Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

Haya mambo usiombe tu yakatokea kwenye familia yako ila ya kitokea utaona tu jamaa km wanamchelewesha
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
 
Katika hii kesi kuna dogo mmoja polisi ambae alikufa katika mazingira ya kutatanisha. Alieleza ukweli kabla hajafia gerezani. Dogo mmoja mchagga nasahau jina. Naona nafsi na imani yake ya kidini vilikua vinamsuta
Aliugua kansa ya ngozi ghafla
 
Adhabu hii ya kunyonga hadi kufa ni kiashiria kingine cha kupuuza utu wa mtu wala si kwamba inawafanya wahukumiwa kujutia makosa yao au waliobaki kuogopa kutenda makosa kama hayo.... Na ndiyo maana bado tunaendelea kusikia visa vya mtu kutekeleza mauaji ya watu kadhaa kwa sababu za kipumbavu kabisa kisha naye kujiua. Yaani ni kama inaonekana muuaji anaogopa yale maumivu ya kimwili na kisaikolojia atakayoyapata wakati wa kuendesha kesi na wakati wa kusubiria utekelezaji wa hukumu kuliko hukumu yenyewe, Pengine ndiyo maana haoni taabu kujiua mara tu! baada ya kuwa amekamilisha uharifu wake wa Mauaji.
Itoshe tu kusema kuwa Adhabu ya kunyongwa hadi kufa haitoi nafasi ya muhusika kujirekebisha wala muathirika kufurahia haki aliyopatiwa na mahakama iliyotoa adhabu hiyo bali ni MAUJI KAMA MAUAJI MENGINE. #NIMEWAZA KWA SAUTI
Nimekushangaa sana. Kwamba, adhabu ya kifo ni kukiuka utu wa mtu, pia inamnyima fursa muuaji kupata kujifunza na kujutia makosa yake,,,na haisaidii kumfurahisha marehemu aliyekatishwa uhai wake.

Unasahau kuwa adhabu yoyote inasaidia kuleta amani na mshikamano (peace & stability) katika jamii, pamoja na kushawishi jamii kufuata mkondo wa sheria. Ina maana haya matukio ya wananchi wenye hasira kali kujichukulia sheria mkononi huyaoni? Unafikiri ndugu/jamaa na marafiki wa marehemu, watamuonaje na kuishije na huyo muuaji akiwa amerudi uraiani, mf. mjane/mgane anamuona mtu aliyemuua mwenzi wake au kijana aliye katika hali ngumu ya kimaisha anaoneshwa mtu aliyemuua baba yake...nini kitafuata?

Nakutaarifu kuwa maoni yako na hao wenzio yamenikera
 
Hivi kwamfano umeibiwa pesa na mwizi aliyekuibia akakamatwa na mahakamani ikawa proved without reasonable doubt kwamba huyo jamaa ni mwizi, mahakama ikaamua kumfunga miaka say 5, hivi ile pesa yako itakua imerudi kwa huyo mwizi kufungwa? Au na wewe utapata the real happiness kwa mwizi kufungwa? Nauliza tu.
Kumpeleka mwizi kwenye vyombo vya sheria ndiyo kulipizana kisasi na ndivyo tutakavyo heshimiana
 
hahahahahahaaa, kesi ya mauaji iendeshwe na kikosi maalum kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa!! safi sanaaaaa!!
Yaani mijitu imetenda kosa la mauaji 2006,hukumu ikatoka 2016,miaka 10 baadae!Hii mijitu bado inapumua!
MTU atakae pinga kwamba haya majambazi hayakutena kosa la mauaji,inabidi aperekwe milembe apimwe akili.
Ingekuwa USA,hawa watu hawakutakiwa kushitkiwa na jeshi la polisi,ambalo wao walikuwa miongoni mwake,hapa haki haiwezi kutendeka,upelelezi wa hii kesi ilibidi ufanywe na kikosi maalum kutoka Takukuru.
 
MTU wa dizaini yako ni hatari sana wewe mwenye damu ya cdm, hujui jinsi watu wanavyocheza na vifungu vya sheria wanavipindisha pindisha mpaka waliotenda kosa wanakuwa nje wasiotenda kosa wanakuwa ndani ngoja ashinde rufaa yake uone aibu mnyama wewee
Dah mkuu yaelelea hujui chochote kuhusu hii kesi ,mkata rufaa annyongwe faster tu maana wqle marehrmu wqlikuja na madini yao ili wauze ,askari wakawakamata na kutaka kuwadhulumu ,ili kutimiza nia yao ovu wakaenda naoo msituni wakawaua na kuyachukua madini pia wakawatangaza kuwa mi majambaz
 
Kumpeleka mwizi kwenye vyombo vya sheria ndiyo kulipizana kisasi na ndivyo tutakavyo heshimiana
Bado swali langu halijajibiwa; huko kwenye vyombo vya sharia ndio watakako mfanga huyo mwizi wako say 5 years then wewe uliyeibiwa UTAKUA happy tu kwa kua kafungwa? That was the question
 
MTU wa dizaini yako ni hatari sana wewe mwenye damu ya cdm, hujui jinsi watu wanavyocheza na vifungu vya sheria wanavipindisha pindisha mpaka waliotenda kosa wanakuwa nje wasiotenda kosa wanakuwa ndani ngoja ashinde rufaa yake uone aibu mnyama wewee
Una mawazo mafupi sana ndugu yangu.
Hapo CDM wanaingiaje ktk uzi huu?

