Nzagambaaa
JF-Expert Member
- Jan 22, 2023
- 1,298
- 2,060
Watapambana nasiii hawataweza,Yanga ni dudee kubwaaa.Kheiri kijana mwerevuu kuliko kua na mzeee asiyejua mipaka yake.
Shida yenu watoto wa 2000 hata hamjui Wakuu wa Wilaya na Mikoa walikuwa ni watu wa aina gani wakati wa utawala wa Nyerere, Mwinyi na Mkapa.Mashabiki wa Yanga hatuwezi kuandika upuuzi namna hii. Umefundishwa na wazazi wako kuwa mkubwa akikutania umrudishie tusi? Hawa wanaojiita wasemaje wadhibitiwe haraka wanaweza kuiingiza nchi kwenye machafuko.
Unanikosea heshima wewe mtoto, mimi wa 2000? Wewe unaona kumwambia Mkuu wa Mkoa "na shati lake la ubatizo" ni sahihi? Shati la ubatizo likoje? Analidharau? Anajua maana ya ubatizo kwa wakristo? Angeitaje kanzu kwa lugha ya dharau, wenye dini yao wangemwacha?Shida yenu watoto wa 2000 hata hamjui Wakuu wa Wilaya na Mikoa walikuwa ni watu wa aina gani wakati wa utawala wa Nyerere, Mwinyi na Mkapa.
Kwa taarifa yako sasa, hawa Wakuu wa Wilaya na Mikoa walianza kudharauliwa kuanzia wakati wa JK baada tu ya kuanza kuteuliwa kwa misingi ya kujuana/ushkaji! Badala ya uwezo wa mtu kwenye kuongoza pamoja na maadili yake katika jamii!!
Na ndiyo maana leo unamkuta Mkuu wa Mkoa anajigeuza kuwa msemaji/mhamasishaji wa timu ya mpira wa miguu! Na mtu huyo huyo analeta maneno ya shombo, unasema aachwe kwa sababu ni mtu mzima! Mtu mzima ndiyo asijiheshimu!!
Ally Kamwe, umefanya jambo zuri kumnyoosha huyo mpuuzi asiyejua hadhi ya cheo chake.
Na ndivyo alivyopaswa kufanya huyo dogo wenu alipochokonolewa na mwenye mamlaka...ukitaka kuheshimiwa na mtu yeyote yule, ni lazima uanze kwanza wewe mwenyewe kujiheshimu!
Kilichotokea au alichosema au namna aliyosema Ahmed Ally kule Mwanza siyo kilichotokea au alichosema au namna aliyosema Ally Kamwe Tabora.Kule Mwanza mbona Ahmed Ally hakuwekwa ndani na Mtanda? Ukishindwa uwanjani unahamia polosi ikusaidie? chuki gani hii mbaya namna hii inatengenezwa kwenye taifa. Yaani hasira za Al-Masry na Tabora United mnatumia polisi. Sisi tunajua ile ahadi ya 70m ilikuwa imechangwa na akina nani kwa malengo gani. Mkuu wa Mkoa aangalie sana Yanga na Simba ni taasisi kubwa kuliko Mkuu wa ukuu wa mkoa. Hebu angalia idadi ya watu waliyotembea barabarani kuipokea na kuisindikiza Yanga ilipowasili Tabora. Hivi Mkuu wa Mkoa, Chacha anaweza kuwafanya watu kama wale wamsindikize au wampokee yeye akienda na kurudi safarini?