Uchaguzi 2020 Aliyoyatamka kwenye kampeni yote yametimia, kwanini asiapishwe?

Ilikuwa zuga tu kwamba msipo

Alikuwa anazuga tu aliposema nileteeni ccm alikuwa anamaanisha msipotaka kuniletea nitawawezesha mwenyewe

cc Sky Eclat
Yeye ni Mfalme wa Tanzania, huwezi kumtoa kwa sanduku la kura na yote anayoyataka yeye hufanyika ipasavyo.
 
Wakati wa kampeni Magufuli alisikika akisema, nileteeni diwani na mbunge wa CCM, alikua na uhakika wa ushindi wake. Yale aliyosema yote yametimia. Majimbo karibu yote ya Tanzania yame pata diwani, mbunge na Magufuli wa CCM.

Ni kwanini tupate tabu tena kuhangaika na uchaguzi 2025. Hizi pesa tunazopoteza kwenye uchaguzi ilhali Magufuli anachosema kinakua si kheri zisaidie ujenzi wa barabara za lami vijijini na maji salama ya kunywa.

Pangeni sherehe ya kumuapisha Magufuli awe Mfalme wetu. Tutekeleze kauli zake kwani tume fanya hivyo kwa miaka mitano. Ata pata nafasi ya kuteua anaowapenda wamsaidie kuuongoza ufalme wake.

Kipigo walichopata raia wasio na silaha waliojaribu tu kuandamana ili kupaza sauti ya uchaguzi usio na haki, kinatosha kutufahamisha kuwa tunatakiwa kuiabudu CCM. Ukihoji maagizo kutoka juu imekula kwako.
Hahahaha tunatafuta connection, mmetuchelewesha sana na pingapinga yenu
 
Hahahahah Mbowe alisema anajiandaa kuwa Prime Minister. Wapinzani wa nchi hii; kura hawapigi lakin vilio vingi.
Sisi wana CCM kura tumepiga za kutosha

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Kura tumepiga ila naona mliroga zile karatasi sio bure, vile vikao vya wakurugenzi wote tz na magufuli walikuwa wanajadili ninj haswa, nyingine kauli ya mama samia kuwa hata tukiwachagua wengine ila lazima wao washinde ni ushahidi tosha kuwa mmehujumu uchaguzi na kuujambia pia
 
Relax mkuu mi jana nimewacharukia maccm humu ndani mpaka wakaogopa saizi hasira zimeisha tayari
 
Wakati wa kampeni Magufuli alisikika akisema, nileteeni diwani na mbunge wa CCM, alikua na uhakika wa ushindi wake. Yale aliyosema yote yametimia. Majimbo karibu yote ya Tanzania yame pata diwani, mbunge na Magufuli wa CCM.

Ni kwanini tupate tabu tena kuhangaika na uchaguzi 2025. Hizi pesa tunazopoteza kwenye uchaguzi ilhali Magufuli anachosema kinakua si kheri zisaidie ujenzi wa barabara za lami vijijini na maji salama ya kunywa.

Pangeni sherehe ya kumuapisha Magufuli awe Mfalme wetu. Tutekeleze kauli zake kwani tume fanya hivyo kwa miaka mitano. Ata pata nafasi ya kuteua anaowapenda wamsaidie kuuongoza ufalme wake.

Kipigo walichopata raia wasio na silaha waliojaribu tu kuandamana ili kupaza sauti ya uchaguzi usio na haki, kinatosha kutufahamisha kuwa tunatakiwa kuiabudu CCM. Ukihoji maagizo kutoka juu imekula kwako.

Tunafanyia kazi mawazo yako. Asante
 
Usiwe na wasiwasi; maisha yataendelea kama kawaida; asiyekubali kushindwa siyo mshindani. Mimi nlianza na kadi ya TANU Youth League mwaka 1973, halafu baadaye nikapata kati ya CCM mwaka 1978, na baadaye nikapata kadi NCCR-Mageuzi mwaka 1995 baadaye nikapata kadi ya CHADEMA 2009. Kadi zote hizo bado ninazo na wala siyo mfuasi wa chama chochote tena na maisha yanaendelea tu.
Kwa hiyo jamaa sasa hivi una miaka 65,miaka yote umesubiri japo kupata mabadiliko lakini panatoka patupu.

But usihofu wajukuu na vitukuu vyako ipo siku watayapata.
 
Kwa hiyo jamaa sasa hivi una miaka 65,miaka yote umesubiri japo kupata mabadiliko lakini panatoka patupu.

But usihofu wajukuu na vitukuu vyako ipo siku watayapata.
Sasa umechangia nini hapo; unatishwa na umri wangu? Ni kweli mimi siyo mtoto wa jana, ndiyo maana ninachangia kwa busara ambazo wato hawajui.
 
Back
Top Bottom