Alitaka kuniibia mke, mzee wa hekima akaokoa jahazi

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,421
40,409
Mwaka 2008 niliona shamba la ekari 23 linatangazwa kuuzwa kupitia mtandaoni, kutokana na picha za hilo shamba, nilivutiwa sana na nikaona ni bidhaa nzuri kwa ajili ya uwekezaji wa siku za baadaye. Nilichukua simu nikapiga namba ya muuzaji ambayo ilikuwa chini ya picha hizo. Katika mazungumzo, alikiri kweli anauza shamba hilo na halina migogoro yoyote. Ndipo nikamuakikishia, kuwa hilo shamba nitalichukua.

Baada ya kurudi nyumbani, nikashea hizo habari na pacha wangu (wife) na pia nikamuonyesha hilo shamba kupitia laptop yangu. Akaafiki, kweli tulichukue; sasa ikawa ni kupanga nani aende akalikague hilo shamba, ikiwezekana na alipe advance. Kutokana na mimi kutingwa na shughuli, nikamruhusu yeye aende akafanye huo mchakato. Alikubali, na akaanza kujiandaa na safari; kesho yake asubuhi aliondoka na gari ya kwanza kuelekea kwenye huo mkoa wenye shamba. Alikuwa amevaa kisista duu, huku akiwa na cash kama advance ya shamba.

Alipofika kwenye huo mkoa, alitafuta lodge maeneo ya hapo mjini; kwa sababu shamba halikuwa mbali sana na mjini, si zaidi ya km 10 kwa makadirio. Baada ya kufika lodge, alipaki mizigo yake na kuchukua tax mpaka kwenye lile shamba, bahati nzuri alimkuta mwenyeji wake (muuzaji). Baada ya kulikagua, wakaafikiana kesho watakutana na serikali ya kijiji kujiridhisha kama hilo shamba ni la kwake. Kila kilichokuwa kinaendelea,tulikuwa tunawasiliana ili ikienda tofauti tujue pa kuanzia.

Baada ya kurudi lodge, pale kaunta akakutana na mzee mmoja ambaye pia alifikia kwenye hiyo lodge, inasemekana alikuwa anatoka kongo, mazungumzo yao yakawa hivi, 'binti hujambo?', Sijambo shikamoo, 'Nakuona umetoka safari ya mbali umekuja kununua shamba' ndio, 'binti yangu nakushauri usinunue hilo shamba, kwani lina migogoro ya kifamilia', 'pia nakuona umekuja na hela za kulipia, pia naona huko kwenu mama yako anachangamoto za kuumwa' ndio ni kweli. Baada ya hayo mazungumzo waliagana, wakahaidiana watatafutana baadaye.

Ndipo pacha wangu, akanipigia simu na kunieleza kilichojiri na mbaya zaidi katika mazungumzo yake alikuwa anamsapoti yule mzee kwa kuwa alithibitisha mama yake ni mgonjwa na atampatia tiba; nilishikwa na hasira, nikamwambia usikutane na huyo mzee kwanza mpaka nitakapomwambia. Nilipiga simu kwa wazazi wa pacha wangu muda ule ule, kuwaeleza kilichotokea. Nao wakanipa muda niwasubiri baada ya dakika chache.

Kumbe huko kwa wakwe walishikwa na bumbuwazi na kuona si hali ya kawaida, ndipo wakawasiliana na mzee wao wa ukoo, ili kupata ushauri na kujua kinachoendelea. Ilikuwa saa nne usiku, baada ya nusu saa hivi, bibi mkubwa akanipigia simu na kunifokea, 'unataka unipotezee mtoto wangu, unajua nilimpataje kwa uchungu?' nikamuuliza mama nini tatizo, akaniambia, 'huyo mtu sio mtu mzuri amempenda huyo binti na anataka achukue hizo fedha aende naye Nairobi; na anavyoendelea kukaa huko anazidi kubadilika na hatoelewana na wewe, atakutukana na atakuachia watoto ulee; yeye ataondoka na mtu wake; kwa sababu kuna vitu vya asili ameshapandikizwa na huyo mkongo.'

Baada ya kupata hizo habari, mwili ulikuwa kama umeganda ndipo nikampigia simu pacha wangu,' ondoka hapo lodge sasa hivi chukua hata tax nenda sehemu yoyote utakapopata usafiri wa kwenda kwenu, hiyo hela niliyokupa tumia hata yote, cha muhimu ufike kwenu.' Bahati nzuri alinisikiliza na kuondoka haraka sana, usiku kucha alikuwa anasafiri mpaka akafika kwa wazazi wake.

Asubuhi wakampeleka kwa babu yao (mzee wa ukoo), alipofika pale tu; marue marue yakampata na kuanza kulopoka yote yaliyokuwa yanatokea kule ugenini, mpaka mipangilio yote ya kutaka kuondoka na mkongo ili awe mke wake. Baada ya kuongea yote, ndipo akazimia kama nusu saa hivi. Nawapigia simu kuwajulia hali na kutaka kuongea na pacha wangu, wakaniambia pacha bado amezimia.

Baadaye anakuja kushtuka anauliza nimefikaje fikaje hapa; kumbe wakati ule amezimia, hile nafsi au marue rue ya mkongo yalikuwa yanamrudia mkongo. Ndipo mzee akasema, yule mkongo atapata ujumbe wa kilichofanyika,kwa kumzidi ujanja. Na akikupigia simu usipokee. Kweli baada ya dakika chache, mkongo akapiga simu na hakuna aliyepokea. ndipo akatuma meseji nashukuru kwa ulichonifanyia.

Baada ya hapo akarudi nyumbani kwao na baada ya wiki 2 akarudi nyumbani (kwangu); nilimfanyia party ndogo tu, 'aliyepotea amepatikana'. Niliwashukuru sana wazazi wake pamoja na yule mzee; kwa kuokoa uhai wa mtoto wao pamoja na ndoa yangu.

Ndipo nilipojua, wazee ni hazina katika maisha yetu kwa sababu wamepitia mengi; tusiwadharau chochote tulichonacho hasa kipindi hiki cha sikukuu tuwakumbuke.
 
Mwaka 2008 niliona shamba la ekari 23 linatangazwa kuuzwa kupitia mtandaoni, kutokana na picha za hilo shamba, nilivutiwa sana na nikaona ni bidhaa nzuri kwa ajili ya uwekezaji wa siku za baadaye. Nilichukua simu nikapiga namba ya muuzaji ambayo ilikuwa chini ya picha hizo. Katika mazungumzo, alikiri kweli anauza shamba hilo na halina migogoro yoyote. Ndipo nikamuakikishia, kuwa hilo shamba nitalichukua.
Sema mzee nawew ulikosea Sana umamuagizaje mkeo aende sehem ngeni eti Kisa Wew Uko busy na eti anafikia lodge mwenyew, Ila unatakiwa umshukuru Mungu Sana na najua Kuna kitu kikubwa Sana umejifunza
 
Jamaa ni mzito sana kuelewa, kapigwa hela bila kujua
Kabxaa..iv mwanamke ni wa kumpa pesa nyingi tena asafirie umbali hata wa km 20 tu?yaan kosa mwamba alilofanya ni kuanza kumuonesha mkewe ambae anamwita pacha kwamba ndo atahusika na project hyo....yaan hapo hapo alianza kupanga mission namna ya kuichukua hyo hela bila kuacha mazingira yyte ya ushahid nyumaa...na kwel amefanikiwa
 
Mwaka 2008 niliona shamba la ekari 23 linatangazwa kuuzwa kupitia mtandaoni, kutokana na picha za hilo shamba, nilivutiwa sana na nikaona ni bidhaa nzuri kwa ajili ya uwekezaji wa siku za baadaye. Nilichukua simu nikapiga namba ya muuzaji ambayo ilikuwa chini ya picha hizo. Katika mazungumzo, alikiri kweli anauza shamba hilo na halina migogoro yoyote. Ndipo nikamuakikishia, kuwa hilo shamba nitalichukua.

Wazee Ni havina? Nyie washirikina tu! Pia Mzee alimgonga Kama story yako sio chai?

Kwa nini? Kama walikubaliana kuoa a overnight, that means Mkeo alikuwa hajijui.

Kwa maana hiyo Mkongo alim du mke wetu Jaman, Ila utakuja kutubishia.
 
Sehemu ulizo feli.

1.kumuita mkeo pacha....kumuonesha ni jinsi gani unampenda...hii kwa mwanamke itakula kwako.

2.kumuamini mwanamke kupita kiasi...hapa lazima utakujalia kulio Cha mbwa usipo Lia Basi hauta sikia maumivu Wala sauti za watu Wala kuwa na pumnzi mapema Sana.


3.pesa ulizo nazo unazani utakuwa nazo kila siku .

4. Mzee wanaume wote tunawapenda wanawake ila sio kwa hiyo style yako......itakukost.
 
Sehemu ulizo feli.

1.kumuita mkeo pacha....kumuonesha ni jinsi gani unampenda...hii kwa mwanamke itakula kwako.

2.kumuamini mwanamke kupita kiasi...hapa lazima utakujalia kulio Cha mbwa usipo Lia Basi hauta sikia maumivu Wala sauti za watu Wala kuwa na pumnzi mapema Sana.


3.pesa ulizo nazo unazani utakuwa nazo kila siku .

4. Mzee wanaume wote tunawapenda wanawake ila sio kwa hiyo style yako......itakukost.
Fake story

Fekero
 
Shamba sikununua, na sikutaka tena kununua kutokana na hali iliyotokea
Endelea kumpenda mkeo ila trust me atleast once hayo yoteee yalotokea ni movie hakuna cha mkongo wala nini hiyo hela ulipigwa mchezo mkeo aliumaliza na mama yake.

Siku nyingine hakikisha kwenye ishu za maana unaambatana na mkeo.

Wewe si una vipesa? Fanya makeke mcheki kijana mmoja wa mtandao husika laini anayotumia mkeo.ukweli wote utaupata.hakikisha ni siri usimwaribia kijana wa watu kazi.

Ila nilichogundua mkeo ni ka gaidi kazoefu yawezekana ana laini ya siri ilo nalo kuwa nalo makini.

Kama una vijisenti fanya nilichokwambia.

Afu wewe mzembe sana hiyo ishu yote imetokea bila wewe unasikiliza tu kwa simu mpaka mkeo anarudi kwako na wewe umerelux? Wenda nakupotosha ila hizi familiya mnazooa unakuta mama na binti yake ni wale wale.siku zote ni kupanga ujinga ujinga.

Narudia tena hakikisha unafatilia hili swala. Zawadi za xmass wewe watumie tu hao wazee wezi utalipwa mbinguni.
 
Back
Top Bottom