Aliyewakosoa watoto wa Obama ajiuzulu

Aliyewakosoa watoto wa Obama ajiuzulu

GreenCity

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Posts
5,904
Reaction score
4,666
Mfanyakazi katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.
Bi Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi kwenye hafla ya jioni.

Rais Obama na mkewe wamejitahidi sana kuwalinda watoto wao kutokana na ndimi kali za vyombo vya habari
Baadaye Lauten alifuta maandiko yake ambayo baadaye aliyataja ya kuumiza moyo na kuudhi.
Bi Lauten pia alikuwa amewakosoa Sasha na Malia kwa kusema walionekana wasio na furaha walipokuwa wamesimama na baba yao katika hafla ya maankuli katika Ikulu ya White House.
Wakati watu wengi walihisi kwamba Sasha na Malia hawakua na furaha kuwa na baba yao katika hafla ile na hata kulizungumzia swala hilo kwenye mitandao ya kijamii,Bi Lauten aliamua kujitoa kimasomaso na kuwakosoa wasichana hao kupitia kwa Facebook.

Sasha na Malia ni miongoni mwa vijana wadogo sana kuwahi kuwa katika ikulu ya White house
Mwanamke huyo akiomba msamaha, alisema baada ya kufanya maombi na hata kuzungumza na wazazi wake na kisha kusoma maandiko yake kuwahusu Sasha na Malia, alihisi kweli aliwakera wasichana hao.
"ningependa kuomba radhi kwa wote niliowaudhi kwa matamshi yangu, na nina ahidi kujifunza na kubadilisha mwenendo wangu, '' alisema Lauten.
BBC.

huku kwetu kujiuzulu ni ishu inayogonganisha mihimili yoooote!
 
tz kuna viongozi wamekutwa na madhoroba ya hatari picha za utupu na kashfa kibao lkn bado wapo tuuu
wabishi
 
Kuwajibika nikujijengea heshima mbele ya umma ila kuwajibishwa nikujidharirisha kwa kuonekana hufai tena!
 
Kwa maneno haya, LISSU anapaswa kujitathmini kwa jinsi alivyomshambulia Rais kuhusiana na IPTL
 
Mpaka Afrika tujue umuhimu wa UWAJIBIKAJI tutakuwa tumefilisi nchi zetu.
Sababu zenyewe za kuwafanya watu wawajbike ni zipi? Za mvutano wa vitalu vya gesi? Fitina kama za akina KAfulila na MASWI?, za UKAWA kutaka kutumia sakata kumrudisha ZITTO kundini?
 
Naweza kukwambia POLE SANA.Ukweli huwa unauma lakini sina njia ya kukusaidia.Waswahili wanasema..."Ukiwa MCHOYO usiwe MROHO"Na ukiwa MUONGO USIWE MSAHAULIFU.:sick::sick:
 
10431488_893551487330184_3684652150716132875_n.jpg

kama Baba yao aliwaona tangu kwake hayo mavazi waliyoyavaa na akaenda nao kuhutubia haea mm SILIONI HILO KOSA LA MAVAZI
141130152136_turkey_640x360_getty.jpg
 
Kwa maneno haya, LISSU anapaswa kujitathmini kwa jinsi alivyomshambulia Rais kuhusiana na IPTL

KIVIPI SASA LISSU AJITATHIMINI? Rais kafanya mambo ya ajabu mara ngapi mbona hajajiuzuru? Halafu Ukweli huko pale pale..aloyasema Lissu ni ya kweli.
 
Back
Top Bottom