
Grace Mugabe na mumewe Robert Mugabe
Mahakama moja nchini Zimbabwe imetupilia mbali baadhi ya mashtaka dhidi ya mbunge mmoja wa chama tawala anayetuhumiwa kumtusi mkewe rais wa taifa hilo Grace Mugabe.
Serikali sasa imeandaa mashtaka madogo dhidi ya mbunge huyo Justice Wadyajena.
Iwapo atapatikana na hatia kwa mashtaka hayo madogo, mbunge huyo anakabiliwa na faini ya dola 200 au kifungo cha miezi sita jela.

Bw Wadyajena ametuhumiwa kwa kumuita Bi Mugabe ''mjinga'' wakati wa kuzuka kwa mgogoro kati yake na mfuasi mwengine wa chama cha ZANU-PF katika mkutano wa kila mwaka wa chama hicho mnamo mwezi Desemba.
Bw Wadyajena ameyataja mashtaka hayo kuwa yanayolenga kumharibia jina.
Kambi mbili zimezuka katika chama tawala, kambi moja ikiwa inamuunga mkono Bi Mugabe huku nyengine ikimuunga mkono naibu wa Mugabe, Bw Emmerson Mnangagwa.
Chanzo: BBC
Last edited by a moderator: