PostGE2025 Amani ndio haki mama ya kila raia

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ebu waambie hawa wahuni, kama wanakuteka, kukuua, kulawiti, kubaka, kutesa wakati wowote una haki gani nyingine, unapataje amani?
Watu wanadai haki zao za msingi! Halafu nyinyi mnaleta porojo za amani! Yaani mnakandamiza haki zao, kwa kisingizio cha amani, kumbe lengo kuu ni kutaka tu kulinda maslahi yenu.
 
Nina uhakika hujui maana ya neno amani kwa maana yake pana.

Peace ni freedom from disturbance; tranquillity.


Kiswahili Amani ni uhuru bila kuonewa, kubughuziwa, usumbufu na mamlaka, yoyote.
Amani ya nchi ni:
*Kukosekana kwa vita, machafuko au fujo.
*Usalama wa raia na mali zao.
*Kuheshimu sheria, haki na mipaka.
*Wananchi kuishi kwa umoja bila ubaguzi na chuki.
*Serikali kufanya kazi zake kwa uadilifu na wananchi kutii taratibu.

Kwa nini ni muhimu?
✓Huwezesha elimu, biashara na maendeleo.
✓Hulinda maisha na mali.
✓Hujenga umoja na mshikamano.
✓Huweka mazingira ya ibada na utulivu wa kijamii.
 
Ni wapi nimesema SITAKI HAKI? Kulingania Amani haimaanishi Hatuitaki Haki. Tuitunze Amani kisha tuzidai haki zetu bila kusababisha madhara kwa RAIA,Mali na miundombinu yetu.
 
Ipi inatangulia amani ya mtu, watu au ya nchi?

Kama hakuna mazingira kupata amani kwa mtu, binafsi, familia, watu kwa kuhofia kutekwa, kuuwawa, kodi zao kuibiwa nchi itapataje amani?

Nini kifanyike kwanza?
 
Watu wanadai haki zao za msingi! Halafu nyinyi mnaleta porojo za amani! Yaani mnakandamiza haki zao, kwa kisingizio cha amani, kumbe lengo kuu ni kutaka tu kulinda maslahi yenu.
Wanafikiri Watanzania wote wa kizazi hiki ni mazuzu.

Amani kwao ni kuendelea kufisadi, kuiba, kuua, kutesa, kula kodi zetu, kuweka ndugu zao serikalini bila kusumbuliwa na yoyote.
 
Tumeishi Kwa amani miaka 60+ ila tafsiri yake sisi ni mafala hamna nywi nywi nasema hiviii acha kiendelee kuwaka tuu Mpaka tutakapo kubaliana hawa mapacha wawili nani atangulie. Kiwake hadi msituni TU Kwa tabia hizi kila siku mtu lazima atekwe..fala mmoja nyinyi
 


..HAKI ndio kila kitu.

..watu huandamana kudai haki, hawaandamani kudai amani.

..ukitenda HAKI utakuwa umelinda amani.

..usipotenda HAKI utachochea vurugu, machafuko, na ukosefu wa amani.
 
..HAKI ndio kila kitu.

..watu huandamana kudai haki, hawaandamani kudai amani.

..ukitenda HAKI utakuwa umelinda amani.

..usipotenda HAKI utachochea vurugu, machafuko, na ukosefu wa amani.
KIPINDI CHA UKOLONI HAKUKUWA NA HAKI, ILA AMANI ILIKUWEPO NA BABA ZETU WALISHI NA HAWAKUDHURIKA.

Sasa tumfuate YESU au PhD??

MSIKIE YESU 👇

Yohana 20:21
“Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.”

AMANI KWANZA 👇

Luka 10:5
“Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwe nyumbani humu.”

1 Wafalme 5:4
“Ila leo Bwana, Mungu wangu, amenipa amani kila upande; hakuna adui, wala tukio baya.”

PhD WANASEMA:
“HAKUNA AMANI BILA HAKI”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…