiyo na msingi ili mradi tu waendelee kufaidi rasilimali za nchi.


  Hebu tazama mawaziri wetu, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya walivyo busy kutafuta ujumbe wa NEC (CCM) kwa kutumia magari, mafuta na posho za umma. Hivi kwa mtindo huu nani amebaki ofisini kufikiri kwa ajili ya wananchi? Tunachokiona iwe isiwe Tanzania isipopata mabadiliko ya msingi itaingia kwenye migogoro mikubwa zaidi ya hii tunayoiona sasa ya kuwaua akina Mwangosi.   
 13. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Nsaji Mpoki,

  Nashukuru sana kwa mchango wako, lakini hasa kwa kutambua umuhimu wa mjadala huu; Kimsingi, nakubaliana na hoja zako, na naweza kuzigawanya katika makundi makuu mawili – kwanza ni Ulakini juu ya Umakini wa Serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa Vijana Tanzania, na pili, ni suala la Ubinafsi wa viongozi wetu;

  Nikianza na suala la kwanza – nakubaliana na wewe kwamba kuna kila dalili kwamba suala la ajira hasa kwa vijana, kisera halipewi uzito unaostahili; Na ushahidi juu ya hili unaweza patikana kupitia hoja yako pia juu ya jinsi gani wizara ya ajira ilivyochanganywa na mambo mengine ambayo kimsingi hayalengi kuwajenga watoto wetu kiakili i.e. ‘mental capability' bali the ‘physical' – michezo n.k; Wizara ya elimu inajulikana kwa mapungufu mengi katika suala zima la kujengea watoto/vijana wetu ‘the required capabilities' ili waweze kupambana na mahitaji ya soko la ajira au kujiajiri katika uchumi wa kisasa; Ilitegemewa pengine mapungufu ya wizara ya elimu yangeboreshwa wizara ya ajira, lakini badala yake, ni dhahiri kwamba wizara zote hizi hazija jipanga katika suala la kuhakukisha watoto/vijana wetu wanapatiwa uwezo wa kupambana katika soko la ajira; Ningependa zaidi kujua ushirikiano baina ya wizara hizi katika hili ni upi na umezaa matunda yepi;

  Tatizo tulilo nalo sasahivi ni kwamba tumeamua kuachia suala la ajira kwa vijana litatuliwe zaidi na nguvu za soko; Hatuwezi fanikiwa kwa njia hii, na hakuna nchi iliyoweza fanikiwa bila ya mkono mrefu wa serikali, hasa kupitia Ujenzi wa Capabilities Kwa vijana wetu, hasa kupitia effective and a comprehensive Industrial Policy ambayo inasimamia mambo kama vile – mabadiliko ya education curriculum iendane na mahitaji ya soko, hasa technological capabilities mbalimbali, serikali kujenga/endeleza taasisi za utafiti kwa ajili ya kuongeza uelewa wa technology mbalimbali zinazoendesha uchumi wa kisasa, serikali kujenga/wekeza kwenye supporting industries, hasa za technology, ili kuja elekeza wawekezaji (FDI) kwenda kwenye manufacturing sector (technological based), ambazo zitakuwa ni viwanda MAMA kwa hizi supporting industries zitakazo anzishwa na serikali;

  Manufacturing sector kwa kawaida hutoa ajira kwa wingi, hivyo vijana wengi watanufaika; Pia muhimu ni kwa serikali kuwabana investors (FDIs) watakao wekeza kwenye manufacturing ‘to diffuse technology', ili vijana ambao watakuwa sasa na basic capabilities za technology mbalimbali waweze kuajiriwa kwa wingi kwenye VALUE CHAINS mbalimbali, huku wengine wengi wakijiajiri as Suppliers wa bidhaa au huduma mbalimbali zinazohitajika katika uchumi ambao utakuwa ni wa kisasa;

  Kuna hoja yako ya pili ambayo nayo ni muhimu sana - inayohusu ubinafsi wa viongozi; tatizo lililopo ni kwamba sisi kama jamii tumeshindwa tofautisha baina ya ajira ya utumishi wa umma na ajira ya sekta binafsi; Tumeshindwa kabisa kutambua kwamba ajira sekta ya umma au uongozi ni dhamana tu, na kazi kubwa ya mwajiriwa wa sekta hii ni kumhudumia mtanzania moja kwa moja, sio kujihudumia mwenyewe au familia yako; Badala yake, leo hii, watanzania wengi wanatamani kazi serikalini au za siasa, sio kwa sababu wanaitikia wito wa kwenda kuhudumia jamii, bali kwa sababu binafsi; na ingawa wanajua mishahara sio minono, bado wanavutiwa na uwepo wa fedha nyingi za umma ambazo wataweza kuiba kupitia mianya mbalimbali;

