Hapana
mpondamali yuko katika nyakati ngumu kuliko kipindi chochote kile, anatakiwa achukue uamuzi mgumu sasa was kuwawajibisha wale wote waliohusishwa kwenye kashfa ya IPTL/ESCROW, lakini wakati huohuo familia yake ikitajwatajwa kuhusika na hii kashfa
Kuna mtifuaano unaendelea ndani ya chama chake maamuzi yoyote atakayochukua yatakuwa na athari kwa ccm, na hapa ishu ya urais mwakani ikihusishwa kwa karibu mno kutokana na maamuzi atakayochukua
Katiba bado haijapigiwa kura ya ndio na kwa hali ilivyo haitaungwa mkono na wananchi walio wengi
UKAWA unatishia uhai wa ccm kwa kiwango cha kutisha na kama kuna kitu ccm inaogopa ni kusikia kuwa UKAWA wanaweza kuchukua nchi kwa kuibwaga ccm kwenye uchaguzi mkuu mwakani
Jk ana hali ngumu kwasasa anaomba kwa miungu yote mambo haya yatokee
-atakaowawajibisha wakubali kuachia ngazi na kukaa kimya ili kumlinda/ kukilinda chama
-katiba pendekezwa ipigiwe kura ya ndio
-UKAWA/CHADEMA visambaratike kabla ya uchaguzi mkuu mwakani
- wote waliopata mgao was escrow wakubali kurudisha pesa yote kimyakimya na bila masharti
Anaomba mambo mengi yatokee kwasasa ambayo si rahisi kuyaandika yote hapa