MUME WA JINI
Member
- Mar 28, 2016
- 40
- 24
Habari zenu wana jamvi,
Poleni na majukumu ya kutwa nzima!
Naomba kwa wenye kuelewa wanisaidie maana nimefikiria kwa upeo wangu nimekosa jibu!!Kuna kijana alikuwa jirani yangu wakati naishi Dar es Salaam ana miaka 18 sasa,kijana huyu nilipohama alikuwa yupo darasa la tano.
Nimekutana nae huku mkoani Tanga leo na baada ya kusalimiana na mazungumzo ya hapa na pale,nilipomuuliza kuhusu masomo aliniambia kuwa
alifaulu lakini wazazi hawakuwa na uwezo wa kumsomesha akashindwa kuendelea na sekondari.
Sasa ameniomba nimsaidie kama kuna uwezekano wa yeye kurudi shule kusoma kwa kutumia nafasi ileile aliyofaulu au hata kama itashindikana nimsomeshe private school
Namuonea sana huruma lakini sina uwezo wa kumsomesha private school,nikajaribu kufikiria kuhusu yeye kurudi shule kwa nafasi ileile hapa nimekosa jibu kama itawezekana au la.
Nimeona niwashirikishe nanyi, anayejua anijulishe kama inawezekana ni hatua zipi nifuate kumsaidia?
Shukrani.