Ally Kamwe amekamatwa na serikali ya CCM?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Mkuu wa Mkoa ni kiongozi wa watu wote, taasisi zote na vikundi vyote. Anapokuwa anatumia pesa ya watu wote kuwapa Tabora United inayoshiriki ligi kuu sawa na timu nyingine sio sawa. Hii ni tofauti na goli la mama ambalo linatolewa kwa timu yoyote inayoshiriki mashindano makubwa. Mkuu wa mkoa anapofanya mambo kama kiongozi wa Tabora uninted atafanyiwa kama kiongozi wa mpira badala ya kiongozi wa Mkoa wa Tabora.

Mkuu wa Mkoa anapodai na kuhoji wanaoipokea Yanga Tabora aliongea kama Mkuu wa Mkoa, kiongozi wa timu ya Tabora United au kama shabiki wa Simba? Kwanini anataka watu wa mpira wamtendee kama mkuu wa Mkoa wakati yeye ametenda kama kiongozi wa timu na shabiki wa simba?

Kumkamata Ally Kama kwa mambo ya mpira amevuka mipaka na kuichonganisha CCM na wananchi bila sababu. Mkuu wa Mkoa ameichafua Yanga kwa kudai wanataka kuwahonga wachezaji wa Tabora na walimroga; huku ni kuvuka mipaka ya kimamlaka. tabora ni ya watanzania kwanini anahoji watu wanaoipokea Yanga?

Nadhani Rais anapaswa kuwakemea wateule kama hawa,
 
Hakuna aliyejuu ya sheria ,CCM ni mfano wa kuigwa kwa utawala wa sheria na utawala bora

USSR
 
Huu upuuzi mnaoleta humu kuna siku utakuja kuwatokea puani. Ni nani aliye juu ya sheria. Yaani Simba na Yanga wana uhuru wa kudhalilisha yeyote?
images (21).jpeg

Kazi mlio baki nayo ni kupindua meza acheni kujificha kwenye kichaka cha kamwe kukamatwa. Huyo belouzdad alikula chuma 4
 
Huu upuuzi mnaoleta humu kuna siku utakuja kuwatokea puani. Ni nani aliye juu ya sheria. Yaani Simba na Yanga wana uhuru wa kudhalilisha yeyote?
Kwa hiyo unataka kusema huyo Chacha ndiyo ana uhuru wa kudhalilisha wengine biala shaka! Kisa tu ni Mkuu wa Mkoa siyo!
Kitu ambacho ndugu Mwasibu hukifahamu ni kimoja tu! Kwenye haya maisha yetu ya kila siku, ukitaka kuheshimiwa na mtu yeyote yule, ni lazima uanze kwanza wewe mwenyewe kujiheshimu!

Sasa kama Mkuu wa Mkoa aliamua kujitoa ufahamu na hivyo kuingia kwenye malumbano na Yanga, ulitegemea hao Yanga wanyamaze? Mfano kama huyo Mkuu wa Mkoa angechagua kuwa neutral, na badala yake hayo malumbano ya kabla ya mechi yakaachwa kwa Ally Kamwe na Christina Mwagala; kuna mtu angemshambulia bila ya sababu?

Binafsi nadhani huyo RC alipata anachostahili. Na hata hiyo ishu ya kumshikilia Ally Kamwe bado ni kumpotezea tu muda. Ila hakuna kesi yoyote hapo.
 
Yaani wewe ukiwa mkuu wa Mkoa uko juu ya sheria? ni kweli kwenye simu za wachezaji wa tabora kuna meseji za Yanga kutaka kuwahonga? mbona ile ni hamasa tu za mpira?
 
Huu upuuzi mnaoleta humu kuna siku utakuja kuwatokea puani. Ni nani aliye juu ya sheria. Yaani Simba na Yanga wana uhuru wa kudhalilisha yeyote?
Ni kweli Yanga wana kiherehere? Mkuu gani wa mkoa anasema maneno kama hayo yaliyozoeleka kusemwa na mashabiki wa Simba na Yanga? Ameongea hivyo kama shabiki wa mpira au kama mkuu wa Mkoa?
 
Ally Kamwe tumeshamuonya mara nyingi kuwa ajue yeye ni kijana bado na kuna maisha baada ya usemaji wa Yanga. Anafanya vizuri katika kuisemea Yanga kuliko watangulizi wake lakini achunge ulimi wake utamuingiza matatizoni kama hivi.
 
Kule Mwanza mbona Ahmed Ally hakuwekwa ndani na Mtanda? Ukishindwa uwanjani unahamia polosi ikusaidie? chuki gani hii mbaya namna hii inatengenezwa kwenye taifa. Yaani hasira za Al-Masry na Tabora United mnatumia polisi. Sisi tunajua ile ahadi ya 70m ilikuwa imechangwa na akina nani kwa malengo gani. Mkuu wa Mkoa aangalie sana Yanga na Simba ni taasisi kubwa kuliko Mkuu wa ukuu wa mkoa. Hebu angalia idadi ya watu waliyotembea barabarani kuipokea na kuisindikiza Yanga ilipowasili Tabora. Hivi Mkuu wa Mkoa, Chacha anaweza kuwafanya watu kama wale wamsindikize au wampokee yeye akienda na kurudi safarini?
 
Kwa hiyo unataka kusema huyo Chacha ndiyo ana uhuru wa kudhalilisha wengine biala shaka! Kisa tu ni Mkuu wa Mkoa siyo!
Kitu ambacho ndugu Mwasibu hukifahamu ni kimoja tu! Kwenye haya maisha yetu ya kila siku, ukitaka kuheshimiwa na mtu yeyote yule, ni lazima uanze kwanza wewe mwenyewe kujiheshimu!

Sasa kama Mkuu wa Mkoa aliamua kujitoa ufahamu na hivyo kuingia kwenye malumbano na Yanga, ulitegemea hao Yanga wanyamaze? Mfano kama huyo Mkuu wa Mkoa angechagua kuwa neutral, na badala yake hayo malumbano ya kabla ya mechi yakaachwa kwa Ally Kamwe na Christina Mwagala; kuna mtu angemshambulia bila ya sababu?

Binafsi nadhani huyo RC alipata anachostahili. Na hata hiyo ishu ya kumshikilia Ally Kamwe bado ni kumpotezea tu muda. Ila hakuna kesi yoyote hapo.
Mashabiki wa Yanga hatuwezi kuandika upuuzi namna hii. Umefundishwa na wazazi wako kuwa mkubwa akikutania umrudishie tusi? Hawa wanaojiita wasemaje wadhibitiwe haraka wanaweza kuiingiza nchi kwenye machafuko.
 
Viongozi wa Tanzania ni miungu; kuwasema kwa lugha isyowafurahisha ni kutenda dhambi.
 
Ally Kamwe tumeshamuonya mara nyingi kuwa ajue yeye ni kijana bado na kuna maisha baada ya usemaji wa Yanga. Anafanya vizuri katika kuisemea Yanga kuliko watangulizi wake lakini achunge ulimi wake utamuingiza matatizoni kama hivi.
Umemuonya wewe na nani?
 
Back
Top Bottom