Aliyefanya shambulio la Ohio ni Mkimbizi kutoka Somalia

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_92703131_tv036625557.jpg

Mwanamume aliyewashambulia na kuwajeruhi watu 11 katia Chuo Kikuu cha Ohio ni asili a Kisomali na alikuwa mwanafunzi katika chuo hicho, maafisa nchini Marekani wanasema.

Abdul Razak Ali Artan, 18, alivurumisha gari hadi kwenye kundi la watu waliokuwa wakipita chuoni na kisha akatoka nje na kuanza kuwadunga kwa kisu.

Alipigwa risasi na kuuawa na maafisa wa polisi.

Mkuu wa polisi wa eneo hilo Kim Jacobs amesema wanachunguza kubaini iwapo shambulio hilo lililotokea Jumatatu asubuhi lilikuwa la kigaidi.

FBI pia wanashiriki katika uchunguzi huo.

Shambulio hilo lilitokea katika bewa la chuo kikuu hicho mjini Colombus ambalo huwa na wanafunzi takriban 60,000.

_92704204_cyxfa_ixeaarowo.jpg

Artan alikuwa mhamiaji kutoka Somalia ambaye amekuwa akiishi Marekani kama mkazi wa kudumu kwa njia halali, vyombo vya habari Marekani vimeripoti.

Alipoulizwa kwenye kikao na wanahabari iwapo hilo lilikuwa shambulio la kigaidi, mkuu wa polisi Bw Jacobs alisema: "Nafikiri tunahitaji kuchunguza hilo."

Kisha, akaongeza: "Bila shaka, ukizingatia nia ambayo ilionekana wazi, kuendesha gari kwenye njia inayotumiwa na watu kutembea, tunachunguza kubaini iwapo ni kisa kilichokuwa kimepangwa."

_92702339_tv036625407.jpg

Artan alisomea somo la usimamizi wa mipango katika kitivo cha Biashara katika chuo hicho, gazeti la Columbus Dispatch limeripoti.

Kisa kilianza mwendo wa saa nne asubuhi Jumatatu pale gari liliporuka na kuanza kuwagonga wapita nia karibu na ukumbi wa Watts Hall.

Baadaye, dereva wa gari hilo alitoka nje na kuanza kuwadunga kisu watu.

Afisa wa polisi Alan Horujko, 28, aliyekuwa karibu alimpiga risasi na kumuua katika kipindi cha chini ya dakika moja.

Chanzo: BBC
 
Yaani wanampa Trump sababu mchana kweupe! Kuna andiko moja linasema hivi; "Hapo, kuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake".

Kwa hakika hata Trump ana haki ya "kurarua mavazi yake" wala hahitaji tena ushahidi kwa sababu matendo ya watu wale ni ushahidi tosha maana wanajishuhudia wenyewe jinsi walivyo. Kinachochekesha zaidi hutasikia huko "walikotokea" wakilaani matendo ya offspring zao hizi; watajifanya kana kwamba hamna kilichotokea.
 
Yaani hii mijitu ni taabu tupu, imeshaharibu nchi zao sasa wamehamia za watu.
 
Duh hawa jamaa zetu sijui ni nini kinawasumbua?..jamaa kitu cha kwanza alivyofika college kitu cha kwanza to post in facebook ni kulalamika hakuna sehemu ya kusali kwa waislam
 
Back
Top Bottom