  Vile vile wanavutiwa na Job Security inayoendana na ajira katiak sekta yetu ya umma kwani hakuna performance assessment za maana on employees zaidi ya mtu kutakiwa uwepo kazini on time na kukaa mpaka saa ya kutoka; hata katika hili, bado watumishi wengi hukaa ofisini masaa machache sana na wengi wakati wa kazi, wengi wanashindwa kutofautisha baina na shughuli binafsi na huduma kwa umma;

  UKiingia kwenye Siasa ndio balaa zaidi kwani wengi wanaofanikiwa kuingia huko, wanaenda kibiashara zaidi; Wabunge wengi wanafadhiliwa na wafanyabisahara kupita chaguzi, na ndio maana wengi wao baada ya kupita ubunge, wanakuwa ‘busy' kurudisha fadhila za wafadhili, na matokeo yake, wanakuwa mbali na wapiga kura; Lakini tusiwalaumu wapiga kura kwani, ili kukupa KURA, wapiga Kura wanataka kwanza KULA; Tatizo hili limeshakua sugu na hata Chadema kwa mfano wakifanikiwa kwenda Ikulu, sioni jinsi gani watafanikiwa kubadilisha hili; Ni rahisi kwa chama cha siasa kupita uchaguzi majimboni bila ya kutumia sana hela kwa sababu YOU ARE AN UNDERDOG, lakini ukishakuwa chama tawala, meza huwa zinageuka;
   
 14. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Nafasi ya walionancho na wasionacho ni kubwa sana na hii hupunguza upendo/uzalendo kwa mwananchi masikini anekutana na matatizo lukuki kila iitwapo leo na hapo hapo wapo viongozi wanaoishi maisha ya hali ya juu na hawawakumbuki makabwela hawa.

  Haki katika mahakama zetu hakuna tena na matokeo yake haki imekuwa ikipatikana katika pesa pekee(vipi kwa wasio na pesa haki yao ipo wapi?).

  Viongozi wa Serikali wamegeuka wezi kwa raslimali za Wstanzania wote,fikiri kidogo hivi ndege ya jeshi inawezaje kuingia nchini kuwachukua wanyama wetu na ikatoka salama?Wale waliokuwa wakihudumu ktk kiwanja cha ndege wanajulikana kuwa ni nani na nani alikuwa zamu lakini Serikali imekuwa nziito kuwashitaki wahujumu uchumi hawa na bado wapo mtaani tu wanajilia vyao.ushahidi wa wazi kabisa lakini hatua ni hafifu.

  Jeshi la Polisi limekuwa ndio la kuondoa uhai wa raia na sio kulinda raia na mali zake.Mwangosi kauwawa ushahidi wa wazi wazi wa picha na video upo lkn mpaka leo amefikishwa mahakamani mtuhumiwa mmoja tu(polisi).Polisi wamekuwa wakitumika ktk kukandamiza demokrasia nchini,wamekuwa wakifanya mauaji bila wao kuchukuliwa hatu yaani nchi hii imekuwa sio ya kufuata sheria na wananchi wanaliona hilo toka kwa Serikali

  Nnaomba yapo mambo mengi yatakayokuwa yamechangia uvunjifu wa amani sababu nchi imekuwa kama imekosa mwenyewe.Leo maeneo ya Kariakoo vipeperushi vya maandamano vimegawiwa baadhi ya watu,VIONGOZI BADO WAMELALA USINGIZI MZITO SIJUI NI LINI WATASTUKA.
   
 15. k

  kigoda JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 1,784
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yote haya tatizo ni KIRUSI ccm. Nchi wamegawana na familia zao,uongozi wanagawana kwa kujuana, Jamani tutafika kweli?aaaaaah
   
 16. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kimsingi nakubaliana na hoja zako nyingi, lakini je, kwa mfano Chadema wakichukua nchi, tuna uhakika gani kwamba suala la kupeana madaraka kama njugu, serikali kutumia state media and resources to dominate the political landscape dhidi ya upinzani etc etc, yote haya yatatoweka? Guarantee ipo wapi? Kama ipo ni muhimu kwa chadema, in my view, kuonyesha hayo, hasa kwa kuzungumzia kwa ufasaha ili iwe kwanza, iwe a contract baina ya chadema na wananchi, lakini pili na muhimu zaidi, ili UMMA uzidi kuitofautisha Chadema na CCM as we head towards 2015; Vinginevyo, ukimuuliza mwananchi wa kawaida leo, nini tofauti ya uhakika baina ya Chadema iliyopo madarakani na CCM iliyopo benchi la upinzani, nina uhakika majibu hayatakuwa ya moja kwa moja na hayata ridhisha;

