Amani tunayoichezea hakika tutaikumbuka

Amani tunayoichezea hakika tutaikumbuka

Wapo wachache wanaosema aheri wali nyama vitani kuliko Ugali dagaa kwenye amani.
Mitutu ya bunduki na kukimbizana tukusikie kwa wenzetu tu.
Wengine wanaombea jeshi lichukue nchi lakini tusiombe hio hali kutokea.Kulala mwisho ni saa kumi na mbili.Tunaropoka kwa kua tuna muda wa kuyafanya haya yanayoendelea nchini
Hao hawana akili , hata Hamas waliodai Bora kufa kuliko unyonge sasa wanawataabisha Raia wao na wanatamani Amani.
 
Wasalaam,kumekua na joto kubwa la kisiasa ndani na nje ya nchi yetu. Amani imetulewesha mpaka hatuoni umuhimu wake. Viongozi wa kidini wamejipenyeza kwenye siasa na wanasiasa wamejipenyeza kwenye dini.
Kutupiana lawama ndio imekua msingi mkuu.Hawa wanasema wameonewa na wale wanasema sheria haifuatwi.
Siku amani ya nchi yetu itakapozimika tukawa kama Congo kwa tamaa za watu wachache kutaka mali na madaraka kwa nguvu hakika tutaikumbuka hii amani.
Amani, Amani,Amani hakuna,Watu wanatekwa,ukiongea Kwa hoja unaoneka muhaini,ukikaa kimya unaonekana Bwege,ukiandamana unavunja Amani!Haki hakuna kila sehemu,Amani hakuna!
 
Ndugu wa waliotekwa na kupotea wao wanao huo utulivu unaousema?
Kwa nini haujawahi kuwashauri watekaji watumie njia mbadala wa hiyo ya kuteka na kupoteza?
Mjomba nawashaurije na mimi ni mwananchi wa chini.Ntapata wapi hio fursa
 
Wasalaam,kumekua na joto kubwa la kisiasa ndani na nje ya nchi yetu. Amani imetulewesha mpaka hatuoni umuhimu wake. Viongozi wa kidini wamejipenyeza kwenye siasa na wanasiasa wamejipenyeza kwenye dini.
Kutupiana lawama ndio imekua msingi mkuu.Hawa wanasema wameonewa na wale wanasema sheria haifuatwi.
Siku amani ya nchi yetu itakapozimika tukawa kama Congo kwa tamaa za watu wachache kutaka mali na madaraka kwa nguvu hakika tutaikumbuka hii amani.
Kama hujawahi kupoteza ndugu yako utaandika haya....lakin sisi wengine tumeshazika wadogo zetu inaa uma saana tu ni vile hatuna namna.
 
Wasalaam,kumekua na joto kubwa la kisiasa ndani na nje ya nchi yetu. Amani imetulewesha mpaka hatuoni umuhimu wake. Viongozi wa kidini wamejipenyeza kwenye siasa na wanasiasa wamejipenyeza kwenye dini.
Kutupiana lawama ndio imekua msingi mkuu.Hawa wanasema wameonewa na wale wanasema sheria haifuatwi.
Siku amani ya nchi yetu itakapozimika tukawa kama Congo kwa tamaa za watu wachache kutaka mali na madaraka kwa nguvu hakika tutaikumbuka hii amani.
Yaani watawala wafanye ufisadi wa kutisha wa Kodi zetu wakope mikopo isiyojulikana ipo wapi Kisha sisi tiwaache na amani?
 
You are very right. Swala la kuhoji mambo lilishafanywa dhambi toka ngazi ya familia. Ukihoji mambo wazazi wanakuona ni mtoto usiye na adabu au mtukutu kumbe kuhoji ni haki ya msingi ya mtu yeyote mwenye akili timamu.

Tuwajenge watoto waweze kuhoji na sio kuwaswaga tu kwa interest zetu. Hali hii imetembea kwenye ngazi za familia, vitongoji, vijiji, wilaya mikoa mpaka taifa kwa ujumla.

Mtu akiwa na mamlaka anataka asihojiwe kila mtu afate anachotaka tu hata kama hakina manufaa. Mwisho tunaanza kufanyiana umafia sasa.
Washika tonge hawataki kuhojiwa ukiwahoji wanakushughulikia wamekuwa wapumbavu Tanzania upumbavu ni kipaji mpumbavu ni mtu aliyebobea kwenye jambo fulani lakini hatekelezi majukumu yake kwa weledi, hata hivyo nyazifa wanapeana tu hata kama kichwani hamna kitu mradi uwe chawa ndiyo maana CCM kuna machwa, viroboto,, kunguni na makupe

CCM kwasasa wananchi wanatuita kenge
 
Wasalaam,kumekua na joto kubwa la kisiasa ndani na nje ya nchi yetu. Amani imetulewesha mpaka hatuoni umuhimu wake. Viongozi wa kidini wamejipenyeza kwenye siasa na wanasiasa wamejipenyeza kwenye dini.
Kutupiana lawama ndio imekua msingi mkuu.Hawa wanasema wameonewa na wale wanasema sheria haifuatwi.
Siku amani ya nchi yetu itakapozimika tukawa kama Congo kwa tamaa za watu wachache kutaka mali na madaraka kwa nguvu hakika tutaikumbuka hii amani.
Yule shekhe mla wake za watu aliyesema tupate stroke umeona anajielewa kweli wapumbavu km wale ndo wanasababisha taifa kutokua na amani
 
Tanzania haijawahi kupitia hali mbaya kiasi hiki "sirikali" inafanya ukatili mwingi sana kwa kila anae wakosoa alafu wanaofanya huo ukatili wanatoka hadharani na kuanza kujisifia na kuonya wengine wakiendelea na wenyewe litawakuta jambo, hiyo ndio amani unayo izungumzia hapa? Watu wanataka haki msijifiche kwenye kichaka cha "amani ikipotea" na wakati wenye mamlaka wenyewe ndio wanao ipoteza hiyo amani, upumbavu huo
 
Wasalaam,kumekua na joto kubwa la kisiasa ndani na nje ya nchi yetu. Amani imetulewesha mpaka hatuoni umuhimu wake. Viongozi wa kidini wamejipenyeza kwenye siasa na wanasiasa wamejipenyeza kwenye dini.
Kutupiana lawama ndio imekua msingi mkuu.Hawa wanasema wameonewa na wale wanasema sheria haifuatwi.
Siku amani ya nchi yetu itakapozimika tukawa kama Congo kwa tamaa za watu wachache kutaka mali na madaraka kwa nguvu hakika tutaikumbuka hii amani.
Kujipenyeza sijui dini kwenye siasa ama siasa kwenye dini havina uzito, hayo mambo ni ya binafsi mno, huo unaitwa ni 'uhuru'.

Kule kutaka madaraka au kutaka kuendelea kutawala kwa kuteka watu, kuuwa na kupoteza ndicho kitakacholeta machofuko na amani kutoweka nchini mwetu.

Uchumi kuporomoka na maisha kuwa magumu kwa wananchi kama ilivyo sasa kwa sababu za kifisadi zinazoonekana wazi huku kakundi ka watu wachache wanaojiita waheshimiwa kuendelea kula keki ya taifa, mwisho wa siku raia wataona hawana cha kulinda wala cha kupoteza.

Na raia wakiisha amua baba, hakuna mwanasiasa laghai atakayesimama kuwanasihi ataweza, maana viongozi wote waliotegemewa kutuliza hali, wapo kimya raha mustarehe wakifurahia yanayoendelea kwa sababu wao wananeemeka.

Kushindwa kuwaelewa na kufuata ushauri wa viongozi waandamizi wastaafu kama kina Warioba waliosimama na kushauri mambo mema ya kuliponya taifa letu, tutabiri balaa na wingu jeusi lililotanda mbele yetu, tujiandae kwa madhila makubwa.

Asiyesikia la mkuu huvunjika guu, kaa ukielewa hivyo.
 
Wasalaam,kumekua na joto kubwa la kisiasa ndani na nje ya nchi yetu. Amani imetulewesha mpaka hatuoni umuhimu wake. Viongozi wa kidini wamejipenyeza kwenye siasa na wanasiasa wamejipenyeza kwenye dini.
Kutupiana lawama ndio imekua msingi mkuu.Hawa wanasema wameonewa na wale wanasema sheria haifuatwi.
Siku amani ya nchi yetu itakapozimika tukawa kama Congo kwa tamaa za watu wachache kutaka mali na madaraka kwa nguvu hakika tutaikumbuka hii amani.
Unaandika ukiwa Lumumba au bakwata?
 
Mkuu changamoto zipo lakini sidhani kwa yanayoendelea kwa sasa ndivyo inavyopaswa kua.Mimi sina upendeleo wa chama au dini. Msimamo na wimbo wangu ni amani
Tanzania kuna amani? Unajua peace ni nini ? freedom from disturbance, tranquillity. Unajua tranquility ni nini ?  A peaceful, calm state, without noise, violence, worry. Watu wakiwa na worry hapo hakuna Amani. Amani ni full package, watu wanatekwa hapo amani iko wapi ? Watu wana wasiwasi amani itakuwepo? Hichi unachokitetea ni sababu people are complaining arleady which means hakuna Amani.. . Kitendo cha watu kudai haki zao za msingi na ninyi mnawatishia kuwa wakiendelea kudai kutatokea vita na vitu kama hivyo ? tuambie nani ataanzisha vita kwa watu wanaodai haki zao? Kwanini vita itokee? Kwanini watawala huwa wanawanyamazisha watu wanaowafumbua watu kwenye haki zao, kuna faida gani wanaipata?. Umeshawahi kufikiria watu wote wanaotekwa wana kitu kimoja in common kwanini WAO tu na sio kina mwijaku? Hata ukiwa baba kwenye familia ukiona wanao hawakupi changamoto yoyote ujue wewe ni baba mjinga, changamoto huwa tunazipokea na tunazifanyia kazi.
 
Back
Top Bottom