Aliyempigisha ‘deki’ Mwalimu aigomea CWT

Nakubaliana nawe kabisa kama watanzania hatutajifunza kusema hapana, tunakoenda pabaya heshima itakuwa hamna tena. Kama kungekuwa na umuhimu wa kumueleza kitu au kumuonya angemwita ofisini kwake na kumueleza, huko ni kudhalilishana.
 
CWT NI....

.SANA yaani wanamtaka aombe radhi? kweli? hivi huyo mwalimu aliyedeki zipo sawa kichwani??? mfano asingedeki wangemfanyaje? naye hajielewi
 
Mkuu umenena jambo la maana sana,wakati wa kunyenyekea hadi upumbavu ushapita!kataa kwa nguvu zote unapoona dhahiri haki yako inapotea.Inauma sana!
 

CWT hawana ubavu wa ku kumkabiri. Kama amefanya ufidhuri huo na aliyemteua hajamfukuza, basi ujue ana baraka zake. CWT wafanye kazi ya ziada
 
Jitu lenyewe linaonekana muflisi kichwani hata kwa kuliangalia tu. Watu wanaofanya vitu vya ajabu ajabu wapewapo madaraka ukifuatilia historia zao huwa wamepitia maisha MABOVU na ya shida sana kwa kiasi ambacho tayari hali hiyo huwa imeshaathiri namna yao ya kufikiri katika mambo fulani.
 
Mbona kawaida sana, angewekwa lokapu sibora kudeki kuliko kulala ndani?, watanzania bana mambo mengine tunayakuza kweli, ni adhabu kama adhabu zingine jamani.
Kulala ndani ni kitu gani mkuu, hata ingekuwa kifungo cha maisha Kwa upande wangu ingekuwa poa tu, adhabu mbele ya wanafunzi hapo heshima hakuna tena na huyo Mwalimu nina uhakika amesha athirika kisaikilojia, ndio ile utakuta hata akipita kwenye kundi la wanafunzi wanacheka yao yeye lazima atajishtukia.. Bora kidogo ingekuwa mbele ya staff wenzake
 
Basi sawa
 
CWT acheni ubabaishaji na kutuhadaa..

Mkurugenzi amefanya kazi yake kwa nia njema ya kuwarekebisha walimu vilaza..

Hamtamuweza Mkurugenzi... Ni boss wenu
 
Mi ningekuwa mwalimu nisingedeki ***** zake, mambo ya utwana hayo. Mi sijui niko tofauti, maana tangu nilivyokuwa mtoto sikuwa na nidhamu ya uoga. Yaani kwasababu we ni boss ndio unitelee mazereu, dah haitakaa itokee hiyo! Yaani ningemwambia kama unaona darasa chafu afadhari leo umekuja utusaidie kudeki.
 
Ila walimu nidham ya uoga inazid huo ni ujinga kwa mwalim kukubali kudeki inauma sana mi ni mwalim, ila huyo cjuwi kaa vyeti ni vyake
 
Kujitambua nako ni muhimu. Teachers need to know who they are and their rights. Unaambiwa upige deki eti nawe unainama kupiga deki. Huyo teacher pia ni tatizo. Ingekuwa mimi ningeshamng'oa meno huyo mkurugenzi. Imefikia hatua sasa ili mtu fulani aonekane anafanya kazi basi amnyanyase wa chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…