Aliyekuwa RTO Arusha alia Njaa, awa Mbeba Mafaili ofisi ya RPC

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Aliyekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha ,(RTO),Joseph Bukombe ambaye hivi karibuni alitimuliwa kwa utovu wa nidhamu ,vitendo vya rushwa na kudharau maagizo ya Mkuu wake wa Kazi,hivi sasa Analia njaa ofisini kwa RPC Arusha alikopangiwa kuwa Mbeba Mafaili mbalimbali.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wenye Magari wamedai kupatwa na usumbufu wa kila mara kupigiwa Simu na bw, Bukombe akibomu fedha baada ya mrija wake kukaushwa ghafla na Waziri mwenye dhamana ,Mh Kangi Lugola.

Tangu ametumbuliwa na kuhamishiwa ofisi ya RPC Arusha amekuwa akilalama na kutuhumu watu mbalimbali kuwa ndio chanzo cha yeye kutumbuliwa na amekuwa akisikika akidai....' yote ni maisha tu'

Hata hivyo baadhi ya askari wa Usalama barabarani jijini Arusha wamefurahishwa mno na hatua ya kutumbuliwa wakidai kuwa alitumia cheo chake kujinufaisha na kuwagawa askari makundi mawili jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Wamempongeza RTO wa sasa kuwa ni mchapakazi asiye na makundi na anasimama kwenye majukumu yake na kumtaka RPC amhamishe haraka Mkoani hapo asije akamtengenezea ajali RTO Mpya.

IMG-20190917-WA0000.jpeg
 
Haki ya nani bora kubeba boksi. What kind of life is this? Are they really happy???

Watu wanafanya kazi kwenye mazingira ya hovyo, majungu na kurogana. Kweli mnafurahi mkiamka asubuhi kwenda kazini?

Poleni aisee ngoja nirudi kumalizia kusafisha corridor ya backside area na men and women changing roons na vyoo viwili karibu na sevirce line halaf faster niende kazi nyingine.
 
Zama zileeee za kuundiwa tume zimesiha...enzi hizi mambo ni papo kwa papo ua gone hakuna ukilitimba ukileta za kuleta unapewa za uso
 
Ikiwezekana mpe mchongo jamaa maana anaweza kutumbuliwa mara ya pili akawe msafisha choo cha boss wake.
Haki ya nani bora kubeba boksi. What kind of life is this? Are they really happy???

Watu wanafanya kazi kwenye mazingira ya hovyo, majungu na kurogana. Kweli mnafurahi mkiamka asubuhi kwenda kazini?

Poleni aisee ngoja nirudi kumalizia kusafisha corridor ya backside area na men and women changing roons na vyoo viwili karibu na sevirce line halaf faster niende kazi nyingine.
 
Wewe agent wa mabasi kumbuka huyo ni Afisa mkubwa Halafu haishi kwa kutegemea Rushwa maana ni Mfanyabiashara pia na ni mtumishi wa serikali mwenye cheo kikubwa.Hata kwenye Ofisi ya RPC anakuwa msaidizi wa karibu sana wa RPC .Kama mafaili hata IGP nayo mafaili sasa wewe unafikiri atakufa njaa.

Superintendent wa polisi Siyo Cheo kidogo halafu huyo mlimtoa kwa mumsingizia Uongo kwakuwa alikataa Kupokea Rushwa na kuwatendea sheria inavyotaka.Tunajua ukweli kuwa ukisimamia ukweli jamii ya waovu itakuchukia.

Wewe unataka Bodaboda asikamatwe hivi unaakili sawasawa.Hana helment,Hana vibali anatumia pikipiki kufanyia uhalifu kadi ya pikipiki ya hana, Eti asikamatwe .Wananchi wa kawaida tumejua kuwa alionewa kwa fitina za wafanyabiashara tu .
 
Wewe agent wa mabasi kumbuka huyo ni Afisa mkubwa Halafu haishi kwa kutegemea Rushwa maana ni Mfanyabiashara pia na ni mtumishi wa serikali mwenye cheo kikubwa.Hata kwenye Ofisi ya RPC anakuwa msaidizi wa karibu sana wa RPC .Kama mafaili hata IGP nayo mafaili sasa wewe unafikiri atakufa njaa.Superintendent wa polisi Siyo Cheo kidogo halafu huyo mlimtoa kwa mumsingizia Uongo kwakuwa alikataa Kupokea Rushwa na kuwatendea sheria inavyotaka.Tunajua ukweli kuwa ukisimamia ukweli jamii ya waovu itakuchukia.Wewe unataka Bodaboda asikamatwe hivi unaakili sawasawa.Hana helment,Hana vibali anatumia pikipiki kufanyia uhalifu kadi ya pikipiki ya hana, Eti asikamatwe .Wananchi wa kawaida tumejua kuwa alionewa kwa fitina za wafanyabiashara tu .

Eti alikataa rushwa?hahah

Kipindi cha huyo RTO Arusha nadhani ndio kipindi police wamekula Rushwa kuliko kipindi chochote kwny historia ya usalama barabarani,yani hawana aibu wala uoga.
 
Taarifa kama hizi utakuta zinawafurahisha watu wake wa Karibu pamoja na ndugu kwa kuwa AFRICA ni bara gumu
 
Aliyekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha ,(RTO),Joseph Bukombe ambaye hivi karibuni alitimuliwa kwa utovu wa nidhamu ,vitendo vya rushwa na kudharau maagizo ya Mkuu wake wa Kazi,hivi sasa Analia njaa ofisini kwa RPC Arusha alikopangiwa kuwa Mbeba Mafaili mbalimbali.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wenye Magari wamedai kupatwa na usumbufu wa kila mara kupigiwa Simu na bw, Bukombe akibomu fedha baada ya mrija wake kukaushwa ghafla na Waziri mwenye dhamana ,Mh Kangi Lugola.

Tangu ametumbuliwa na kuhamishiwa ofisi ya RPC Arusha amekuwa akilalama na kutuhumu watu mbalimbali kuwa ndio chanzo cha yeye kutumbuliwa na amekuwa akisikika akidai....' yote ni maisha tu'

Hata hivyo baadhi ya askari wa Usalama barabarani jijini Arusha wamefurahishwa mno na hatua ya kutumbuliwa wakidai kuwa alitumia cheo chake kujinufaisha na kuwagawa askari makundi mawili jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Wamempongeza RTO wa sasa kuwa ni mchapakazi asiye na makundi na anasimama kwenye majukumu yake na kumtaka RPC amhamishe haraka Mkoani hapo asije akamtengenezea ajali RTO Mpya.

View attachment 1209491
Sasa hii picha ni ya yupi, wa zamani au 'mupya'?
 
Back
Top Bottom