Aliyetuloga Watanzania ni wale watu wa Ndiyoooooo

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,867
2,000
Jana nilikuwa makini kuangalia Tv ili kujua ripoti ya Tume ya pili juu ya uchunguzi wa mchanga pamoja na ushauri wa nini kifanyike.

Raisi aliongea kwa uchungu sana, na mwisho akasema Watanzania sijui nani alituloga. Binafsi huwa siamini Dini yoyote wala Mganga yeyote chini ya jua. Mimi daima huwa namwamini Mungu Tu. Huwa naamini kuwa Kushindwa na kushinda ni hesabu ya Mtu mwenyewe. Ukiifanya vibaya lazima utalalamika kwa sababu itakupa matokeo Mabaya

Binafsi nilipatwa na mawazo mengi sana juu ya kauli ya Mkuu wetu. Ya kwamba, ni nani aliyetuloga!
Jibu ni wale watu ktk Bunge letu ambao huwa hawajui walitendalo. Haiwezekani, watu wazima ati wanapelekewa mswada wa dharura ktk Jambo Muhimu na ambalo wanajua litaigarimu nchi, halafu wao wakakubali na wakijua kabisa ni dhambi kubwa wanayoitendea Nchi.

Kwa hiyo Adui wetu Mkubwa ktk hii Nchi ni wabunge wa CCM, hili halina ubishi. Juzi tu Ndugu yetu Mwijage naye alipeleka Mswada wa dharura kuhusu Gesi yetu, na Kama kawaida Hawa Wabunge wa CCM bila aibu walisema, Ndiyooooooooo! Leo huyu mtu ni Waziri, Yeye anajua kabisa ukweli juu ya Dharura ile. Na ndiyo Maana hata Raisi ktk hotuba yake Hakuthubutu kuongelea Juu ya Mkataba wa Gesi.

Wakati wa kampeni Raisi wetu huyu huyu alikuwa anatuahidi Watanzania kuwa Hii Gesi itatupeleka ktk Uchumi wa Kati.leo kila mtu anaona aibu kumkumbusha Raisi juu ya ahadi yake ile. Kama hivi ndiyo mfumo wetu wa kuishi, basi tutatafuta Wachawi wengi Sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom