Pendo amekosa tu kujitambua na kujiamini. Ukiwa kama mshauri wake msaidie ajitambue kuwa Clement hamfai, hastahili kuwa naye na sie wa hadhi yake kimaadili na hata kimapenzi. Kitendo cha Clement kumshauri tu kuitoa ile mimba ilikuwa ni dalili tosha kuwa Clement hakuwa amedhamiria kuishi naye kama mpenzi wake. Mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na nia angemwambia imeshatokea, twende kwa wazazi tukaji'shtaki', tuombe msamaha tupewe Baraka ya kuwa mwili mmoja tulee mwanetu. Lakini kwa kuwa Clement hakuwa amempenda kwa dhati ndio maana alimwambia akaitoe. Pili mwambie Pendo kuwa yeye ana bahati kuwa MUNGU amemwonyesha mapema kuwa Clement siye, ingekuwa vipi kama angeolewa naye kasha Clement akamletea mwanamke mwingine ndani na kuanza kuishi naye? Au angemtesa kimapenzi? Mwisho mwambie Pendo aamke Clement siyo wake, wake yupo na anavyozidi kumfuata Clement ndivyo Clement anavyozidi kumdharau na anaweza hata kumtake for his advantage ili tu ajifurahishe. Na pia kwa kumfuata fuata Clement na kulilia asipopendwa hajitendei haki yeye na nafsi yake. Mdedicatie wimbo wa Serebuka wa Mwasiti
Pendo alimaliza elimu ya secondary, still job less.
Ila mwisho wa siku sie wanawake ndio huwa tunaishia kuwa victims.........
Ni bora kujua nini unataka katika maisha
unahisi kwanini mabinti waliosoma kuanzia 2008 hawajui? ni elimu haitolewi ipasavyo au ni uvivu wa kufatilia haya mambo? hivi lakini kama unatoka na kitoto cha secondary unashindwaje kuwa mwongozo wake? mnawaza kuto.mba tu na kuchapa lapa???
Hao ninao kueleza ni wale ambao wameshamaliza form 6 na wengine wapo vyuo vikuu, Tatizo lenu haswa kwa watu ambao hawakusoma masomo ya science 0-level hampendi kusoma biolojia ndilp tatizo kubwa kwenu, unakuta mkiulizwa hata maswali marahisi tu mnashindwa lakini kila simu za google na kuangalia ngono na mambo ya udaku mnazo. Mnadhani hapo nani alaumiwe mwanaume?
hiyo mimba iliingia yenyewe!!!!!!!!!!!
Mie nilipiga mimba mke wangu b4 marriage. Nakumbuka nilimshauri kuitoa akagoma kata kata. Hakuwa tayari kuua just kutunza heshima kwa wazazi wetu. Kitendo cha yeye kutoafik kutoa mimba, ilikuwa ni ishara ya upendo wake kwangu. Nilimpokea kwa Mikono miwili, tukatunza ujauzito hadi akajifungua. Ndipo nikajisalimisha, nikapigwa fain, nikalipa na kulipa mahali na nikafunga naye ndoa.
Mwanamke anayekubali kutoa mimba, ni mwuuaji, siku ukimkera hata wewe atakuua tu. Hana huruma
wewe ukome, nitoe huko kabisaa. ukome tena.