Aliyetengeneza Smart phones ni mchawi mkuu duniani!

Aliyetengeneza Smart phones ni mchawi mkuu duniani!

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,427
Reaction score
10,749
Wadau,

Hapa niko na jamaa yangu. Mi nna smart phones mbili na yeye ana moja. Sasa kila mmoja anachat kivyake. Jana kalala ka saa nane yupo watsup. Mie hapa, napiga pote pote!

Dah! Nikipiga hesabu ya muda watu wanaotumia kwa simu tangu hizi smart phones ziingie ni very big loss. Yes, kuna wakat mtu unatumia kwa mambo ya muhimu lakin most of people hutumia kwa entertainments, ujinga ujinga, na kuchezea tu! Yaani tunakuwa ka tumerogwa.

Mtu huwez ku-concentrate ktk jambo bila kukumbuka kurudi kwa smart phone yako. Huu ni uchawi uliopitiliza na tusipokuwa makini na kuji-discipline hakika tutaishia kurudi nyuma badala ya kuendelea mbele.

NB: Watanzania tumeendelea na tunaendelea katika manunuzi ya smart phones na si sekta nyingine.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Akili kichwani, kwa smartphone you can learn a lot, ni Sawa na radio na tv stations, ni mindset yako tu, kama wewe ni wa bongo movies haya.
 
Sana nakubaliana na wewe kuwa smartphones are very addictive
Ila la kusema kuwa ni mchawi mkuu duniani hapo nakupinga
 
leo shemeji yangu aliongea km wewe
analala saa nane kila siku
mi asa hv nimepunguza mana naona ntakosa mwana na maji ya moto
 
Mvumbuzi wa smart phone ni mchawi kwasababu kawafanya watu ku concentrate kwenye smart phone!? This is poor thinking, mbona huzungumzii aliyegundua nguo ambazo tunakuwa nazo mwilini muda mwingi (usiku tumejifunika, na mchana tumevaa)?
 
Tena mkuu ukizingatia tusivyojua madhara ya kuanika habari zetu na wengine kutupiana picha zisizotazamika ni taabu tupu. Ila zikitumiwa vizuri zina matokeo mema na kama ujuavyo kila kitu kina pande mbili positive na negative abarikiwe aliyegundua hii kitu.
 
Yaani kila anayepiga picha akaona nzuri anaanika mtandaoni. Mbaya zaidi wadada zangu, picha inayoonesha maungo vzr ndo anatupiaaaa! Mmmh kaaazi haswa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mvumbuzi wa smart phone ni mchawi kwasababu kawafanya watu ku concentrate kwenye smart phone!? This is poor thinking, mbona huzungumzii aliyegundua nguo ambazo tunakuwa nazo mwilini muda mwingi (usiku tumejifunika, na mchana tumevaa)?

Mkuu tofautisha Nguo na CM nguo ukishaivaa utaakuwa unajiangalia kila.wakati?
 
Sana nakubaliana na wewe kuwa smartphones are very addictive
Ila la kusema kuwa ni mchawi mkuu duniani hapo nakupinga

Mkuu hukusomaga Fasihi simulizi na fasihi andish? Uchawi si matunguli tu ya manyau nyau!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Binafsi NILIACHA KUTUMIA HIZI SIMU NIKITUMIA SANA DAMU YA VIDOLE HUWA INA VILIA NIMESHINDWA KUJUA KWA NINI? WACHA NIONEKANE MSHAMBA TU.
 
hongera kwa kuwa na smart phones 2 mkuu.
Asante mpendwa, siku hz znapatikana kirahisi tu as mchina karahisisha. Ukiona ka hela kanasumbua unanunua used! Yaani kuna jamaa nilimkuta ana nguo zimerapuka rapuka lakini alipochomoa smart phone yake sikuamini, kitu Sumsung galaxy S4! Nikajiuliza kwa nini asinunue ka mchina kama kangu na salio lililobaki anunue mavazi?
Anyway, kila mtu ana preference zake, ila ukienda na fashion sana unaishia kuumia tu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Binafsi NILIACHA KUTUMIA HIZI SIMU NIKITUMIA SANA DAMU YA VIDOLE HUWA INA VILIA NIMESHINDWA KUJUA KWA NINI? WACHA NIONEKANE MSHAMBA TU.

Hee hii kali sasa, umewahi kufuatilia tatizo ni nini? Manake ingekuwa hivyo kwa wote nazani nchi ingeamua kuweka sheria ya kutumia nokia ya tochi kwa wote! Pole sana best!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
mwisho wa kufikiria kwako ndiyo mwanzo wa matatizo yako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom