Innovator97
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 282
- 397
Moshi. Wakati Shwaibu Jumanne akitafakari jinsi ya kuanza tena maisha uraiani, mambo mawili bado yanamtesa baada ya kukaa mahabusu kwa miaka mitano.
Jumanne, maarufu kwa jina la Mredii, ndiye pekee aliyeepuka hukumu ya kifo wakati Mahakama Kuu ilipotoa hukumu dhidi ya watu sita walioshtakiwa kwa kosa la kumuua mfanyabiashara maarufu wa Mirerani mkoani Manyara, Erasto Msuya.
Washtakiwa wenzake watano wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa, lakini Mredii amerudi uraiani akitafakari maisha mapya baada ya kusimama kazi yake ya uchimbaji madini kwa miaka mitano.
Hata hivyo, tafakuri hiyo inakabiliwa na kumbukumbu mbaya ya tukio lake; kuanzia alipokamatwa hadi maisha ya mahabusu.
“Moja ya mambo ambayo sitakaa niyasahau ni maumivu niliyoyapata wakati nilipokamatwa,” anasema Mrediii katika mahojiano maalumu na Mwananchi baada ya kuachiwa huru.
“Kipigo nilichokipata mikononi mwa polisi kimemsababishia kilema na maumivu.”
Pamoja na kwamba hakusema bayana katika mazungumzo na Mwananchi, Mredii aliiambia mahakama wakati wa utetezi kuwa aliteswa na polisi hadi kupewa ulemavu, ikiwamo kuhasiwa.
Kutokana na kuhasiwa, Mredii alidai aliamua kumpa talaka mmoja ya wake zake, aliyemtaja kuwa ni Zuhura Hassan kwa vile alikuwa hana uwezo tena kama mwanamume. Amebakiwa na mkewe anayeitwa Adile Juma.
Akiongozwa na wakili wake Majura Magafu kutoa utetezi wake, Mredii alidai mbali na kuhasiwa, polisi walimvunja mara mbili mguu wa kushoto na mara moja mguu wa kulia.
Alisema wakati fulani walimfunga kamba na kumning’iniza kama mbuzi aliyebanikwa.
“Kwa hayo mateso niliyopata hapo kituoni nimekuwa mlemavu. Niliwekwa staili ya mbuzi anayechomwa nikiwa sina nguo,” alidai mahakamani.
Katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Mredii alisema hakupata matibabu mazuri kutokana na kipigo hicho na kwamba kwa vile sasa yuko huru, moja ya vipaumbele vyake ni kupata matibabu sahihi ya afya yake.
Anasema jambo jingine ambalo hatalisahau ni kulazimishwa kulala saa 9:00 alasiri na kufungiwa vyumbani hata kama huna usingizi. “Wakati mwingine watu wako nje kwenye shughuli zao, lakini sisi tunalazimishwa kulala,” alisema Mredii.
“Hili jambo haliwezi kutoka kwenye akili yangu kwa haraka na litanisumbua kwa muda mrefu sana.
“Kuanzia saa 9:00 (alasiri) mtu unafungiwa ndani, unaambiwa ulale. Kwa kweli yale yalikuwa mateso makubwa kwangu. Halafu chumba kimoja tunalala watu 18 hadi 27. Kwa kweli sitakaa niyasahau maisha haya.”
Hali hiyo ndiyo inamfanya ashauri vijana na watu wengine kutojihusisha na mambo ambayo yanaweza kusababisha wapelekwee gerezani.
“Waepuke kufanya jambo lolote litakalowafanya wapelekwe gerezani kwa kuwa kule ni mahali pa kudhalilisha sana,” anasema.
“Mtu unapokuwa gerezani unakuchukuliwa kama mhalifu na unapokuwa kwenye lile karandinga watu wanaona wewe ni mhalifu na wengine wanakuita mwizi bila kujua ni kosa gani limekupeleka gerezani".
Source : Mwananchi