Alphonce Mawazo Kutokuzikwa Kesho

Alphonce Mawazo Kutokuzikwa Kesho

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Habari za hivi Pundi Zilizotufikia kutoka kanda ya ziwa na kudhibitishwa na msemaji mkuu wa Chadema Tumaini Makene.

Kwa sasa inaweza kuthibitishwa rasmi na kwa usahihi kuwa ratiba ya kumpatia heshima za mwisho kumuaga kiongozi wetu mahiri na kipenzi cha watu Alphonce Mawazo imebadilika.

Baada ya mashauriano kupitia vikao yaliyofanyika takriban siku nzima ya jana hadi usiku, imekubalika kuwa Mawazo hatazikwa kesho Jumatatu kama ilivyokuwa imepangwa awali na leo hataagwa mjini Geita kama ambavyo wananchi walikuwa wameshataarifiwa kupitia njia mbalimbali.

Taarifa ya ratiba nyingine kuhusu utoaji heshima za mwisho kumuaga Mawazo na mazishi yake, itatolewa baadae.

Tumaini Makene

Viongozi waandamizi walioko jijini Mwanza pamoja na Wabunge wa Kambi ya Upinzani ambao wameshafika hapa jijini Mwanza watazungumza na waandishi wa habari saa sita mchana, Gold Crest Hotel. Chombo chako kinakaribishwa.

Makene.
 
mzikeni jamani,kwa nini mnamtesa namna hii marehemu?
 
Marehemu hana la kuteseka tena best... mateso yake yaliishia kwenye tone lake la mwisho la damu baada ya unyama alofanyiwa
 
Walianza na Lowassa wakahamia kwa Maalim Seif wakaenda kuzomea Bungeni wakaenda kutimuliwa kwny Msosi Dodoma sasa wamehamia kwny Maigizo ya Kutembeza mwili wa Marehemi. Kuweni na Adabu acheni familia ipumzishe mwili wa Marehemu panapostahili, ingekuwa kafa ndugu yao wangefanya hayo maigizo?
 
Sasa wewe kinachokuwasha ni nini?
 
Walianza na Lowassa wakahamia kwa Maalim Seif wakaenda kuzomea Bungeni wakaenda kutimuliwa kwny Msosi Dodoma sasa wamehamia kwny Maigizo ya Kutembeza mwili wa Marehemi. Kuweni na Adabu acheni familia ipumzishe mwili wa Marehemu panapostahili, ingekuwa kafa ndugu yao wangefanya hayo maigizo?

Ingekua na adabu usingekua una andika pumba na pointless hivi kwenye forum
 
wanaoteseka ni waliopanga,wanaofurahia na waliotumia mikono yao kumuua, Na MUNGU hatakawia kulipiza kisasi.
 
labda wanahitaji huruma katika hilo... Watu Wazima lakini wapo kama Maroboti yakuendeshwa kwa rimoti
 
Hamna kitu kama hicho. Wanamtesa kwa vipi?

kwahiyo wewe huoni jinsi wanavyomuhangaisha marehemu? Matokeo yake anaweza kuamka na kuwaambia mumzike maana Naona Mnaleta Siasa Hata kwenye Misiba
 
Ni vema ktk hili busara itumike kuondoa mvutano kwani hakuna sababu ya kuvutana kwa ajiri ya taratibu za mazishi.
Cdm na police malizeni tofauti.
 
Back
Top Bottom