All Way Up - Bongo Versions

Kafiti

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
537
220
Habari wanaburudani, kuna nyimbo ya Fat Joe na Remmy Ma inaitwa All Way Up wadau wa mziki wa kufokafoka watakuwa wameshapata kuisikia.
Hii nyimbo imekuwa ikirudiwa na wasanii tofautitofauti duniani kwa kuingiza verse zao kwenye beat ile ile aliyoitumia Fat Joe.

Sasa nimesikia All Way Up ya kiswahili leo nilivyokuwa kwenye daladala, sina hakika kama ilikuwa nyimbo kabisa au iliwekwa kama tangazo tu.

Naomba anayejua version za All Way Up ambazo zimefanywa na wasanii wa hapa nyumbani - Tanzania aweze kushare nasi hapa iwe jina la msanii aliyefanya na hata wimbo wenyewe kama inawezekana.
 
Back
Top Bottom