Amoxlin
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 3,782
- 4,118
Habari wana JF,
Kuna imani imetanda miongoni mwa watu kwamba ukioa mwanamke bikira ni vigumu kusalitiwa (mwanamke huyo kuchepuka).
Mwaka 1998 nilihudhuria ndoa ya jirani yangu hapa mtaani ambapo alinihakikishia kwamba yeye ndie wa kwanza kukutana na mke wake kimwili.
Miaka ilisonga na ilipofikia mwaka 2013 jirani yangu huyu aliposafiri kikazi katika mkoa jirani mambo yalianza kubadilika ambapo mpiga kinanda wa kanisani alianza kumnyemelea mke wa jirani na hatimae kufanikiwa kuvunja amri ya 6 katika kitanda cha mmewe.
Siri hii ilifichuka baada ya watoto kumwambia baba yao kwamba anaposafiri huja baba mwingine na hulala chumbani kwake.
Mama jirani alikiri kosa na maisha yakaendelea kama kawaida ila katika hali isiyotazamiwa mama jirani kaingia mtegoni tena na sasa anachepuka na boss flani ambapo mitego imeshategwa inasubiriwa kunasa tu.
Ushauri wangu:-
Kuoa mwanamke bikira sio kigezo cha uaminifu katika ndoa ila mambo haya ni tabia ya mtu tu.