Alphabeti ya Kiswahili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alphabeti ya Kiswahili.

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Lunanilo, Jul 8, 2009.

 1. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Salamu marafiki.

  Nimekuwa nikisoma mabandiko kadhaa katika ukumbi. Nimeona kuwa kuna watu wana tabia ya kufupisha maneno kama kusikia basi nakadhalika kwa kueka herufi "c" badala ya herufi "s". Kitu kinachonishangaza utaona kuwa mtu anaadika bac akimaanisha kuwa ni kifupisho cha basi au "kuckia" badala ya "kusikia".
  Kwa ulewa wangu mimi "c" siyo "si" kwa kiswahili

  c ni Che .

  Ni maoni yangu kuwa japokuwa tumeathiriwa na lugha ya kupelekeana habari kwa kutumia simu zetu za mikononi, ukatishaji wa maneno unaweza ukabadilisha maana ya neno na hata kupotosha lugha yetu.

  Shukrani.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  NOTED. Ahsantum
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Unataka kumfundisha mtu anayetafuta lughamkato ya mitaani iliyotokana na text messaging systems alifubete ya Kiswahili wakati wafuatiliaji wengi wa kiswahili wa kawaida hawaijui?

  Nia yao si kufuata istilahi na nahau iliyojaa ulimbwende yakinifu, nia ni kufupisha maneno kwa gharama yoyote ile itakayotokea kwa kiswahili.Kama unamaka kwa hili maka useme unamakia hili, lakini usitake kuwafundisha njia mjarab ya kuboronga Kiswahili.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  mi nadhani lugha yoyote duniani ni lazima ipitie kwenye misukosuko na mara nyingi matokeo yake ni eidha lugha kufa kabisa au kupanuka zaidi, kiswahili ni mchanganyiko wa lugha nyingi (kichina, hindi, english, kireno, arab,jerumani, kibantu nk), na matatizo makubwa ya kiswahili ni kukosa alfabeti zake, yaani namaanisha herufi ambazo ni tofauti na hizi za kiingereza ambazo ni za kilatini, kwa kukosa huko herufi za kiswahili kumepelekea kiswahili kuwa na muingiliano mkubwa wa kimatamshi wa kiherufi na kiingereza.
   
 5. C

  Choveki JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2009
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35

  Lugha zote zisokuwa, mwisho wake hujifia
  kiswahili kinakuwa, mwenzetu kakumbushia
  Paukwa pia pakawa, misemo ya asilia
  Shukurani we Kituko, kutukumbusha kwa hilo
   
 6. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
   
 8. D

  Dingiswayo Member

  #8
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 15
  Wakuu nadhani watu wengi huwa wanatumia maneno kwa ufupisho wakati yakiwa hayana maana kamili kama wanavyotaka hasa kwenye text messages kwa simu za mkononi..unaweza kuwa umebaki na pesa ya kuandika msg moja na unaona inaishia bila kueleweka basi pale ndo vifupisho vinapoanzia..sasa tabu ni pale haki hiyo inapomuathiri mtu na kuendelea kutumia hata pale pasipostahili.
   
 9. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante Dingiswayo. Umeelewa ninachokisema. Ukiandika katika hati mkato za mawasiliano ya simu za mkononi na rafiki zako haidhuru sana . Lakini unapoandika mada nyingine au insha kwa maoni yangu haipendezi sana. mawasiliano ya watu katika hati mkato ni juu yao wenyewe, ninakwamishwa nikiona kuwa hiyo tabia inaendelea katika mawasiliano mengine, hasa unapowasiliana na watu wasiokufahamu.

  siku njema.
   
Loading...