Aliyemnyonga Mkewe Usingizini Aachiwa Huru Brian Thomas na mkewe enzi zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyemnyonga Mkewe Usingizini Aachiwa Huru Brian Thomas na mkewe enzi zao

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Nov 24, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Brian Thomas na mkewe enzi zao Monday, November 23, 2009 1:21 PM
  Mwanaume wa nchini Uingereza ambaye alimyonga mkewe usingizini wakati alipoota ndoto anapigana na wezi, ameachiwa huru na mahakama. Brian Thomas, 59, aliota ndoto mwizi ameingia kwenye gari lao aina ya caravan wakati alipokuwa amelala na mkewe usiku kwenye gari hilo, alimuua mkewe kwa kumkaba koo kwa nguvu akidhania anapigana na mwizi.

  Aliamka asubuhi na kugundua amemuua mke wake Christine Thomas na kuamua kuwapigia simu polisi ambapo alikamatwa na kupandishwa kizimbani kwa kosa la mauaji.

  Akitoa hukumu jaji wa kesi hiyo alisema kwamba Brian alikuwa mume mwaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa mkewe na alikuwa hajijui wakati alipokuwa akifanya kitendo hicho.

  Mahakama iliambiwa kuwa hali aliyokuwa nayo Brian imewahi kuwatokea watu 50 tu dunia nzima.

  Brian alimnyonga mkewe usingizini mwezi julai mwaka jana wakati walipokuwa kwenye vakesheni katika mji wa Aberporth, Wales.

  Brian aliota ndoto mmoja wa vijana waendesha pikipiki waliokuwa wakiwafanyia vurugu mchana wa siku hiyo, amevamia kwenye gari lao na yeye alianza kupigana naye.

  Lakini alipozinduka asubuhi aligundua amemuua mke wake aliyeishi naye miaka 40 kwenye ndoa.

  Mahakama iliambiwa kuwa Brian alikuwa na matatizo mengi ya usingizi karibia maisha yake yote na alikuwa na ugonjwa wa kutembea huku akiwa amelala.

  Alikuwa akitumia madawa mbali mbali ya usingizi, dipresheni na Parkison na aliacha kutumia madawa hayo wakati wa vakesheni hiyo kwakuwa yaliufanya uume wake ushindwe kusimama na hivyo kushindwa kufanya mapenzi na mkewe. Pia madawa hayo yalimsababishia mapungufu ya akili zake.

  Mahakama ilimuachia huru Brian ikisema kuwa hajamuua mkewe kwa kukusudia na alikuwa hajijui wakati anafanya kitendo hicho.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3598614&&Cat=2
   
Loading...