Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,149
- 3,088
Wakuu,
Muda mfupi baada ya kuthibitisha kuwa waasi wamemtoa Assad madarakani na Rais huyu kukimbia nchi, video za waasi wakiwa ndani ya kasri lake zimeanza kuibuka.
Huyu jamaa alikuwa anakula maisha kweli kweli na pengine ndo maana walikuwa wanataka kumtoa.
Video hizi zinasambaa sana X zikionesha ukubwa na ufahari wa jumba lake ilhali wananchi wake wakiwa wanateseka na njaa na magonjwa lukuki.
Video nyingine pia zimeonesha silaha nyingi zilizokuwemo kwenye kasri lake la kifahari.
Hapa Afrika kuna spika wa Bunge fulani alishawahi kuonesha jumba lake la kifahari. Kwa sasa watu wanaweza kujifanya hawaoni hilo kasri lake lakin mambo yakishaharibika watu watapita hapo kutuma salamu.