Uchaguzi 2020 Aliyoyatamka kwenye kampeni yote yametimia, kwanini asiapishwe?

Mfalme Magufuli, ni muhimu ufahamu kuwa unakwenda kutawala mioyo inayovuja damu.
Lakini pia asisahau kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.

Hakuna kipindi kigumu atakachotawala kama kiki cha awamu ya pili. Serikali haitakuwa na fedha. Nyingi zilikwapuliwa na ccm kuhakikisha wanasalia madarakani. Nchi wahisani watatupiga pini kwenye misaada na mikopo.

Njia pekee anayoitegemea ni kubana matumizi. Nayo haitampa usingizi kwani hataweza kuwaongezea Watumishi mishahara. Hii itasababisha huduma kuwa duni.

Kuna uwezejano mkubwa pia kupunguza mishahara na marupurupu ya Wabunge na Madiwani au kupunguza muda wa vikao vya kawaida. Nayo haitakuwa ni dawa kwani Wateule wale hawatafurahishwa nalo.

Muda ni Mwalimu mzuri tuombe uzima.
 
Jitendeeni haki kwa kutumia neno "nikipewa" badala ya "mkipata."

Tunafahamu kuwa hiyo tatu ndiyo mliyopanga kuwapa chadema. Hatuna haja nayo.

Mpambano wa haki hauwahusu.
Kwan awali walishinda Congo ama? Si apa APA Tanzania, tuliwaaambia mapema tumewachoka mkajikuta MNA mdomo
 
Yaani Nyie Ni Vilaza kweli
Kwa Akili yenu Mliamini Huyo Mamluki Amshinde Magufuli kweli
Kutwa na Vi ID vyenu uchwara kumi kumi humu Na Kelele kama vitoto vya Ndege kwenye Kiota
Tuliwaambia Mkipata 20% mjue mmeshinda
Sasa ndiyo nimeelewa kwnini yule OCD wa Hai alimtamkia Mh Mbowe maneno yale hadharani. Kumbe uchaguzi ulishamalizika hata kabla kampeni hazijaanza.

Damu za watu wasio na hatia zimemwagika wewe unaleta kejeli?? Tusipopaza sauti zetu juu yao basi ardhi iliyomeza damu yao itawalilia.
 
Unalo hilo. .......
Mmemdanganya tundu watu wamemchoka magu. kaja mzima mzima akadondokea pua. Sasa mnaanza kukagua watu spelling kwenye mitandao. Shame on you

Kuna tofauti kubwa hapa:

"Apa apa", "amna", "apo", "apana", "ali badala ya "hali" na wenye vi maneno vya namna hiyo hawajawahi kuwa na hoja popote zaidi ya utopolo utopolo tu ambao hata bakini navyo huko usengeremani Lumumba. Waungwana hatuvihitaji!

Umesikia Mr. Delicious!
 
Ni kwanini tupate tabu tena kuhangaika na uchaguzi 2025. Hizi pesa tunazopoteza kwenye uchaguzi ilhali Magufuli anachosema kinakua si kheri zisaidie ujenzi wa barabara za lami vijijini na maji salama ya kunywa.
Kama hamtagombea mtakuwa mmetusaidia sana kama taifa!
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom