Aliyeingia ndani ya kasri la Malkia akamatwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,814
34,196
160519152245_buckingham_palace_640x360_bbc_nocredit.jpg

Kasri la Buckingham
Mwanamme mmoja amekamatwa ndani ya makao ya kifalme nchini Uingereza ya Buckingham baada ya kuvuka ua.

Mwanamme huyo wa umri wa miaka 41 alipatikana katika uwanja wa kasri hilo dakika saba baada ya ving'ora kuanza kulia siku ya Jumatano jioni.

Mshukiwa huyo ambaye hakuwa na silaha yoyote alikamatwa kwa kushukiwa kuingia eneo linalolindwa na sasa yuko kizuizini.

160511173548_queen_640x360_bbc_nocredit.jpg

Malkia Elizabeth
Inafahamika kuwa Malkia alikuwa ndani ya kasri wakati wa kisa hicho.

Kumeshuhudiwa utata mara kadha kwenye ulinzi wa kasri la Buckingham miaka ya nyuma, kikiwemo kisa cha Michael Fagan ambaye aliingia hadi chumba cha kulala cha Malkia mwaka 1982, na kukaa kwa muda wa dakika 10 akizungumza na malkia kabla ya Malkia kufanikiwa kupiga king'ora wakati mtu huyo alipoomba sigara
chanzo.Aliyeingia ndani ya kasri la Malkia akamatwa - BBC Swahili
 
Itakuwa baharia alisikia moshi wa sigara chumbani humo akajua kumbe mwenyeji wake naye mwanachama.
Kugongea siyo mbaya kama mazingira yanaruhusu

Sent from my Nokia 3.1 using JamiiForums mobile app
 
160519152245_buckingham_palace_640x360_bbc_nocredit.jpg

Kasri la Buckingham
Mwanamme mmoja amekamatwa ndani ya makao ya kifalme nchini Uingereza ya Buckingham baada ya kuvuka ua.

Mwanamme huyo wa umri wa miaka 41 alipatikana katika uwanja wa kasri hilo dakika saba baada ya ving'ora kuanza kulia siku ya Jumatano jioni.

Mshukiwa huyo ambaye hakuwa na silaha yoyote alikamatwa kwa kushukiwa kuingia eneo linalolindwa na sasa yuko kizuizini.

160511173548_queen_640x360_bbc_nocredit.jpg

Malkia Elizabeth
Inafahamika kuwa Malkia alikuwa ndani ya kasri wakati wa kisa hicho.

Kumeshuhudiwa utata mara kadha kwenye ulinzi wa kasri la Buckingham miaka ya nyuma, kikiwemo kisa cha Michael Fagan ambaye aliingia hadi chumba cha kulala cha Malkia mwaka 1982, na kukaa kwa muda wa dakika 10 akizungumza na malkia kabla ya Malkia kufanikiwa kupiga king'ora wakati mtu huyo alipoomba sigara
chanzo.Aliyeingia ndani ya kasri la Malkia akamatwa - BBC Swahili
Kwa issues za kiulinzi fault ya dakika saba ni nyingi sana mtu kufanya tukio. Waingereza wajiangalie katika issue za ulinzi. Mara ya pili mtu anaingia kwenye kadri Buckingham🤷
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom