GE2025 Aliyekuwa Katibu wa Rais Magufuli, Ngussa Samike ajitosa kuwania ubunge jimbo la Sengerema

GE2025 Aliyekuwa Katibu wa Rais Magufuli, Ngussa Samike ajitosa kuwania ubunge jimbo la Sengerema

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Aliyekuwa Katibu wa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Ndugu Ngussa Samike leo Jumamosi Juni 28, 2025 amechukua Fomu ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya Chama hicho kwenye Kinyang'anyiro cha Ubunge, Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025.

Kuchukua fomu kwa Bw. Ngussa Samike kumeongeza msisimko katika kinyang'anyiro cha Ubunge katika Jimbo hilo ambalo kwasasa linaongozwa na Mhe. Hamis Tabasamu kutokana na ushawishi wake kisiasa uliopanda zaidi wakati wa utawala wa Awamu ya tano na awamu hii ya sita. Bw. Ngussa amewahi kuwa Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza na Mkoa wa Lindi katika utawala wa awamu ya sita.
1751130782867.png

Chanzo: Jambo TV
 
Back
Top Bottom