  Nasema haya kwa sababu nchi zote za afrika ambako UMMA ulivitoa vyama tawala madarakani na kuweka vyama vipya, hapakuwa na chochote kipya; ni muhimu Chadema wakafanyia kazi suala hili kwa mtindo wa some sort of a social contract baina yake na umma kama nilivyojadili;
   
 17. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ukubwa wa makamasi si wingi wa pua.
  Kichwa na makala, hasi na chanya.
  Maelezo ni kama kazi ya kupeleka shule ya uchambuzi.
  Nikili sijaelewa makusudi ya mleta mada.
  Nisamehe.
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Nadhani uelewa wako juu ya mada yangu umekuwa finyu kutokana na wewe kuingia kwenye uzi huu ukiwa tayari unayo 'a pre - determined analytical framework' ya KISIASA ambayo inaangalia Chadema inaumia wapi; In other words, umefungua uzi huu kutafuta maslahi ya Chadema; Vinginevyo mimi nimelijadili kijamii na kiuchumi zaidi, na iwapo naingiza siasa, ni from the policy point of view kwani sera haziwezi kwenda bila matumizi ya siasa; Kama nitalazimika nikutafunie, kwanza naomba uondoe uchadema katika hili na uvae utanzania, kisha zingatia kwamba suala la msingi hapa ni je:

  -Chanzo cha Vurugu katika nchi kwa mujibu wa nadharia juu ya machafuko ndani ya nchi ni zipi?
  -Je nadharia hizi zina mahusiano gani na Tanzania au Tanzania tuna virutubisho gani kati ya hivi?
  -Je, nani na nini ni cha kulaumu kutokana na uwepo wa virutubisho hivyo?
  -Je, Ufumbuzi ni nini? sio kisiasa tu, bali kiuchumi na kijamii;

  Vinginevyo huwa nakusoma sana humu na nadhani una uelewa mzito sana juu ya mwenendo wa siasa za Tanzania, hasa katika hali ya sasa ambapo CCM na Chadema vina exchange maneno kila siku kuhusu nani ni mhusika mkuu wa vurugu zinazonyemelea nchi yetu; Kwa mtu wa kiwango chako, nilitegemea maswali yale sita kwenye bandiko langu namba moja la uzi huu ungeyaelewa vizuri tu kwani yapo straightforward, bila ya kujalisha kama ungeyajadili au lah, hasa iwapo una amini kwamba Azimio la arusha lilichangia sana nchi yetu ifanikiwe kisiasa (amani, umoja na utulivu), licha ya mafanikio ya kiuchumi kuwa haba; Iwapo nitalazimika kurudia maswali yangu, yalikuwa kama ifuatavyo:

  1-Nini ni Chanzo Kikuu cha Mmomonyoko wa Amani na Utulivu Nchini Tanzania?
  2-Je, Ni Chadema? Kwa Hoja Zipi?
  3-Je, Ni Kweli Kwamba Mjenzi wa Taifa La Amani Na Utulivu Ni ‘Mwalimu Nyerere' Kupitia Azimio La Arusha?
  4-Kama Jibu Kwa Swali la Tatu ni NDIO, Kwa Vile Nyerere Hatunaye Tena na Azimio La Arusha Hatunalo Tena, JE, nini imebakia kuwa nguzo kuu ya Kulinda Amani na Utulivu Katika Nchi Yetu?
  5-Je, Ni CCM? Kwa Hoja Zipi?
  6-Kama Jibu Kwa Swali la Tatu ni HAPANA, Bila ya Kujali Itikadi Zetu Za Vyama, Nini Ni Mbadala Rasmi Wa Azimio La Arusha Ambao Unaeleweka na Unaokubaliwa na Walio Wengi Kwamba Una Manufaa Kwa Taifa, na Mbadala ambao CCM na Chadema Wote Wapo Tayari Kuufanyia Kazi, CCM ikiwa Chama Tawala au Chama Kikuu Cha Upinzani au Chadema ikiwa Chama Tawala au Chama Kikuu Cha Upinzani?

  Karibu sana kwenye mjadala na asante kwa mchango wako;
   
Loading...