GE2025 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kupitia CCM, Priscus Tarimo, ameibuka mshindi katika kura za maoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Priscus Tarimo, ameibuka mshindi katika kura za maoni za chama hicho kwa kupata kura 1,539 kati ya kura halali 3,288 zilizopigwa, na hivyo kutetea nafasi yake ya kuwania tena ubunge.

Matokeo hayo yametangazwa leo, Agosti 4, 2025, na Msimamizi wa Uchaguzi wa CCM Jimbo la Moshi Mjini, Ndg. Ivan Moshi, ambaye alisema kura 10 kati ya zilizopigwa zilihesabiwa kuwa batili.

Tarimo amewazidi washindani wake wakiwemo Ibrahim Shayo aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,495, Amini Twaha (143), Samwel Ngowi (67), Theresia Komba (36), na Neema Kumburu (8).

Zoezi hilo la kupiga kura limefanyika mapema leo katika kata zote 21 za Jimbo la Moshi Mjini na limeshirikisha wagombea sita waliowania tiketi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

1754338156169.png
 
Wanawake ni vizuri sana kupigwa chini kwenye mambo ya uongozi nimependa sana matokeo ya kura chache kwa wanawake 😁😁🙏🙏
 
Wachaga wa CCM na uislamu wapi na wapi?
Ibrahim Shayo (Ibra line) labda abadili dini na kuwa mgalatia ndio ataweza kupata ubunge.

Mtu ameanza kugombea tangu akiwa kijana mpaka anazeeka lakini wapi, CCM sijui ilimkosea nini huyo kijana?
Safari hii nasikia aligawa pesa mpaka makanisani lakini ngoma bado imegonga mwamba.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Priscus Tarimo, ameibuka mshindi katika kura za maoni za chama hicho kwa kupata kura 1,539 kati ya kura halali 3,288 zilizopigwa, na hivyo kutetea nafasi yake ya kuwania tena ubunge.

Matokeo hayo yametangazwa leo, Agosti 4, 2025, na Msimamizi wa Uchaguzi wa CCM Jimbo la Moshi Mjini, Ndg. Ivan Moshi, ambaye alisema kura 10 kati ya zilizopigwa zilihesabiwa kuwa batili.

Tarimo amewazidi washindani wake wakiwemo Ibrahim Shayo aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,495, Amini Twaha (143), Samwel Ngowi (67), Theresia Komba (36), na Neema Kumburu (8).

Zoezi hilo la kupiga kura limefanyika mapema leo katika kata zote 21 za Jimbo la Moshi Mjini na limeshirikisha wagombea sita waliowania tiketi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Kwa matokeo hayo inaashiria mshindi hakuweza kuvuka 50% ya kura zote.
CCM ingekuwa ni chama chenye watu wenye akili timamu za kidemokrasia, basi kesho asubuhi na mapema kinyang'anyiro kingeendelea kwa wagombea wawili tu waliopata kura nyingi.
 
Huyu kumburu ambaye alikuwa anaturinhoshia degree mitandaoni ndiyo Kawa wa mwisho?
 
Wachaga wa CCM na uislamu wapi na wapi?
Ibrahim Shayo (Ibra line) labda abadili dini na kuwa mgalatia ndio ataweza kupata ubunge.

Mtu ameanza kugombea tangu akiwa kijana mpaka anazeeka lakini wapi, CCM sijui ilimkosea nini huyo kijana?
Safari hii nasikia aligawa pesa mpaka makanisani lakini ngoma bado imegonga mwamba.
Dah nmemuonea.huruma mwamba aachane na hizi mambo afocus kwenye biashara zake atafute hela zaidi..siasa ni stress tu na fitna nyingi...huyo alieshinda ana fitna nyingi
 
Wananchi wako na Ibra line, wajumbe wako na Ibra line, Ibrahim Mohammed Shayo ndio mbunge mteule wa Moshi mjini ... Alamsik.
 
Wachaga wa CCM na uislamu wapi na wapi?
Ibrahim Shayo (Ibra line) labda abadili dini na kuwa mgalatia ndio ataweza kupata ubunge.

Mtu ameanza kugombea tangu akiwa kijana mpaka anazeeka lakini wapi, CCM sijui ilimkosea nini huyo kijana?
Safari hii nasikia aligawa pesa mpaka makanisani lakini ngoma bado imegonga mwamba.
Mwamba katoboa
 
Back
Top Bottom