Nicole
JF-Expert Member
- Sep 7, 2012
- 4,274
- 2,514
Siku ya leo niliamka nikiwa najifeel so down kwakweli, ni kutokana na ishu moja iliyonikuta hivi karibuni.Basi hata kibaruani nilikwenda shingo upande tu kwani walinipigia simu kuniita.siku ilienda kichovuchovu na niliondoka mapema, basi wakati nimefika kwenye kituo cha daladala nikaamua niende chachi nikaonane na baba padri nimweleze yalonisibu.kanisa liko maeneo ya karibu na kibaruani na mwendo wa nusu saa kutoka kituo cha daladala.Nilifika nikaeleza hitaji langu nikaelekezwa shambani alimokuwepo baba padri akishughulika.Nikamsalimu then akanikaribisha bustanini, tukaketi na nikamweleza shida yangu.lilikuwa ni swala la kiroho ambalo kwakweli lilikuwa limenikosesha raha, basi alinipa msaada mkubwa kweli na kwa kiasi kikubwa alinitua mzigo ulokuwa umenielemea.
baada ya kumaliza kunitibu kiroho, basi baba padri akanichapa swali, akaniuliza binti una umri gani??? nikamtajia magunia ya chumvi niliyokula, then akanitundika swali lingine, akaniuliza, je una mpango gani na swala la ndoa?? (nikajisemea moyoni loh huu mwaka wa kupewa ujumbe wa ndoa) nikamjibu baba padri wajua vijana wa sikuhizi hawapendi kuingia kwenye ndoa, kwani kwao ni jukumu kubwa na miye sitaki kuuvaa mkenge so bado nasoma mazingira.Basi baba padri akaanza kutiririka ,akanambia unajua kijana wa kiume aweza kutana na binti kwenye daladala na wakifika mwisho wa safari wanaishia gesti...limekuwa jambo la kawaida kwa vijana wa sasa kwani maisha wanayachukulia kiteknolojia zaidi.wasichana wanaangalia nani mwenye qualifications za kumwezesha kufikia malengo yake hivyo ni rahisi kwao kubadili wapenzi mara kwa mara, hivyo swala la mahusiano na ndoa wengi wanayachukulia kama ajira, na mwenye vigezo ndo anapewa nafasi.swala la upendo wa dhati halipewi kipaumbele kwenye mahusiano ya siku hizi na ndo sababu ndoa nyingi hazidumu.Ila hayo(huku akinitazama usoni) yasikufanye uepuke sakramenti ya ndoa, Mungu aliiweka kwa makusudi yake ya kuendeleza kizazi na ni muhimu watoto wazaliwe, wakue na walelewe katika familia ili tuweze kupata jamii iliyo bora.Akahitimisha kwa sala nami nikaaga na kurudi kwangu.Huu ni ujumbe wa baba padri kwa vijana wote so muusome na muufanyie kazi.