Aliyekimbia vita Sudan ajuta kurudi kwao

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,317
11,175
Ahmad Shams ni mfanyabiashara aliyekimbia vita vya wenyewe nchini Lebanon takriban miaka 17 iliyopita.

Akiwa Sudan alifanikiwa sana kibiashara baada ya kuanzisha mkahawa karibu na uwanja wa ndege wa Khartoum na jirani ya makazi ya watu wenye uwezo kimaisha.

Machafuko yalipoanza wiki mbili zilizopita alikuwa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuathiriwa na hali hiyo. Aliposikia kuna msaada wa kuhama nchi kwa kutumia meli iliyotolewa na Saudi Arabia na yeye akajipakiza pamoja na mke wake na mtoto wao wa miaka 10.

Hatimae kufika Saudi Arabia ikabidi apelekwe nchi yake ya asili ya Lebanon nchi ambayo katika miaka ya karibuni imekumbwa na machafuko makubwa yatokanayo na hali mbaya ya kiuchumi.

Alipofika nyumbani na kuhojiwa kwa uchungu akasema. Ni kweli Sudan kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini si tofauti na vile tulivyonavyo hapa kwetu.Akaongeza kwa kusema "Kama kungekuwa na uchaguzi wa nchi ya kwenda basi wala nisingelikuja Lebanon"

de371fd6fb40f9735730bb192ec1a4e4
 
Ahmad Shams ni mfanyabiashara aliyekimbia vita vya wenyewe nchini Lebanon takriban miaka 17 iliyopita. Akiwa Sudan alifanikiwa sana kibiashara baada ya kuanzisha mkahawa karibu na uwanja wa ndege wa Khartoum na jirani ya makazi ya watu wenye uwezo kimaisha.
Machafuko yalipoanza wiki mbili zilizopita alikuwa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuathiriwa na hali hiyo. Aliposikia kuna msaada wa kuhama nchi kwa kutumia meli iliyotolewa na Saudi Arabia na yeye akajipakiza pamoja na mke wake na mtoto wao wa miaka 10.Hatimae kufika Saudi Arabia ikabidi apelekwe nchi yake ya asili ya Lebanon nchi ambayo katika miaka ya karibuni imekumbwa na machafuko makubwa yatokanayo na hali mbaya ya kiuchumi.
Alipofika nyumbani na kuhojiwa kwa uchungu akasema.Ni kweli Sudan kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini si tofauti na vile tulivyonavyo hapa kwetu.Akaongeza kwa kusema "Kama kungekuwa na uchaguzi wa nchi ya kwenda basi wala nisingelikuja Lebanon."

de371fd6fb40f9735730bb192ec1a4e4
Arudi Sudani
 
Aliingia kwenye mkumbo wa kukimbia bila kujua aendako.Saudia walimsaidia kuhama tu .Hawataki mizigo kwao.
Na karudi kwao alikokimbia miaka
Wanajua Saudia hanaga hayo yeye anatoa mchango wake UN kusaidia wakimbizi kwa hela tu na sio kuwahifadhi maana cheap labour's wanatoka Bangladesh, India na Pakistan
 
Angenunua bunduki abaki akiuza mkahawa kwa kuwalinda wateja wangali wanakula.
 
Back
Top Bottom