Aliyeniroga kuwa mlevi alaaniwe (ashukuriwe)[emoji1787][emoji1787]

Memtata

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
552
1,800
Nna miezi kadhaa bila kunywa pombe baada ya kunitesa na hesabu baada ya matumizi, leo nikaamua kurudi kundini kuendeleza gambe sasa raha nnayoipata hadi najikuta najilaumu kwanini nilipumzika kunywa.

Niliamua leo nitoke na hela ndogo mfukoni nna 50,000 tu, baada ya kutoka shamba (kazini) nikapita grocery ya dem mmoja hivi niliwahi kumpenda miaka hiyo lakini sikuwahi kupita nae (usiniulize, hakuna sababu ya msingi ila ushen** tu). Basi nikapiga bia zangu kadhaa pale nikaacha 15 kabla sijaondoka rafiki yangu mmoja ananipigia kunikumbusha kikao cha send off ya dada'ake nikalipa then nikaelekea kwenye kikao.

Kwenye kikao nikiwa na rafiki yangu mmoja mlevi mwenzangu akaninong'oneza "oy hapa pledge ni mia tu!" Nikamjibu "kama kawaida hatunaga hela sisi mambo ya kupledge hela nyingi zitupe mawazo..."

Muhudumu akaja nisikiza huku nikimshika kiuno nikamwambia "leta Heineken ya moto kama wewe" (ugonjwa wa kupendaga wahudumu ushashindikana kwangu) akanambia budget aloambiwa ni bia3 za bei ya taifa (buku jero) kwa kila mgeni nikamwambia 'nipe Heineken 1 change kunywa soda". Walevi bana natoa ofa hadi hela za sherehe!?

Baada ya kutoka kwenye kikao kama kawaida nikaingia ushenzini, kumbuka mfukoni nimebaki na 35 tu! Sijalewa sana najitambua moyoni naambia nafsi yangu "tulikubliana hakuna kuchezea hela".

Nilianza kuvuta mvinyo taratibu, muhudumu anayenihudumia nshamtoa moyoni kwa kasoro moja tu. Ana uso mzuri nywele ndefu (natural) lakini hana sehemu kubwa ya kukalia . Actual sipendagi ukubwa tu ila napenda mzigo ulojengeka, hatakama ni mwembamba lakini chini ya kiuno chake kuwe na kauvimbe basi . (Wale wenye mamizigo ya tembo msinisumbue nikiwa tajiri)

Tatizo limeeanzia hapa baada ya bia ya3 yule muhudumu kapita hapa naanza kuwaza kumbe sikuona vizuri wakati nimefika, alafu kila nikizungusha macho wanawake wazuri wote kama wananikonyeza . Japokuwa sijatembea na credit card lakini nshaanza kupiga hesabu kuwa nna simu naweza kuhamisha salio toka bank kuja Mpesa

Moyoni nakumbuka kabisa "tulikubaliana hakuna kuchezea hela" lakini daaah!!! Pombe ina raha sana. Naanza kujiuliza nimlaumu aliyenionyesha raha ya pombe au nimshukuru!? Kesho asubuhi msiniulize kama mnajua machungu yake but I don't care

Ujumbe huu nimeuandika live sehemu ya tukio kama kuna sehemu mkiona makosa sio mimi ni pombeee...
 
Kunyweni pombe by chalamila
Ndo tunakunywa sasa
IMG_20210529_232952_220.jpg
 
Kuna mzungu hapa kala castle tatu tu chali ..najiuliza zina uchungu kiasi gani?

Mie nakula budweiser ya baridii taratibuuuu.

Naona jamaa kanyanyuka meza ya pili, ana demu ana takroooooo najilaumu sijalewa ningeenda kumuwashia nje nimbebe mie huo uthubut ninao sana.
 
Kuna mzungu hapa kala castle tatu tu chali ..najiuliza zina uchungu kiasi gani?

Mie nakula budweiser ya baridii taratibuuuu.

Naonanjamaa kanyanyula meza ya pili ana demu ana takroooooo najilaumu sijalewa ningeenda kumuwashia nje nimbebe mie huo utubut ninao sana.
Kunywa haraka haraka ulewe haraka
 
Back
Top Bottom