Kwani kaka tangu alipokutana na huyo ex na wewe ulivyoreact baada ya kukwambia ameshafanya kitu kama hicho tena? Je kuna kingine ambacho kinaweza kuwa kimeashiria kutokuwa muaminifu?
Kwanza mimi ninaamini kabisa mpaka akwambie wewe ukweli kuwa nilikutana na ex wangu juzi huyu ni mwaminifu sana kwako kwa sababu angeweza kukwambia kuwa hajakutana naye miaka wala hajui alipo. Kaka wanawake huwa tuna tabia ya kupenda kuonekana wasafi so kwa kitendo hicho nampa pongezi wifi kwa kuwa mkweli kwako.
Chunguza kama hakutani naye tena na wala hana dalili ya kutokuwa muaminifu kwako. Kama kosa hilo la kukwambia ukweli ndio doa pekee, please think twice before dumping her kwa kosa hilo
naona kesi umeivutia kwako pekee. Ingawa mwenzi wake anayo haki ya kusikilizwa nadhani tunaweza kujenga picha ya mwanzo wa mahusiano yenu.wakati tupo chuo niliingia kwenye mahusiano na binti mmoja ambaye tulikuwa tunashare baadhi ya masomo (options). Tulianza mahusiano mapema tu, ila siku moja tukiwa mwaka wa pili likizo ndefu mimi nikiwa nimeenda nyumbani-mkoani. Mwenzangu kwao ni hapa DSM akawa anaendelea na mahusiano ya kimapenzi na bwana wake wa zamani. Baada ya likizo kwisha siku moja ikawa tunapiga story kawaida ikatokea tu tukaanza kuongea kuhusu wapenzi wetu wa zamani. Sijui ilikuwaje tukaanza kuulizana siku za mwisho kukutana nao. SIKUAMINI PALE GIRLFRIEND WANGU ALIPONIAMBIA KUWA NI MWEZI WA SABA, kumbuka hicho kumbuka ndio tulikuwa likizo na tulikuwa tunawasiliana sana hata kuandikiana meseji za TAKE CARE EEH! Nilipomuuliza akaniambia ni kwasababu anajua hatoishi naye, kwahiyo haina athari zozote. Sio siri iliniuma sana ila kwakuwa nilikuwa nampenda tuliendelea hivyo mpaka tulivyograduate. Sasa umefika wakati wa kuanza kufikiria ndoa napata shida kweli kama nitaweza kuishi na mwanamke huyu kwa kuwa yale maumivu bado yapo moyoni mwangu bado. Ingawa yeye anasisitiza kuwa ameshaacha kukutana naye toka kipindi kile kutokana na reaction niliyoonyesha.
Naombeni mnisaidie
Nifanye nini kwani bado inaniuma sana hasa nikikumbuka wakati mimi niko likizo tulikvyokuwa tunawsiliana PLEASE TAKE CARE MY LOVE kumbe mwenzangu inawezekana hata wakati anaandika hizo messeji alikuwa kwenye kifua cha huyo mwanamume!
nashukuru lakini hawa ni watu ambao kwa maelezo yake ni kwamba huyo jamaa wake alikuwa mpangaji wao na mpaka sasa ni mpangaji wao. kwahiyo ni watu ambao kwa kuonana tu ni daily kwa sababu wanakatiza korido moja. Ila tu kwa sasa jamaa kaoa. Ila kilichoniumiza sana ni suala la yeye kupokea michango ya harusi ya huyu bwana kutoka kwa waliokuwa shemeji zake hapo nyuma kabla ya kuwa na mimi. Halafu pia wakati wa graduation huyu bwana alikuwepo na hadi kwenye picha za ukumbini ame-appear, nilivyomuuliza akasema Mama yake ndie alieyemualika kama mpangaji wake. Anway kaalikwa na mama yake kwanini akaacha hiyo picha iwepo kwenye albamu yake ambayo mimi lazima ningeiona. Akakosa jibu.
Ni kweli inaonekana kuwa maelezo yangu yanamkandamiz sana huyu binti, ilo siwezi kulipinga hata kidogo. Lakini nasema yale ambayo ni ya kweli kwa upande wangu pasipo kumkandamiza. Ila kuhusu kumuondoa kwa bwanake wa zamani sio kweli. Mimi wakati namtongoza aliniambia alikuwa hana mtu.
wewe ni mwanaume na unajua au ushawahi kushuhudia namna mbavyo wadada wanavyosaliti mahusiano yao kwa kutamani makuu. Ulihakikisha vipi kama ameachana na huyo switi wake? na pia alikueleza ni lini waliachana and ukafanya comparizoni ya muda kabla ya kumrecruit inn? Na kingine kiwango cha elimu ya bwanake wa kale uliulizia??? maana siku hizi wanawake wengi wakishamzidi mwanaume kielimu basi kibuti kinatembea wanasaka wa kufanana nao kielimu kitu ambacho ni wrong.Ni kweli inaonekana kuwa maelezo yangu yanamkandamiz sana huyu binti, ilo siwezi kulipinga hata kidogo. Lakini nasema yale ambayo ni ya kweli kwa upande wangu pasipo kumkandamiza. Ila kuhusu kumuondoa kwa bwanake wa zamani sio kweli. Mimi wakati namtongoza aliniambia alikuwa hana mtu.