Am I a loner,selfish?

Am I a loner,selfish?

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
57,769
Reaction score
129,509
Habari za Pasaka. Jana ilikuwa sikukuu hivyo nilipata mialiko. Ajabu nilikataa mialiko yote nikaamua kukaa nyumbani peke yangu siku nzima na sikuboreka hata kidogo kwasababu nishazoea na nilipanga nisitoke.

Mwaliko wa kwanza Bi Mkubwa kanipigia asubuhi,anajua nakaa mwenyewe, kaniomba niende nyumbani nikajumuike nao. Bila kujiuliza nikamjibu leo sitaweza kuja nimetoka nje ya mji wakati nimepanga kushinda nyumbani.

Baadae kanipigia binamu wangu,me, kaniomba aje nae nikamwambia leo sitakuwepo nyumbani. Wa mwisho rafiki yangu mkubwa kanipigia jioni kaniuliza kama nipo tu nyumbani anipitie tukasafishe macho maeneo fulani, huyu nilimjibu tu kuwa nipo ila leo sitoki.

Nimekaa nikajifikiria naweza kuwa mbinafsi au loner fulani bila kujijua? Maanake napenda sana kukaa mwenyewe nyumbani au naweza kwenda sehemu ya starehe peke yangu. Na kuna marafiki wananishangaa nawezaje kukaa mwenyewe siku nzima!
 
Mimi mwenyewe hivyo hivyo, kuna kipindi nataka niwe peke yangu tu, na simu sometimes sitakagi kupokea unless iwe kwa watu muhimu sana.
Wewe ni pacha wangu!!
Kawaida tu mkuu.

Familia na marafiki inabidi waelewe ulivyo.

Binafsi natumia siku zangu za mapumziko mwenyewe. Nakaa ndani mwenyewe nafanya mambo yangu.

Muhimu watu wako wakaribu wafahamu upo mzima

'miss chagga' watu kama nyie anasemaga ni 'uchoyo tu' unakusumbueni

Hata hivyo Mkuu haupo pekee yako,Mimi mwenyewe ni 'criminal' wa masherehe

Kumbe tupo wengi maanake nilikuwa najishtukia.
 
Back
Top Bottom