Aliyedhaniwa kufa Shinyanga awashtua Wafanyakaza wenzake

Mfumwa

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
1,456
42
Aliyedhaniwa kufa Shinyanga awashtua Wafanyakaza wenzake
JuliusAliyedhaniwa kufa Shinyanga awashtua Wafanyakaza wenzake
Julius Sazia, Shinyanga
WAFANYAKAZI wa Manispaa ya Shinyanga jana walipatwa na kiwewe cha mshituko baada ya kumkuta mfanyakazi mwenzao aliyedhaniwa kufa akiwa hai.

Uongozi wa manispaa hiyo ulianza maandalizi ya kuusafirisha mwili wa mfanyakazi huyo, lakini kumbe aliyefariki sio mfanyakazi wao.

Kifo cha mtu anayefanana na mfanyakazi huyo kilitokea juzi usiku baada ya kupata ajali mbaya ya pikipiki ambayo inafanana pia na ya Mfanyakazi wa Manispaa hiyo.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Hassan Mwendapole, alithibitisha kutokea tukio la kudhaniwa mtumishi wao kafariki dunia na baadaye kuonekana akiwa hai na kulieleza tukio hilo kuwa ni la kushangaza na kustaajabisha.

Akifafanua Mwendapole alisema, majira ya saa nne usiku, wakati akiwa amelala, alitumiwa ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa mfanyakazi mmoja wa Halmashauri ya Manispaa yake, aliyemtaja kwa jina moja la Asha ikimtaarifu tukio la ajali lililompata mtumishi mwenzao,Gwakila Lagile.

Alisema taarifa hiyo pia ilisema hali yake ilikuwa ni mbaya na alipelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu.

"Kwa vile namfahamu vyema mtumishi huyo, nilishtuka sana na nilikwenda hospitali ya mkoa wa Shinyanga, niliwakuta baadhi ya watumishi wa halmashauri wakiwa mapokezi na madaktari wakichukua vipimo, nilipomwangalia mgonjwa ni kweli nilikuwa namfahamu kama mtumishi wa halmashauri yangu na alikuwa ameumia sana mguu wake wa kulia kiasikwamba ulikuwa ukining'inia akiwa amelowa tope na damu mwili mzima." Alisema mstahiki Meya.

Meya huyo alisema maandalizi yote ya kumpeleka x-ray na baadaye chumba cha upasuaji yalikuwa yakiendelea vizuri kwa ushirikiano mzuri kati ya madaktari wa hospitali hiyo, daktari wa Manispaa na watumishi wa Manispaa hiyo, lakini ilipofika majira ya saa 6 usiku, aliondoka na kwenda kulala.

"Ilipofika asubuhi nilitumiwa ujumbe mfupi wa simu, kwamba mgonjwa amefariki na ndipo nilipoamka na kwenda ofisini ili kufanya mipango ya kuutibu mwili na wakati tunaingia ofisini, mimi na Mkurugenzi wa Manispaa, Jane Mutagurwa, tulishangaa kuwaona watumishi wenzetu wakikimbia kuelekea kwenye lango kuu na baadaye tulipata taarifa kuwa tuliyemdhania kuwa amefariki dunia siye." Alisema.

"Mimi nimemuangalia kwa macho yangu pale hospitali, na kwa kweli wanafanana sana, kwani hata umbo lake ni lilelile la unene, na weusi wake." Alisema Meya.

Kwa upande wake Ofisa biashara wa Manispaa ya Shinyanga, Mark Bizogwanko, alisema alikuwa wa kwanza kufika hospitali ya mkoa, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wa mtaa wa Matanda waliomuona majeruhi kuwa ni mtumishi wa halamashauri yake, muda mfupi baada ya kupata ajali.

Alisema yeye alianza kuwaarifu wafanyakazi wenzake wa kuhusu ajali hiyo na uongozi ukachukua hatua ya kufuatilia.

"Kilichojitokeza hapa ni ubinadamu wa kusaidiana haraka katika matukio ya namna hii na baada ya wananchi hao kumfikisha hospitali na uongozi wa halmashauri kufika eneo hilo, waliondoka na kurejea makwao", alisema

Alisema walipoona ndugu wa majeruhi, hawashtuki kufuatilia tukio hilo, usiku huo wa manane, walikwenda moja kwa moja kwenye mji wa majeruhi na wakamkuta nyumbani kwake akiwa amelala,"alisema .

Ofisa biashara huyo alisema ilipofika usiku huo wa manane, Gwakila Lagije, aliposikia taarifa za kifo chake wakati yeye yupo hai nyumbani, alianza kuhangaika kupiga simu kuwajulisha wafanyakazi wenzake kuwa yeye yupo salama na kusisitiza kwamba walikuwa wakimfananisha.

Mdhaniwa huyo alipiga simu, lakini simu yake ya mkononi haikuwa na salio na ndipo alipotuma ujumbe mfupi kwa mfanyakazi mmoja isemayo tafadhari nipigie.

"Ujumbe huo ulimchanganya zaidi mtumishi huyo kwa vile namba na jina vinavyodhaniwa kuwa vya marehemu alikuwa navyo kwenye simu na ilimshtua zaidi kutumiwa ujumbe na mtu ambaye tayari ni marehemu." Alisema.

Mkurugenzi mtendaji wa halamashauri ya manispaa ya Shinyanga, Jane Mutagurwa, hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwa maelezo kuwa yuko kwenye kikao maalumu na watumishi wa halmashauri hiyo.

Source: Mwananchi Read News
 
...huko shinyanga nako!

inanikumbusha enzi za Ben Kiko enzi hizo na taarifa zake katika kipindi cha majira RTD tatu usiku!
 
Back
Top Bottom