Amani karume yuko wapi?

Amani karume yuko wapi?

Makaimati

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2011
Posts
462
Reaction score
87
Katika kuadhimisha miaka 47 ya Muungano wa JMT, Kiongozi mmoja na immediate past President, Dr. Amani Karume hakuonekana.

Jee alikuwa wapi (maana hatujasikia kusairi) na inaashiria nini?

Mwenye taarifa atupe.
 
Hata Mizengo, Mkapa hawakuwepo. Kwa nini JK hakuhutubia kama ilivyo kawaida kwenye sherehe hii?
 
Alianza utaratibu wa kususia maadhimisho haya siku nyingi kidogo ndo maana hata wakaamua kuyapeleka znz ili wa waplease wa zenji labda bado anaendeleza mgomo baridi
 
Hata Mizengo, Mkapa hawakuwepo. Kwa nini JK hakuhutubia kama ilivyo kawaida kwenye sherehe hii?

ahutubie nini ilhali kila mtu anajua muungano haupo ni kiini macho na wala huhitaji kuambiwa juu ya hilo? Kwanza yeye kama President sidhani kama hata alishasoma au kuona hati ya muungano.
 
Karume amesafari na imeelezwa na Radio BBC jana jioni. Naye ni binadamu anaweza kuomba udhuru kama mambo yameingiliana na siku ya Muungano lakini zaidi hivi sasa halazimiki kama ilivyo kwa Rais aliyepo madarakani.
 
sijui ni kwanini au wanaigiza maana tukio kama hili ni la kukosa kweli mbona Mwinyi alikuwepo
 
huyu jamaa si kuna kipindi alitangazwa kuwa amepata post ya kuwa mwalimu university moja huko marekani, labda yupo huko, maana kwa zanzibar ilivyo ndogo angekuwa pale angejulikana.
 
maana kwa ninavyokua mm huyu jamaa darasa dogo sana sasa sijui amekuwa offerd na univesity gani ambayo itatoa wahitimu bomu
 
mwalimu wa kitu gani kufundisha watu kuiba au kunywa pombe hebu tuweke sawa hapo ndugu...
Chipati.
Unataka kutuhabarisha kuwa huyu "Kiongozi" pia ni kiongozi na mtaalamu katika hayo yaliyo katika rangu nyekundu?

Duh..hawa TAKUKURU...kurukuru..kulakuku hawajui habari hii?
 
Karume fisadi na moja Tanzania, kuna mambo madogo madogo yanaanza kuja nje, mfano hoteli aliyoijenga kwenye makaburi ya wakristo mweni zanzibar, pia kavunja kijiji cha wabara huko mkoa kazkazini unguja, kilikuwa kinaitwa kibanda ugali, pia akajenga hotel na hekalu.
mnataka ushahidi? nendeni kanisa la anglikana Zanzibar
 
Hata Mizengo, Mkapa hawakuwepo. Kwa nini JK hakuhutubia kama ilivyo kawaida kwenye sherehe hii?

Mhh sherehe hii kwa mujibu wa kumbukumbu yangu, huwa haina hotuba. Kinachofanyika huwa ni kukagua gwaride, kupigiwa mizinga na askari kutoa kiapo cha utii kwa Rais, na baada ya hapo ni watu kutawanyika. Huwa hakuna hotuba!!!
 
Back
Top Bottom