Am I qualified for loan?

Mama kdev

Member
Mar 30, 2016
49
32
Habari
Mimi ni mwalimu nilieajiriwa mwaka jana. Nataka kuchukua mkopo wa 7mil. Je naruhusiwa kukopa katika benki kama NMB AU CRDB? Ama katika taasisi za kukopesha kama finca, platnum au bayport? Nauliza hivi kwa sababu bado sina barua ya kuthibitishwa kazini wala tsd number kwa sababu bado hatujapewa na nina shida ya haraka.
Msaada tafadhalini
 
KWA HIYO MPAKA TUKUULIZE KUWA NI MWALIMU WA NGAZI GANI??!!!

ND'O MAANA WENGINE WANAPITA TU!
JIBAINISHE VIZURI USAIDIWE!
 
Mdogo wangu pole kwa matatizo. Sina ushauri wa wapi na vipi utakopa ila ushauri wangu ni kuhusu hao FINCA, BAYPORT NA PLATINUM. Usijaribu kabisa kukopa huko. Utajuta milele. Bora hata uende jela miezi sita kama ni issue ya kukufunga jela kuliko kukopa huko. Huko riba zinafikaga mpaka asilimia 300. Chunga sana
 
Muulize afisa uajiri wako kama wana makubaliano na benki yoyote juu ya mikopo. Otherwise ingia nmb uulizie masharti ya mikopo. Wana interest sio kubwa sana na kama hawana mkataba na mwajiri wako wanaweza kuingia sasa.
 
Kwa ufupi huwezi pewa mkopo kama mwajiri hajakudhibitisha yaani confirmation
 
Mdogo wangu pole kwa matatizo. Sina ushauri wa wapi na vipi utakopa ila ushauri wangu ni kuhusu hao FINCA, BAYPORT NA PLATINUM. Usijaribu kabisa kukopa huko. Utajuta milele. Bora hata uende jela miezi sita kama ni issue ya kukufunga jela kuliko kukopa huko. Huko riba zinafikaga mpaka asilimia 300. Chunga sana
Hahahhaha mkuuu yalikukuta Ninii but all in all mkopo unakufanya kuwa mtumwaa aseee ...
 
Ebu kaa mbali na hizo taasisi kama Finca,Bayport, Amacha,Platinum credit na vikundu kundi vingine nakushauri postal,nmb au crdb,DTB na zinginezo
 
Mdogo wangu pole kwa matatizo. Sina ushauri wa wapi na vipi utakopa ila ushauri wangu ni kuhusu hao FINCA, BAYPORT NA PLATINUM. Usijaribu kabisa kukopa huko. Utajuta milele. Bora hata uende jela miezi sita kama ni issue ya kukufunga jela kuliko kukopa huko. Huko riba zinafikaga mpaka asilimia 300. Chunga sana
Hizi ndizo taasisi pengine mbaya za kukopesha kupata kutokea duniani ulishaona wapi mtu anakopa na analipa kwa mshahara wake lakini mnamtahadharisha na tangazo ''KOPA KWA SABABU MAALUM"ukiona hivyo machale ya kwenye makalio yakupate!kifupi watumishi wengi wanazilalamikia hizo taasisi kuwa si rafiki kimakato hivyo vumilia shida zipo tu.
 
Kwa ufupi huwezi pewa mkopo kama mwajiri hajakudhibitisha yaani confirmation
Acha kupotosha umma,mimi nimeajiriwa mwaka jana kama huyo mwalimu nimekopa mwezi wa kwanza mil 1 kwa riba ya lk 1 kwa muda wa miez sita toka faidika,
 
Mwalimu fuata ushauri wa wengi! Vumilia hizo changamoto zinazokukabili zipite. Ukishathibitishwa kazini utakua na uwezo wa kukopa zaidi ya milioni 10 benki kama crdb.

Usijaribu kukopa kwenye hizo taasisi zinazowadanganya watu wenye shida kama yako kuwapa mkopo ndani ya masaa 24! Utaijutia riba yao ilivyo juu na watakurudisha nyuma kimaendeleo. Hao wanahitaji kitambulisho, atm card na salary slip za karibuni! Don't try it madam! you will regret.
 
Back
Top Bottom