Siasa si uadui,ni namna ya kutoa mawazo yako kwa watu ili wakiona unafaa wakuchague. Kama la basi wewe ueleze kwa hoja kwanini ni tofauti na alichosema mwenzako.

Imawezekana una wivu wa kike ndiyo sababu ya matusi yote haya.
 
nimekuelewa mkuu wote sisi ni binadamu ila kutekelezwa kwa adhabu hii hakutarudisha mpendwa wako uhai wake,na sidhani utapata any closure,na haisaidii chochote maana mauaji bado ni mengi mno na ndio yanazidi.
Mbona watu wanaiba na wanafungwa jela lkn wizi haushi? Lengo la adhabu sio kwamba hilo jambo liishe big no, adhabu zipo kisheria ukikutwa na hatia uadhibiwe kadir ya makosa yako
 
Jamaa hawa wana roho dhaifu sana sijui ni shida au dhiki yani wanaweza fanya vitu mpaka mtu unashangaa
Sio roho dhaifu, ni nafasi kubwa ya kufanya chochote nyuma ya uaskari. Watu hawa wameaminiwa na jamhuri kusimamia usalama wa watu na mali zao.

Inahitaji moyo wa kujikana haswaa, sio story za humu jf,wana tofauti gani na viongozi mbali mbali wanaofisadi mali za umma, na tumewapa dhamana???
 
daaah hii kesi ilitiksa sana miaka ile..et akina zombe wakatoka dismis.. daaaah iliumiza sana..wafanya biashara wamekamatwa sinza..wamepelekwa mabwepande kuuliwa afu waliowapeleka uko na kuwaua wanatoka dismis... daaaah inaumiza sana
 
Umeandika askari aliyefyetua risasi hakuwahi kukamatwa,umeandika tena walirudisha silaha zikiwa na risasi kamili isipokuwa mmoja ambaye ndio aliyetiwa hatina na umemaliza kusema hakufyatua risasi hata moja mbona kama hueleweki? Kama hakufyetua hata moja je risasi zake zilienda wapi na alirudisha pungufu?
Duuuh.....si utulie usome vizuri...
 
Nimekushangaa sana. Kwamba, adhabu ya kifo ni kukiuka utu wa mtu, pia inamnyima fursa muuaji kupata kujifunza na kujutia makosa yake,,,na haisaidii kumfurahisha marehemu aliyekatishwa uhai wake.

Unasahau kuwa adhabu yoyote inasaidia kuleta amani na mshikamano (peace & stability) katika jamii, pamoja na kushawishi jamii kufuata mkondo wa sheria. Ina maana haya matukio ya wananchi wenye hasira kali kujichukulia sheria mkononi huyaoni? Unafikiri ndugu/jamaa na marafiki wa marehemu, watamuonaje na kuishije na huyo muuaji akiwa amerudi uraiani, mf. mjane/mgane anamuona mtu aliyemuua mwenzi wake au kijana aliye katika hali ngumu ya kimaisha anaoneshwa mtu aliyemuua baba yake...nini kitafuata?

Nakutaarifu kuwa maoni yako na hao wenzio yamenikera
Binafsi SIWEZI kushangaa wewe kuwa na maoni tofauti na ya kwangu maana natambua kila mtu ana utashi na fikra huru juu ya jambo au mtazamo fulani. Soma tena ulichokiandika kisha ukizidishe japo mara tano tu alafu ujiulize kwa mtindo huwa itakuwa inazalishwa jamii ya watu gani?
Kuhusu maoni yangu kukukera huo nao ni uongo kama ulivyo uongo mwingine maana mwenye uwezo wa kuchagua kipi kikukere na kipi kisikukere ni wewe mwenyewe na wala si nje ya utashi wako
 
Kama mtu kamiminia Risasi watu watano au katoa hiyo amri watu wauliwee na ikathibitika bhasi huyo hatakiwi Kujifunza kitu zaidi zaidi anyongwee ili wanaobaki wajifunze kuwa Cheo ni dhamana hivyo wasikitumie kunyanyasa na Kuumiza wenginee...!! Kibadeni anastahili Kunyongwaaa...
Kwanini itolewe adhabu ambayo inawafanya wengine ndiyo wajifunze kama kweli kuna kujifunza badala ya mkosaji? Kwani yeye hastahili tena nafasi ya kujutia na kujirekebisha? N kama adhabu hiyo inawafanya wengine wajifunze mbona yeye hakujifunza kabla? kwani hakuna walio wahi kuadhibiwa kwa adhabu hiyo hapo kabla?
Lakini tukifahamu kuwa 6 inaweza kuwa 9 tutaelewa umuhimu wa kulipima jambo kwa kuzingatia tuko kona gani.
 
Mtu alieua watu watano kwa kuwapiga risasi kisa mali hakuna kitu anaweza jifunza aende tu atajifunza Ahelaa labda...
 
thanks,mimi sio mke,haya ni opinions zangu ambazo ni haki yangu na next time play the ball sio mtu,maamuzi ya kihasira kama haya inaonekana maambukizi yameshaanza kukupata
Mkuu unapendekeza adhabu gani kwa wanaoua kwa kukusudia?
 
Back
Top Bottom