Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,804
- 1,871
Takribani miaka 3 iliyopita nilipitia Thread moja ambayo mwandishi alitabiri kuwa ACT- Wazalendo kitakuwa chama kikubwa cha upinzani na hatimaye kuwa chama cha kwanza nchini Tanzania kuitoa CCM madarakani huko mbeleni. Nilimuona mwendawazimu, na sikukubaliana naye. Leo namuona aliona mbali sana, nami binafsi namuunga mkono.
Baada ya Maalim na wafuasi wake kujiunga ACT- Wazalendo, imekifanya chama hicho kuwa na mvuto wa pekee katika pande zote za Tanzania mpaka msajili na chama tawala hawalali usingizi. Wanasababu ya kufanya hivyo kwani sasahivi ni uhalisia kuwa chama hicho kipo karibu sana kuwa kimbilio la Watanzania.
ACT- Wazalendo watachukua dola 2025 kwa sababu zifuatazo:

- Chama kimejikita katika utatuzi wa matatizo ya nchi yetu kuliko propaganda.
- Chama kimeingiza nguvu mpya (sunami) toka CUF, ambao ni timu makini katika mapambano (wasionunulika)
- Idiolijia ya chama ni madhubuti, inayolenga kutatua matatizo ya watanzania wote.
- Chama kinarekodi nzuri ya matumizi ya fedha zake kutokana na ukaguzi wa CAG, toka kisajiliwe.
- Chama hakina migogoro, kutokana na kuwa na viongozi dhabiti
- Chama hakijaundwa katika misingi ya kikanda hivyo kuwasilisha watanzania wote.
- Chama kina kiongozi kijana mwenye mtazamo chanya kwa vijana
- Bendera ya chama ina rangi ya purple ambaye ni rangi pendwa kwa wanawake, hivyo akina dada wengi watavutiwa na rangi hiyo na kujiunga nacho.
- Ni chama kisicho na papara wala mihemko pale matatizo inapokikabili
- Viongozi wake hueleza mambo magumu kwa lugha nyepesi na ya kueleweka kwa watanzania wote hata wenye shule hafifu.